Msanii wa hip hop Bongo ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Mikumi mkoani Morogoro kwa tiketi ya CHADEMA, Joseph Haule a.k.a Prof. Jay ameteugua kitendawili cha ndoa yake kwa kutaja rasmi siku atakayofunga ndoa.
Prof. Jay ambaye leo ametimiza miaka 41 tangu kuzaliwa kwake amefunguka suala hilo katika mahojiano na Planet Bongo ya East Africa Radio yaliyokuwa maalum kwa ajili ya siku yake ya kuzaliwa, na kusema kuwa yeye na mpenzi wake Grace wanataraji kufunga ndoa mwakani (2017) kabla ya mwezi Juni.
Pia Prof Jay ametumia nafasi hiyo kuwashukuru mashabiki wake katika muziki, pamoja na wananchi jimbo la Mikumi kwa sapoti kubwa wanayompa huku akiahidi kuendelea kuwatumikia bila ubaguzi wowote.
Katika hatua nyingine Prof Jay amemzungumzia mkulima mmoja wa jimboni kwake aliyejeruhiwa kwa kupigwa mkuki mdomoni hivi karibuni na kusema kuwa hali yake inaendelea vizuri.