SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 28 Desemba 2016

T media news

Wilfred Zaha Kuchezea Ivory Coast Komba la CAN


Wilfred Zaha alizaliwa Ivory Coast lakini ameiwakilisha Uingereza mara mbili ikiwemo dhidi ya Sweden Novemba 2012 na Scotland mwaka 2013.

Winga wa zamani wa Uingereza anayeichezea klabu ya Crystal Palace, Wilfried Zaha ametajwa katika kikosi cha Ivory kitakachoshiriki Kombe la mataifa bingwa barani Afrika litakaloandaliwa Gaon mwaka ujao.

Hii ni baada ya Zaha kubadili uraia kutoka Uingereza ambapo alilelewa hadi Ivory Coast.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24, alizaliwa Ivory Coast lakini ameiwakilisha Uingereza mara mbili ikiwemo dhidi ya Sweden Novemba 2012 na Scotland mwaka 2013.

Hata hivyo ameruhusiwa kuiwakilisha Ivory Coast kwani mechi hizo zilikuwa ni za kirafiki.

Iwapo atajumuishwa katika kikosi cha mwisho, huenda asishiriki ligi ya Uingereza kwa wiki sita .

Wengine walioitwa ni pamoja na beki wa Manchester United, Eric Bailly na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Salomon Kalou.

Kocha Michel Dussuyer, raia wa Ufaransa anatarajiwa kuongoza kikosi hicho kitakachoingia kambini Abu Dhabi, kuanzia tarehe mbili Januari.

Ivory Coast iko kundi moja na Togo, DR Congo na Morocco.