Apongeza uongozi wa kata YA Ipinda na Vijiji ktk kata hiyo kuchangia upanuzi wa kituo cha Afya
Afurahishwa na uongozi wa Kamati YA Shule YA Ipinda kushirikisha wadau kukarabati madarasa 8 na matundu YA choo 10
Awaonya wanasiasa wanaopinga wananchi kushiriki shughuli za maendeleo
MKuu wa Mkoa wa Mbeya leo amekagua ujenzi wa wodi YA mama na Mtoto, ukarabati wa madarasa nane na ujenzi wa vyoo 10 ktk Shule YA msingi Ipinda kisha kufanya mkutano wa hadhara kwa kusikiliza kero za wananchi katika Kijiji cha Ipinda wilayani KYELA pamoja na mambo mengine amewaomba wananchi kuendelea kushirikiana na serikali ktk ujenzi wa zahanati kila Kijiji, vituo vya Afya kila kata na ujenzi wa miundombinu Ktk Shule ikiwemo madarasa na vyoo
Amewapongeza wananchi , wadau na viongozi wa kata ya Ipinda kwa kushirikiana kukarabati madarasa, ujenzi wa vyoo na upanuzi wa kituo cha Afya
Amesema serikali peke yake haiwezi kufanya kila kitu bali kwa kushirikiana na wananchi na wadau wa maendeleo malengo YA kuwa na zahanati, vituo vya Afya na miundombinu YA Shule itawezekana
Amewaonya wanasiasa na kuwataka kuacha mara moja kuwashawishi wananchi kutoshiriki shughuli za maendeleo