Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ameitaka CCM iache kujidanganya kuwa haiwezi kuondoka madarakani akiitaka iangalie alama za nyakati hasa mabadiliko ya uongozi yanayotokea kwingineko duniani.
Hata hivyo, Lowassa ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA amesema unahitajika muungano wa dhati wa vyama na uliopangiliwa vizuri katika juhudi za kuiondoa CCM madarakani.
Lowassa alisema hayo alipoombwa na mwandishi wa habari hizi kutoa tathmini ya maisha yake ya kisiasa mwaka mmoja na nusu tangu alipojiondoa CCM na kujiunga na CHADEMA ambako aliteuliwa kuwa mgombea urais wa chama hicho akiwakilisha muungano wa vyama vinne – CHADEMA, CUF, NCCR - Mageuzi na NLD – Iliopewa jina la Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).
Chanzo: Gazeti la Mwananchi