Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia 2017

Manchester United yapata matokeo mabovu

Picha
Klabu ya Manchester United bado imeendelea kupata matokeo mabovu kwenye Ligi Kuu soka England baada ya jana kulazimishwa sare ya bila kufungana dhidi ya klabu ya Southampton. Kwa matokeo hayo Manchester United ambayo ilikuwa nafasi ya pili kwa muda mrefu kwenye msimamo wa EPL imeshuka hadi nafasi ya tatu baada ya Chelsea jana kupata ushindi mnono. Wakati hayo yakitokea Manchester United imepata janga lingine kubwa zaidi kwa kuumia mchezaji wao tegemezi, Paul Pogba jana kwenye mchezo huo. Pia kupitia mtandao wa klabu hiyo umethibitisha kuwa mshambuliaji wao Zlatan Ibrahimović kuwa atakuwa nje ya uwanja kwa mwezi mmoja kuanzia jana. Matokeo hayo yanaifanya Manchester United kupata sare tatu mfululizo kwenye EPL na kupoteza mechi moja ya kombe la EFL. Matokeo mengine ya ya mechi za jana za EPL ni kama ifuatavyo

Kamishna wa Magereza azungumzia msongamano wa wafungwa

Picha
Kamishna Jenerali wa Magereza, Juma Malewa amesema jeshi hilo linakabiliwa na msongamano wa wafungwa kutokana na kuongezeka vitendo vya uhalifu na makosa ya kijinai. Dk Malewa amesema hayo leo Jumapili Desemba 31,2017 katika Gereza Kuu la Mkoa wa Mbeya akiwa ziarani kukagua magereza na kuzungumza na askari wa jeshi hilo. Amesema msongamano unatokana na majengo yanayotumika kuwahifadhi wafungwa ni yaliyojengwa enzi za mkoloni. Hata hivyo, amesema wamejipanga kuendelea kuongeza idadi ya magereza kwa kila wilaya licha ya baadhi ya wananchi kutopendezewa na jambo hilo. “Wakati tunapata Uhuru watu tulikuwa kama 10 milioni, hadi sasa majengo kama yameongezeka basi ni mawili lakini ni yaleyale; pia kuna makosa mapya ya uhalifu yameongeza ambayo zamani hayakuwepo,” amesema. Amesema makosa ya dawa za kulevya na utakatishaji fedha yamejitokeza; huku mauaji yakiongezeka. Pia, amesema msongamano unasababishwa na kesi zinavyoendeshwa mahakamani ambako zipo zinazochukua muda mrefu ...

Kanisa Katoliki yaitisha maandamano ya amani Kongo

Picha
Kuna wasi wasi wa kukosekana utulivu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inayokabiliwa kwa sasa na mgogoro wa kisiasa kufuatia kanisa Katoliki lenye ushawishi mkubwa nchini humo kuitisha maandamano ya amani. Kabila ambaye waandaaji wa maandamano hayo wanamtaka atamke wazi kuwa hatawania muhula wa tatu wa uongozi, amekuwa madarakani tangu mwaka 2001 wakati aliposhika madaraka ya urais baada ya baba yake Laurent Kabila kuuawa. Kabila alikataa kujiuzulu bada ya kumalizika  kipindi chake cha pili na cha mwisho  Desemba 2016 hatua iliyosababisha maandamano pamoja na machafuko. Tangu kipindi hicho maanadamano yamekuwa yakipigwa marufuku licha ya wakati mwingine waandamanaji kukiuka amri ya serikali na kuendelea na maandamano hali ambayo pia imekuwa ikisababisha umwagaji wa damu. Hatua ya kanisa Katoliki kuitisha maandamano  ya leo Jumapili licha ya serikali kuyazuia yasifanyike inawafanya baadhi ya wachambuzi kuonya juu ya uwezekano wa kukosekana utulivu. “Maand...

Babu Seya Wako Wapi na Papii Kocha?

Picha
Toka Babu Seya na Mtoto wake watoke jela Watu tulitegemea tutasikia wakifanya mengi na pengine kuimba au kufanya matamasha na appearance nyingi ili kukata kiu ya mashabiki zao ambao wamewamiss muda mrefu lakini kinyume chake ..Babu Seya na Mwanamwe toka Watoke wamekuwa kimya na kujichimbia kabisa...Je wameamua kuacha mziki au wanaandaa mabomu mapya?

Bongo Fleva inaenda Mbali, Diamond Anaipushi Sana – Shilole

Picha
Msanii wa Bongo Fleva, Shilole amedai kuwa muziki wa Bongo Fleva kwa sasa unakua kwa kasi duniani na kuufanya muziki huo kubadilisha maisha ya Wasanii huku akimtaja Diamond Platnumz kama moja ya wasanii wanaopambana kukuza muziki huo. Shilole amesema kuwa kitendo cha Diamond Platnumz kufanya kolabo na Wasanii wakubwa wa nje ya bara la Afrika kimefanya muziki wa Bongo Fleva kukua kwa kasi. “Bongo Fleva inaenda mbali sana, hususani! tuseme ukweli Diamond anaipushi sana Bongo Fleva yetu, sikutegemea kama  Diamond siku moja atafanya ngoma na Rick Ross sijui na akina Ne-Yo nilikuwa nikiona tuu tutafika huku? lakini tumeanza kujaribu na tunafika..Natamani na mimi siku moja nifanye kazi na Nicki Minaj.“amesema Shilole kwenye mahojiano yake na BBC Swahili. Shilole ambaye yupo nchini Uingereza alikoenda kutumbuiza kwenye show maalumu amesema kuwa show za nje ya nchi siku hizi zinalipa tofauti na zamani.

Rais Magufuli Asali Ibada Ya Familia Takatifu Katika Kanisa La Mtakatifu Petro Jijini Dar Es Salaam.

Picha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishukuru mara baada ya kushiriki Sakramenti Takatifu katika Ibada ya Jumapili ya  Familia Takatifu iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na waumini wa Kanisa la Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam mara baada ya Ibada ya jumapili ya  Familia Takatifu katika Kanisa hilo jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na waumini wa Kanisa la Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam mara baada ya Ibada ya jumapili ya  Familia Takatifu katika Kanisa hilo jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na waumini wengine wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay wakishiriki Ibada ya ...

Waziri Mkuu amwagiza Ofisa madini aitishe kikao na wananchi.......Ni baada ya kupokea mabango ya wananchi wakidai kunyanyaswa

Picha
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Kanda ya Kusini, Bw. Ogesa Charles Tale afike eneo la mgodi wa dhahabu wa Namumgo na kuitisha kikao cha wananchi leo (Jumapili) saa 4 asubuhi. “Sasa hivi natoka kwenda Matambare, twende wote, lakini kesho (leo) saa 4 asubuhi uje hapa Namungo, uitishe mkutano wa hadhara na uwasikilize hawa wachimbaji wadogo na kisha uniletee maelezo ofisini kwangu,” alisema. Ametoa agizo hilo jana mchana (Jumamosi, Desemba 30, 2017), wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Namungo, wilayani Ruangwa baada ya kupokea mabango mawili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo. Waziri Mkuu yuko kwenye mapumziko ya mwisho wa mwaka, na ameamua kukagua miradi ya maji, ujenzi wa zahanati na kuzungumza na wananchi katika wilaya hii. Waziri Mkuu alisema Serikali ya awamu ya tano imejikita kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi na alipomuuliza afisa huyo kama ameshawahi kupata nafasi ya kuwasikiliza wachimbaji...

Mjumbe Wa Halmashauri Kuu Ya Ccm Mkoa Wa Arusha Robert Pjn Kaseko Amjibu Askofu Zacharia Kakobe.

Picha
Askofu Kakobe Umekosea sana kuigeuza nyumba ya Ibada takatifu na kuifanya kama Uwanja wa kuongelea mambo yahusuyo Siasa. Ni kweli  kila mtanzania  ana Uhuru wa kuongea na kutoa maoni yake lakini pia tufahamu wakati sahihi na mahala Sahihi pa kuwasilisha jambo fulani na wewe  kama Kiongozi na Mtumishi wa Mungu  tambua  MUKTADHA ama Ujumbe wako na Mazingira ya kuongelea jambo fulani, haikuwa mahala sahihi kuongelea mambo yahusuyo Siasa tena unayemlenga hayumo humo kanisani. Kwa Uelewa wangu mdogo, kanisa kama eneo ama jengo ni mahala ambapo watu hukusanyika ili kupewa mahubiri/ mafunzo ya maneno matakatifu ya Mungu. Kanisani ni sehemu takatifu ya Kumwabudu Mungu, ni sehemu ya kuwaambia waumini waliokusanyika humo maovu yao ili  wayaache na kumrudia Mungu. Sasa huwezi kuacha kuhubiri habari za  Yesu Kristo ukaanza kuwahubiria  waumini habari za Siasa na wakati wamekuja kujifunza neno la Mungu.   Tukumbuke  Kuna namna nzuri ya kuwasi...

Kanusho la taarifa inayosambazwa kumuhusu Makamu wa Rais

Picha
Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakanusha tangazo linalosambaa katika Mitandao ya Kijamii linalomhusisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  kuwa atashiriki zoezi la kupanda miti kwenye Chuo Kikuu Cha Dodoma siku ya tarehe 1-1-2018.  Ofisi ya Makamu wa Rais inapenda kuujulisha umma kuwa tangazo hilo si la kweli na Makamu wa Rais hana ratiba ya kupanda miti kwenye chuo hicho kwa tarehe iliyotajwa. Ikumbukwe kuwa siku ya tarehe 15-12-2017 wakati wa hafla ya kuhamia Makao Makuu ya Nchi, Makamu wa Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan alitangaza kampeni ya kupanda miti Dodoma ambayo itaratibiwa na Ofisi yake . Ofisi ya Makamu wa Rais inawataka Wananchi kuzingatia matangazo, taarifa na ratiba zitakazotolewa na Ofisi yake kuhusu programu ya upandaji miti Dodoma.  Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dodoma  30 Desemba,

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya Disemba 31

Picha

KWANINI Wanawake Wanapenda Wanaume Masharobaro aka Bad Boys

Picha
Wanawake kuchagua wanaume masharobaro aka badboys kuwaliko wanaume wa kawaida si jambo geni na hutokea mara kwa mara. -aidha katika vyuo, vilabuni, sinema, maktabani ama sehemu yeyote ile. Wanaume masharobaro, kama wanaume wengine, wao pia wanamaumbo ya kila aina, shepu na mvutio wa kijinsia. Kama wewe ni mwanamume wa kawaida ambaye humaliza wa mwisho ama ushawahi kupoteza mpenzi wako kwa sharobaro fulani, hapo chini kuna nadharia ambazo zitasaidia kueleza kwa nini  wanawake wanapenda sana kuvutiwa na wanaume masharobaro. 1. Hamu ya kufuata Kufuata kitu ambacho unakipenda huwa kuna msisimko fulani mtu hupata. Lakini msisimko zaidi hutokea wakati ambapo mtu anajaribu kufuata mtu ambaye hataki kujulikana mienendo yake ya kimaisha, kufuatwa ama kueleweka kimaisha. Haya ndio maisha anayoishi mwanamume sharobaro. Wanawake wanapenda sana wanaume ambao hawaeleweki kimaisha (yaani hawatambuliki) ama kutaka kujua maisha yao. Na wewe kama mwanamume unataka kutumia huu udhaifu kwa manufaa ...

Lisome hapa agizo la Waziri Mkuu kwa Mawaziri ambao bado wanaishi Dar es Salaam

Picha
Disemba 12 mwaka huu, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliandika barua kwenda kwa Mawaziri, Manaibu Waziri, Wakurugenzi na watumishi wengine wa serikali ambao hawakai kwenye vituo vyao vya kazi kwa mujibu wa sheria, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitoa agizo hilo kufuatia kuwapo kwa mawaziri na viongozi wengine ambao wamepangiwa kuhamia Dodoma, kuendelea kukaa Dar es Salaam, badala ya vituo vyao. Isome hapa chini barua hiyo;

Habari Mbaya: Ofisa wa polisi ajiua kwa kujinyonga

Picha
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Kituo cha Nansio wilayani Ukerewe, John Kalongola amejinyonga kwa kipande cha chandarua nyumbani kwake. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema mwili wa askari huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe. Amesema baada ya uchunguzi na utaratibu kukamilika mwili utasafirishwa kwa mazishi mkoani Iringa. Kamanda Msangi amesema mwili huo ulibainika baada ya harufu kutoka ndani ya nyumba yake na mlango ulipovunjwa ulikutwa ukining’inia. Mwili wa askari huo uligunduliwa jana Ijumaa Desemba 29,2017. Amesema kipande cha chandarua kilifungwa juu ya dari.

Waziri Njemba atoa agizo hili kwa wasiokuwa na kitambulisho cha Taifa

Picha
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dr. Mwigulu Nchemba akiwa kwenye ziara ya kikazi mkoani Ruvuma ameagiza kila mtanzania kujiandikisha kupata kitambulisho cha taifa kwakuwa sio jambo la hiari bali ni lazima kwa kila Mtanzania aliyeko ndani ya mipaka ya nchi kutambuliwa. “Hili zoezi la vitambulisho vya utaifa ni lalazima kwa kila mtanzania aliye nchini, ni kosa kubwa kama wewe ni raia ukaamua kukaidi ikiwa Rais wetu Magufuli ameamua kutoa vitambulisho hivyo bure bila malipo yoyote”–Dr Nchemba “Hili ni jambo la Nchi na ni kubwa hivyo tusililinganishe na jambo lingine lolote, baada ya mchakato huu kuisha tukamkuta mtu hana kitambulisho maelezo yake yatakuwa ni magumu kueleweka kama kweli yeye ni mtanzania halali” –Dr Nchemba

TRA kumchunguza Askofu Kakobe baada ya kumsikia akisema ana hela kuliko Serikali

Picha
Siku chache baada ya kiongozi wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship Askofu Zachary  Kakobe kusema kuwa ana fedha nyingi kuliko Serikali, Mamlaka ya Mapato nchini TRA imejipanga kuanza kufuatilia ulipaji wake wa kodi. Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere amesema mamlaka yake imeipokea kwa furaha kauli ya Askofu Kakobe na inataka kujiridhisha vyanzo vya utajiri huo. Kichere amesema TRA inafahamu kuwa shughuli za kidini hazitozwi kodi lakini inataka kufahamu kama fedha hizo za Askofu Kakobe zinatokana na sadaka pekee au kuna shughuli nyingine za kiuchumi. "Tumefuatilia hakuna kumbukumbu za Askofu Kakobe kulipa kodi, sasa tumeona tumfuate maofisa wetu wakajiridhishe kama fedha hizo anazozizungumzia zinatokana na sadaka," "Na kama hana shughuli zozote za kiuchumi ikiwa ina maana utajiri huo unatokana na sadaka ni jambo la kushtua kidogo lakini sisi tutaishia hapo," Amesema katika taarifa za mamlaka hiyo wapo watu wengi wenye fedha nyingi na kumbukumbu zao za k...

Benki Kuu ( BOT ) yaiagiza Airtel kupeleka taarifa zake za Fedha tangu mwaka 2000

Picha
Kufuatia sakata la umiliki wa kampuni ya mawasiliano ya Airtel, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Disemba 28, 2017 iliziandikia benki zote na taasisi za kifedha ambazo zimekuwa zikisimamia akaunti za iliyokuwa Celtel, Zain au Airtel kuwasilisha taarifa hizo. BoT imezitaka taasisi hizo ama benki kueleza kama zimewahi kuendesha ama zinaendesha akaunti zinazohusiana na kampuni tajwa. Aidha, taasisi zote ambazo zitakuwa zina akaunti za kampuni hiyo tajwa, zimetakiwa kuwasilisha jina la akaunti, namba ya akaunti, aina ya fedha zilizomo kwenye akaunti na kiwango cha mwisho kilichokuwemo kwenye akaunti hadi Disemba 27, 2017. Taarifa za akaunti hizo zinazotakiwa kuwasilishwa ni kaunzia Januari 1, 2000 hadi Disemba 27, 2017. Taarifa zinazotakiwa kuwasilisha zinatakiwa kuwa katika nakala ngumu (hardcopy) na nakala teke (soft copy) na zilitakiwa kuwasilishwa  jana saa 5 asubuhi.

Waziri Jafo Avitaka Vituo Vyote Vya Afya Kutengeneza Bustani Za Kupumzikia!

Picha
Nteghenjwa Hosseah, TAMISEMI. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amevitaka vituo vyote vya Afya Nchini sambamba na hospital za Wilaya kutengeneza bustani ya kupumzikia kwa wagonjwa wanaosubiria matibabu katika maeneo hayo. Waziri jafo ameyasema hayo wakati akikagua Ujenzi wa miundombinu ya Afya katika Kituo cha Afya Makole kilichopo Manispaa ya Dodoma na kuutaka uongozi wa Kituo hicho kutenegenza bustani ya kisasa pamoja na kupanda miti ya kutosha ili kutunza matunzingira lakini kupendezesha eneo la hospital. “Hili Agizo liende kwa Vituo vyote Nchini pamoja na Hospital za Wilaya zilizoko chini ya TAMISEMI kuhakikisha wanaekeleza maelekezo haya katika ameneo yote nataka hospital iwe sehemu ya kupa faraja mgonjwa kwa kupata huduma nzuri lakini pia kusubiria huduma hiyo katika maeneo yanayovutia wakati wote” Alisema Waziri Jafo. Akikagua majengo matano yanayojengwa katika Kituo hicho cha Afya na kusimamiwa na TAMISEMI Wazi...