Wengi wetu tunafanya kazi maeneo tofauti tofauti, wakiwemo wanaofanya kazi kwenye maeneo ya jua, wakiwemo wafanyabiashara wanaotembeza vitu njiani na hata wanaouza vitu sokoni ambako hakuna kivuli.
Pia wapo wanaolima au kufanya kazi nyingine kama mafundi ujenzi na hata wajenzi wa miundombinu ya barabarani, ambao muda mrefu huutumia kufanya kazi juani.
Matokeo ya kufanya kazi juani ni ngozi kuungua kwa sababu mionzi ya jua ni sumu, hivyo ngozi inapopata mionzi hiyo, huzalisha kemikali iitwayo Melanin inayosababisha mtu kuwa na ngozi nyeusi au kua na rangi ya kahawia.
Iwapo miale ya jua imekupiga usoni moja kwa moja kwa muda mrefu au kwa Zaidi ya asilimia 70, ngozi yako ya uso itabadilika na kuuwa nyeusi au yenye mabaka ya rangi ya kahawia.
Usihofu, kwani ukigundua tatizo ni rahisi kulipatia tiba, hivyo tumia kipodozi maalum chenye vitamin E, kwani ina uwezo mkubwa wa kuzuia mtu asipigwe na miale ya jua usoni, au kupunguza athari kwa wale waliokwisha haribika.
Iwapo umeathirika na jua usoni, unaweza kutibu tatizo hilo kwa kula vyakula vyenye vitamin E kwa wingi, ambavyo ni kama nafaka ambazo hazija kobolewa, kiini cha yai, mafuta ya soya, karanga na mboga za majani.
Hivyo kama kazi zako muda mrefu ni kwenye mazingira ya jua, ni vyema ujitambue na kuanza kutumia vipodozi vyenye vitamin E na kujikinga kwa kuvaa kofia kubwa kichwani, itakayokusaidia kuzuia miale ya jua isikupate moja kwa moja.
Pia vitamin E husaidia kukua kwa nywele mara mbili ya kiwango cha kawaida. Watu ambao ngozi zao zimeathirika na jua, wanatakiwa kuepuka kukaa juani, bali wanywe maji mengi na kula mboga za majani na matunda kwa wingi, ili kurekebisha tatizo lao.
Pia ni vyema kutambua kwamba miili yetu inahitaji vitu vingi kwa ajili ya kufanya ngozi zetu kuwa nzuri, ambavyo ni pamoja na kulala usingizi wa kutosha, kupata muda wa kupumzika, kufanya mazoezi na kula mlo uliokamilika.