AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA
Na taratibu Amina mfanyakazi wa madam Zena akashika panga alilo kabidhiwa na Olvia Hitler na taratibu akaanza kupiga hatua za taratibu na kisimama nyuma ya Madam Zena na kulinyanyua panga lake juu na kabla hajalishusha mwilini mwa Madama Zena nakiajikuta nikimrukia Madam Zena na sote tukaanguka chini ya kitanda na kumfanya madam Zena kutoa ukelele mmoja wa maumivu makali na akakaa kimya na watu wote nilio waona ndani ya chumba sikuweza kuwaona tena na kujikuta nikianza kuchangajikiwa baada ya kumuona madama Zena akitokwa na damu za puani na mdomoni
ENDELEA
Nikamnyanyua Madam Zena na kumuweka kitandani huku nikihema kisha nikachukua kanga iliyoning’inizwa nyuma ya mlango kisha nikaanza kumfuta Madam Zena damu zinazo mtoka,Nikikiweka kiganja changu kwenye kifua chake na kukuta mapigo yake ya moyo yakienda kama kawaida na kujikuta nikipata matumaini na wasi wasi ukanipungua kwa kiasi kikubwa.Nikakaa pembeni ya Madam Zena na ndani ya dakika 45 madam Zena akapiga chafya kisha akaanza kufumbua macho na tabasamu likaanza kutawala usoni mwangu baada ya madam Zena kufumbua macho yake na kukaa kitako kitandani
“Unajisikiaje mpenzi?”
“Kidogo afadhali”
“Samahani sana kwa kitendo kilicho tokea”
“Kwani Eddy wewe una tatizo gani?”
“Ahaaa ukiwa sawa nitakuambia tatizo langu ila kwa sasa ninakuomba utulie”
“Nitatulia vipi wakati unaonekana kama mtu mwenye mapepo?”
“Sio hivyo ila ukiwa salama nitakuambia”
Nikaanza kujihisi tofauti kwenye viganja vya vidole vyangu vya mkono wa kushoto hii ni baada ya kuto kuiona pete niliyo vishwa na Yudia.Nikasimama huku nikiwa wasiwasi huku nikijitazama kwenye vidole vyangu na nisione kitu cha aina yoyote,
“Unatafuta nini?”
“Kuna pete nilikuwa nayo kidoleni siiioni?”
“Ni pete ya nini?”
“Hiyo pete inanisaidia sana kwenye mambo yangu”
“Ahaa nilikuvua pete hiyo asubuhi wakati ulipo kuwa umelala.....Nilitokea kuipenda sana pete yako”
“Ohooo ipo wapi?”
“Niliweka ndani ya droo ya dreasing table”
Madam Zena akanyanyuka na kufungua droo ya dreasing table akaanza kuitafuta taratibu jambo lililo anza kunipa wasiwasi kwani kipindi nilipo kuwa nayo sikuweza kupata tatizo la aina yoyote ila baada ya kuvuliwa na Madam Zena vitu vya ajabu ajabu vinaanza kujitokeza.Nikanyanyuka kitandani na kwenda alipo madamZena na tukasaidiana kuitafuta
“Kwani wewe uliiweka wapi?”
“Niliiweka humu ndani tuu kwenye hii droo”
“Aaahh sasa atakuwa ameichukua nani?”
“Saijajua.....kwani ina umuhimu sana”
“Tena umuhimu wake ni zaidi ya sana”
Tukaendelea kuitafuta pasipo kuiona kiasi kwamba nikaanza kuchanganyikiwa japo madam Zena analichukulia ni jambo la kawaida sana katika pete hiyo.