Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May amesema kuwa serikali yake ina amini kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa Urusi imehusika katika shambulio la mpelelezi wa zamani wa Urusi, Sergei Skripal na mtoto wake wa kike, lililotokea kusini mwa Uingereza katika mji wa Salisbury.
Amesema kuwa inawezekana tukio hilo limefanywa na Urusi ili kuweza kuichafua Uingereza kwa kushindwa kudhibiti kemikali zake hatari.
“kuna mambo mawili tu yanaweza kuhusika kwa shambulio lilotokea, inawezekana serikali ya Urusi ilikusudia kufanya tukio hili hapa Uingereza, ama imeshindwa kudhibiti silaha hizi hatari za kemikali na hivyo imesababisha imetumiwa na watu wengine” Amesema May
Aidha, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Rex Tillerson ameiunga mkono Uingereza kwa kusema kuwa huenda Urusi inahusika moja kwa moja katika shambulio hilo,
kwa upande wake msemaji wa ikulu ya Marekani, Sarah Sanders ametoa pole kwa raia wa Uingereza bila kuunga mkono shutuma ya Uingereza dhidi ya Urusi.
Hata hivyo, mbunge kutoka chama tawala nchini Urusi , Vitaly Milonov amesema kuwa shambulio hilo dhidi ya mpelelezi wa zamani ni mbinu iliyotumika kuihusisha Urusi na si vinginevyo.