Babu Seya na mwanawe wajiandaa kwenda DRC

Wasanii Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanae Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ wanatarajia kwenda kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kwa ajili ya mapumziko, na baada ya hapo watarejea nchini na kuweza kuzungumza na mshabiki wao.

Hayo yamesemwa na rafiki wa karibu wa familia ya Nguza, mwanamuziki nguli, Kikumba Mwanza Mpango (King Kikii) katika mahojiano na kituo cha Azam Tv ambapo alieleza watakwenda kwa familia yao na hapo baadae ndio mambo ya kazi yatafuata.

King Kikii amesema kuwa wasanii hao wanatakiwa kwenda DRC kutembelea kaburi la mama mzazi ili kutimiza mila. Mama alifariki wakati wao wakiwa gerezani.

Alipoulizwa kuhusu ahadi ya kuonana na mashabiki waliyokuwa wamesema ingetelelezwa baada ya wiki mbili, King Kikii alifafanua kwamba, ni kweli walitoa ahadi hiyo, lakini kwa sasa wasanii hao wanatakiwa kukamilisha kwanza masuala ya kifamilia yaliyopo mbele yao.

Aidha, amesema kwamba wasanii hao wanaangalia uwezekano uliopo wa kuonana na Rais Dkt Magufuli ili kumshukuru kabla hawajaondoka kwenda DRC.

Wasanii hao wawili waliachiwa Disemba 9 mwaka huu kwa msamaha wa Rais ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa Tanzania.

Familia ya Nguza ilikuwa imehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kukutwa na hatia ya kuwanajisi watoto kumi ambapo hukumu hiyo ilitolewa mwaka 2004.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: UTAMU WA MADAM JESCA

Simulizi; MTOTO WA BOSS WANGU

SIMULIZI FUPI: UCHI WANGU UMENIPONZA