Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inakusudia kufanya mabadiliko ya viwango vya gharama halisi vya maingiliano baina ya mitando ya simu nchini vtakavyotumika kuanzia mwaka 2018 hadi mwaka 2022.
Katika taarifa iliyotolewa na TCRA mapema mwezi huu, ili waalika wadau wa mawasiliano na watanzania kwa ujumla kuhuduria katika mkutano huu wa wazi ulifanyika tarehe 12 Desemba, katika Ofisi za TCRA zilizopo Mawasiliano Towers, Ghorofa ya Tatu, kwa ajili ya kutoa maoni yao.
Viwango vya sasa vinavyotumika ambavyo ni shilingi 26.96 kwa dakika, vinaishia Disemba 31, 2017. Viwango hivyo vilitokana na
uamuzi uliofanywa na mamlaka ya masiliano mwaka 2013 baada ya kufanya uchunguzi wa gharama halisi za maingiliano ya mitandao ya simu pamoja na maoni ya wadau.
Viwango vya maingiliano vya gharama halisi baina ya mitandao ya simu vinavyopendekezwa kutumika rasmi kuanzia tarehe 1 Januari 2018 hadi tarehe 31 Desemba 2022 katika Shilingi ya Tanzania ni kama ifuatavyo
Gharama za maingiliano, ni kiasi cha fedha kinacholipwa na kampuni ya simu kwa kuunganishwa au kutumia mtandao mwingine