Aliyekuwa Mkuu wa Majeshi serikali ya Mugabe aapishwa kuwa Makamu wa Rais
Mkuu wa Jeshi la Zimbabwe aliyestaafu hivi karibuni, Jenerali Constantino Guvheya Dominic Nyikadzino Chiwenga ameapishwa kuwa Makamu wa Rais wa nchi hiyo Ikulu jijini Harare leo.
Pamoja nae ameapishwa pia Cde Kembo Mohadi kuwa Makamu wa pili wa Rais wa nchi hiyo.
Novemba 15, Jenerali Chiwenga, alionekana katika Televisheni ya Taifa ya Zimbabwe (ZBC) akitangaza na kusema kuwa Rais Mugabe yuko katika mikono salama na lengo la jeshi halikuwa kuipindua serikali, bali ni kuwashughulikia wale wote walio kinyume na serikali iliyokuwa chini ya uogozi wa Rais Mugabe.
Kitendo hicho cha jeshi kulivamia bunge, kumuweka kizuizini Rais Mugabe pamoja na kukichukua kituo cha matangazo chaZBC kilipelekea kujiuzulu kwa Rais Mugabe aliyekuwa ameiongoza nchi hiyo kwa muda wa miaka 37.
Maoni
Chapisha Maoni