Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti, 2016

BW.GERSON MSIGWA ATHIBITISHWA KUWA MKURUGENZI WA MAWASILIANO IKULU

Picha
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Rais, (Director of Presidential Communication - DPC). Bw. Gerson Partinus Msigwa,aliyethibitishwa leo na Rais Dkt John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemthibitisha Bw. Gerson Partinus Msigwa kuwa Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Rais, (Director of Presidential Communication - DPC). Taarifa iliyotolewa leo Jumatano Agosti 31,2016 na Katibu Mkuu Ikulu Bw. Peter Ilomo imeeleza kuwa Bw. Gerson Partinus Msigwa amethibitishwa kuanzia leo tarehe 31 Agosti, 2016 kushika wadhifa huo. Kabla ya uthibitisho huo, Bw. Gerson Partinus Msigwa alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Rais, katika Ofisi ya Rais Ikulu kuanzia tarehe 17 Novemba, 2015. Jaffar Haniu Kaimu Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi. Dar es Salaam 31 Agosti, 2016

VIONGOZI WA DINI, TAASISI ZA KIRAIA ZASAIDIA CHADEMA KUSITISHA MAANDAMANO YAO YA UKUTA

Picha
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA Mh.Freeman Mbowe, amesitisha shughuli za maandamano zilizokuwa zimepewa jina la (UKUTA) kwa Muda wa mwezi mmoja,kwa kile alichodai baada ya kuombwa na viongozi wa Dini na taasisi Mbalimbali, ambapo maandamano hayo yalitarajiwa kufanyika kesho Septemba Mosi nchi nzima. Viongozi mbalimbali wa kidini pamoja na Taasisi mbalimbali za kiraia hatimaye wamesaidia kutokomeza UKUTA kwa kuuomba uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kuahirisha Oparesheni hiyo iliyopangwa kufanyika Septemba mosi nchi nzima.  Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Makao Makuu ya CHADEMA Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa,  Freeman Mbowe amesema  Viongozi hao wakuu wa kidini wamewaomba na kuwasihi katika vikao mbalimbali walivyokaa pamoja nao na kusema tunaheshimu viongozi hao.  Mbowe amesema wanawapa muda wa wiki mbili au tatu ili waonane na Rais Magufuli kwa lengo la kutafuta suluhu ya kudumu ya mgogoro huu wa kisiasa...

Rais mstaafu wa Kenya Mwai Kibaki aondoka hospitalini

Picha
Rais mstaafu wa Kenya Mwai Kibaki Aliyekuwa  rais wa Kenya Mwai Kibaki, ambaye amekuwa akipokea matibabu nchini Afrika Kusini kwa kipindi cha wiki moja, ameruhusiwa kuondoka hospitalini. Taarifa kutoka kwa familia yake Jumanne ilisema kiongozi huyo wa zamani "yupo katika hali nzuri". Rais mstaafu wa Kenya Kibaki alazwa Afrika Kusini Hata hivyo, ataendelea kukaa nchini Afrika Kusini kwa muda akiendelea kupata nafuu kabla yake kurejea Kenya. Rais Kibaki alifanyiwa upasuaji katika hospitali ya Netcare Sunninghill kuondoa damu iliyokuwa imeganda kwenye mshipa wa shingoni siku chache baada ya kulazwa.

MSANII AFANDE SELE AKAMATWA NA POLISI MOROGORO

Picha
Msanii mkongwe wa muziki kutoka Morogoro, Afande Sele amedai anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Morogoro kwa madai anagawa pesa kwa watu ili kuwashawishi wajitokeze katika maandamano ya UKUTA ambayo yamepigwa marufuku. Rapper huyo ambaye ni mwanasiasa na aligombea ubunge kupitia cha ACT Wazalendo katika uchaguzi uliyopita, amedai yupo mikononi mwa polisi toka jana. “Huku ni kushindwa kama sio kufeli, toka jana nipo mikononi mwa polisi eti naambiwa nimeratibu mkutano wa UKUTA , nimechapisha T-shirt na kugawa fedha ili kesho watu waandamane, pia kuaandaa mkutano maeneo ya Msamvu.,” aliandika Afande Sele kupitia facebook yake. Aliongeza, “Nina zaidi ya mwezi sijakaa maeeneo ya Msamvu zaidi ya kupita nikiwa naelekea mikoani tena nikiwa kwenye gari yangu. Ila hii aibu na fedheha kwa jeshi la polisi, maamuzi ya kukurupuka . Tusubiri,” Hata hivyo Bongo5 inaendelea kufuatilia taarifa rasmi kutoka jeshi la polisi la Morogoro kuhusu kukamatwa kwake.

TANAPA KUTUMIA TUKIO LA KUPATWA KWA JUA KUFUNGUA LANGO LA PILI LA KUINGIA RUAHA NATIONAL PARK.

Picha
Mkuu wa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya ,Reuben Fune akiangalia jua kwa kutumia kifaa maalum ambacho kinachuja mwanga ili usiweze kuathiri macho kifaa hicho kitatumika katika tukio la kupatwa kwa jua linalotarajia kutokea Septemba mosi .Kushoto ni mnajimu Dkt Noorali Jiwaji akimuelekeza namna ya kukitumia.  Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) Pascal Shelutete akizungumza na wanahabari wilayani Mbarali (hawapo pichani) namna ambavyo Tanapa ilivyo jipanga na tukio la kupatwa kwa jua litakalotokea Septemba mosi. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mbarali , Reuben Fune  Mtaalam wa masuala ya anga (Mnajimu) Dkt Noorali Jiwaji akizungumza na waandishi wa habari wilayani Mbarali mkoani Mbeya kuhusu maandalizi na uwepo wa vifaa vya kuangalizia jua wakati wa tukio la kupatwa litakalotokea Septemba Mosi.  Mahema yakiwa yameanza kuwekwa katika eneo la Mpunga Relini ,Rujewa wilayani Mbarali,eneo lililotengwa maalum kwa ajili ya kutizamia tukio la kupatwa kwa jua li...

Ukuta: Upinzani waahirisha maandamano Tanzania

Picha
Image captionViongozi wa upinzani wakati wa kikao na wanahabari Dar es Salaam Muungano wa vyama vya upinzani nchini Tanzania umeahirisha maandamano ya kitaifa ambayo yalikuwa yamepangiwa kufanyika kesho. Viongozi wa upinzani, akiwemo Edward Lowassa wa Chadema, wametangaza hatua hiyo kwenye kikao na wanahabari Dar es Salaam. Wamesema wameahirisha maandamano hayo kwa kipindi cha mwezi mmoja baada ya kusikia ombi la viongozi wa kidini na wadau wengine waliowaomba kukumbatia na kuyapa muda mazungumzo. Viongozi wa chama hicho walikuwa wameitisha maandamano na mikutano ya kisiasa Septemba Mosi kupinga walichosema kuwa ni ukandamizaji unaoendelezwa na serikali. Baada ya mkutano wa kikao cha Kamati Kuu ya chama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mwishoni mwa Julai, viongozi walisema: "Yapo Matukio ambayo yamekua yakifanywa na kukandamiza demokrasia na misingi ikipuuzwa na kudharauliwa." Viongozi wa upinzani Tanzania kuhojiwa zaidi Maafisa wa Chadema wakamatwa Tanzania...

Taarifa Toka IKULU : Rais Magufuli atengua uteuzi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha.

Picha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 31 Agosti, 2016 amemteua Bw. Doto M. James kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango. Kabla ya uteuzi huo Bw. Doto M. James alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango (Sera). Bw. Doto M. James ataapishwa kesho tarehe 01 Septemba, 2016 saa 2:45 Asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam. Kufuatia uteuzi huo aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile atapangiwa kazi nyingine. Gerson Msigwa Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU Dar es Salaam 31 Agosti, 2016

TANGAZO: EQUITY BANK AGENT BUNDA

Picha
TAWFIQ MONEY SERVICE: WAKALA PEKEE WA EQUITY BANK BUNDA TUNATOA HUDUMA ZIFATAZO: -KUFUNGUA  A/C -KUWEKA PESA -KUTOA     PESA -KUTUMA  PESA -KULIPIA ADA ZA SHULE -KULIPIA MALIPO MBALIBALI YA SEREKALI. KUWEKA PESA NA KUTUMA NI BURE KABISA. SIMU NAMBA 0784699901,0756141420            

Hizi Hapa Nafasi za Kazi Zilizotangazwa leo Mitandaoni na Magazetini

Picha
Bonyeza Links Hizi Hapa Chini kusoma zaidi na Kuapply: 1.  Job Opportunities at Ifakara Health Institute (IHI), Apply Before 16 Sep 2016 2.  Job Opportunity at Mohammed Enterprises Tanzania Limited 3.  Job Opportunity at UNDP, Application Deadline 09 Sep 2016 4.  Job Opportunities at Tunakopesha Ltd, Sales Consultants 5.  Job Opportunity at CVPeople Africa, Accountant 6.  Job Opportunities at PSI Tanzania, Application Deadline 24 Sep 2016 Kazi Zingine zaidi Bonyeza HAPA :  www.ajirayako.com

TANGAZO: TAWFIQ MONEY SERVICE WAKALA WA NMB BUNDA

Picha
ANAPATIKANA BARABARA YA BOMANI MKABALA NA STENDI YA ZAMANI TUNATOA HUDUMA ZIFATAZO: -KUWEKA PESA -KUTOA     PESA  -KUTUMA  PESA -KULIPIA ADA ZA SHULE -KULIPIA MALIPO MBALIBALI YA SEREKALI. KUWEKA PESA NA KUTUMA NI BURE KABISA. SIMU NAMBA 0784699901,0756141420            

TANGAZO:CRIMA BARBER SHOP NOW OPEN

Picha
Crima barber shop of products and services for Men, Women and Children. CRIMA  Barbershop, men Hair Salon, Kids Salon, Facial, Pedicure, Manicure, Massage, Hot Stone Therapy, Body Scrub, Waxing, Haircut, Hair Plaiting/Braiding, Weddings, Makeup, Beauty Shop Contact us +255 745422462 +255  Location Musoma road, opposite reza hotel Area: BUNDA MARA  

Watalii kutoka nje ya nchi kushuhudia kupatwa jua Mbeya

Picha
WAGENI  mbalimbali wa ndani na nje ya nchi wameanza kuwasili mkoani hapa kushuhudia tukio la kupatwa kwa jua katika eneo la Rujewa wilayani Mbarali. Tukio hilo la historia ambalo kwa mara ya mwisho linatajwa na wataalamu kwamba lilitokea mwaka 1977, linatarajia kutokea tena Septemba mosi mwaka huu nchini Tanzania ikiwa ni mara ya kwanza. Akizungumzia tukio hilo jana, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amosi Makalla, alisema   Serikali imeanza kupokea wageni mbalimbali kutoka ndani ya nchi na nje. “Baadhi ya wageni  kutoka nje ya nchi ambao wamewasili tayari ni kutoka Ujerumani, wengine watawasili leo kutoka Zambia na Malawi, lakini wageni wa ndani ni wengi,” alisema. Alisema  kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wataalamu, inasemekana tukio la kupatwa kwa jua litatokea katika maeneo mawili tofauti katika  mikoa miwili ya Nyanda za Juu Kusini. Alisema  mkoani Mbeya, tukio hilo litatokea Rujewa wilayani Mbarali  na   mkoani Njombe ni katika eneo l...

Polisi wapiga kambi Chadema

Picha
NI mwendo  wa doria. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya askari polisi kulazimika kupiga kambi katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), zilizopo Mtaa wa Ufipa, Dar es Salaam. Polisi hao tangu jana asubuhi walikuwa wakifanya doria katika eneo hilo huku wengine wakizingira ofisi za chama hicho wakiwa wamevaa kiraia. Kutokana na hali hiyo, MTANZANIA ilituma timu ya waandishi ambao kutwa nzima ya jana waliwashuhudia askari polisi wakiwa nje ya ofisi za chama hicho na wengine wakiwa ndani ya magari ya doria. Hatua hiyo ilionekana kuzua taharuki kwa baadhi ya wanachama na viongozi wa juu wa chama hicho ambao walijikuta wakishindwa kufanya kikao cha dharura cha Kamati Kuu kwa hofu ya kuzuka vurugu. Ilipotimu saa tano asubuhi, timu ya walinzi wa Chadema ‘Red Brigade’ waliongezeka na kusimama nje ya ofisi za makao makuu huku wakionekana kuwa tayari kwa lolote, ikiwamo kujihami kwa kuwalinda viongozi wao; mawaziri wakuu wa zamani, Edward Lowa...

CHRIS BROWN AKAMATWA NA POLISI BAADA YA UCHUNGUZI KUMALIZIKA

Picha
Bad Newz kwa Chris Brown, kikosi cha polisi cha LAPD kimemkata Chris Brown baada ya kukutwa na silaha za mangamizi. Chris Brown alikumbana na mkasa huo ni pale aliporipotiwa kumtishia mwanamke mmoja aliyefahamika kama Baylee Curran alipo mripoti Chris Brown baada ya Chris Brown na rafiki zake ambao walikuwepo ndani walimtishia silaha wakimtaka kusaini makubaliano ambayo hayakuwa mazuri kwake ndipo mwanadada huyo alipoamua kukimbia na kuwapigia simu polisi. Kupitia taarifa iliyotolewa na ABC imesema kwamba Chris Brown amekamatwa na polisi hao ni pale aliporuhusu kuingia nao ndani kwa ajili ya kumkagua ndipo wakamkuta na Silaha hizo za maangamizi. Tukio zima lilianza asubuhi ya jana Jumanne pale polisi walipovamia na kuzunguka nyumba ya Chris Brown wakisubiri kupata kibali cha kukagua ndani ya nyumba yake, vilevile polisi hao wamesema bado hawawezi elezea kama kweli hizo silaha ni za Brown au la japo zimekutwa ndani ya Mjengo wake.

TIMU KUBWA 6 ZA ULAYA ZENYE VIWANJA KAMA CHA AZAM

Picha
Na Athumani Adam Miongoni mwa habari kwenye soka hapa nchi ni suala la Azam kucheza mechi dhidi ya timu kongwe Simba na Yanga kwenyye uwanja wa Azam Complex kule Chamanzi. Wakati sakata la Azam likiendelea kupamba moto, kumbe hata Ulaya zipo timu ambazo zinacheza mechi zake kwenye viwanja ambavyo vinabeba mashabiki sawa na ule uwanja wa Chamanzi au kuzidi kidogo. Makala hii inakupa timu sita ambazo zinacheza mechi zake kwenye viwanja vidogo kutoka kwenye ligi nne kubwa duniani. EIBAR (Spanish La liga) Ipurua Municipal, watu 5250 Ni uwanja unaomilikwa na Mamlaka ya jiji la Eibar. Ulijengwa mwaka 1947 pia unatumiwa kwenye michezo mbali mbali hususani mpira wa miguu. LEGANES (Spanish La Liga), Municipal De Butarque, watu 8000 Uwanja huu unapatika katika jiji la Madrid eneo la Leganes, ulijengwa kati ya mwaka 1997-1998. Klabu ya  CD LEGANES inatumia uwanja huu kucheza mechi zake za nyumbani. CROTONE (Serie A), Ezio Scida, watu 9631 Kwenye mji mdogo wa Crotone kule Italy, ku...

Lowassa, Mbowe Watakiwa Kuripoti Polisi Keshoi Septemba 1

Picha
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho, Edward Lowassa na viongozi wengine waandamizi wameitwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwenda kuripoti keshoSeptemba Mosi. Hatua hiyo inatokana na viongozi hao kukamatwa juzi, baada ya kufanya mkutano maalumu wa ndani wa Kamati Kuu, na walipelekwa Kituo Kikuu cha Polisi cha Kanda hiyo na kuhojiwa kabla ya kuachiwa. Mbali na Mbowe na Lowassa, viongozi wengine wa Chadema waliokamatwa na kutakiwa kwenda Polisi kesho ni Katibu Mkuu, Vincent Mashinji, Naibu wake, John Mnyika na Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, Said Issa Mohammed. “Wameitwa Polisi waende Septemba mosi kuripoti baada ya jana kukamatwa na kuhojiwa wakituhumiwa kukiuka maagizo ya Polisi,”  alisema Msemaji wa Chadema, Tumaini Makene na kufafanua: “Lakini wanaweza kwenda au wakaanzia kwenye maandamano kisha wakaenda Polisi kuripoti.” Alisema maandamano hayo yatakuwapo kama yalivyopangwa kwani maanda...

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 33 & 34 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

Picha
Mtunzi:EDDAZARIA G.MSULWA ILIPOISHIA.... “Duu kweli malipo ni hapa hapa duniani?” “Kwa nini baba?” “MAMA YAKO NI KATILI SANA TENA ZAIDI YA SANA JAPO USONI MWEKE NI MWAMA KUPITILIZA” Maneno ya baba yakanicha mdomo wazi huku nikishangaa nisijue ni kwanini amesema mama yangu ni katili sana ENDELEA... Nikaendelea kumtazama baba kwa macho ya mshangao “Mama yako ni katili sana kiasi kwamba aliyaaribu maisha yangu kwa kiasi kikuwa....Kipindi ambacho wewe bado hujazaliwa tulikuwa tunapendana sana na kaka yangu na kwajinsi tulivyokuwa tunapenda tuliamini kwamba hakuna kitu amaco kitaweza kutuchonganisha...Ila ninanakumbuka kipindi baba yaka anaingia jeshini mimi nilifeli majaribio kutokana kipindi kile nilikuwa ninaumwa na ugonjwa wa miguu” “Basi baba yako akaja kukutana na mama yako na kutokana kipindi kile sisi tulikuwa ni fukara sana na wazazi wetu walisha fariki ikabidi kaka ambaye nilisha zoea kumuita kurwa aliniomba nihamie kw...

Waziri aliyesinzia mkutanoni auawa Korea Kaskazini

Picha
Image copyrightEPAImage captionRais Kim Jong-un na mkewe Ri Sol-ju Serikali ya Korea Kusini imesema waziri wa elimu nchini Korea Kaskazini ameuawa na maafisa wa serikali. Waziri huyo wa elimu Kim Yong-jin anadaiwa kusinzia katika mkutano wa kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un. Baadhi ya ripoti zinasema waziri huyo, ambaye amekuwa pia akihudumu kama mmoja wa manaibu wa waziri mkuu, alitekwa na usingizi wakati wa mkutano huo jambo ambalo lilichukuliwa kama kumkosea heshima kiongozi huyo. Maafisa wa Korea Kusini wamesema wanaamini waziri huyo aliuawa kwa kupigwa risasi mwezi Julai. Serikali hiyo inasema maafisa wengine wawili walilazimishwa kwenda kuishi maeneo ya mashambani, "kupewa upya mafunzo". Korea Kusini iliwahi kutoa taarifa kwamba kiongozi wa jeshi la Korea Kaskazini Ri Yong-gil alikuwa ameuawa mwezi Februari mwaka huu. Lakini mwezi Mei mwaka huu, ilibainika kwamba alikuwa bado hai na alikuwa akihudhuria mikutano na hafla rasmi za serikali. Mara ya mwisho Korea Ka...

SERIKALI Yapiga Marufuku Mashindano ya Wanawake Wenye Makalio Makubwa

Picha
Makalio MakubwaSerikali ya Burkina Faso imepiga marufu shindano ya kila mwaka kwa wanawake wene makalio makubwa kwa maelezo kuwa shindano hilo halina maadili na linaleta ubaguzi katika jamii. Tangazo la shindano hilo maarufu kama “Miss Bim-Bim” lililoonyesha wanawake wawili wenye makalio makubwa sana, lilizungua maswali mengi kwenye mitandao ya kijamii nchini humo. Baada ya watu kukosoa tamasha hilo, Waziri mwenye dhamana, Laure Zongo alisema kazi ya serikali ni kuhakikisha kuwa mwanamke hanyanyaswi na kuwa maoni ya watu kwenye mitandao ya kijamii imemsukuma kuzungumzia tukio hilo. Mtayarishaji wa mashindani hayo, Hamado Doambahe alisema kuwa walikuwa na lengo la kusifia umbo zuri la mwanamke wa ki-Afrika na wala sio kulenga kufanya jambo lolote baya. Mashindano ya namna hii yamekuwa yakifanyika katika nchi nyingine Magharibi mwa Afrika na kuwa wanawake wamekuwa na mitazamo tofauti juu ya mashindano haya.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano ya Agosti 31

Picha