SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 31 Agosti 2016

T media news

CHRIS BROWN AKAMATWA NA POLISI BAADA YA UCHUNGUZI KUMALIZIKA

Bad Newz kwa Chris Brown, kikosi cha polisi cha LAPD kimemkata Chris Brown baada ya kukutwa na silaha za mangamizi.

Chris Brown alikumbana na mkasa huo ni pale aliporipotiwa kumtishia mwanamke mmoja aliyefahamika kama Baylee Curran alipo mripoti Chris Brown baada ya Chris Brown na rafiki zake ambao walikuwepo ndani walimtishia silaha wakimtaka kusaini makubaliano ambayo hayakuwa mazuri kwake ndipo mwanadada huyo alipoamua kukimbia na kuwapigia simu polisi.

Kupitia taarifa iliyotolewa na ABC imesema kwamba Chris Brown amekamatwa na polisi hao ni pale aliporuhusu kuingia nao ndani kwa ajili ya kumkagua ndipo wakamkuta na Silaha hizo za maangamizi.

Tukio zima lilianza asubuhi ya jana Jumanne pale polisi walipovamia na kuzunguka nyumba ya Chris Brown wakisubiri kupata kibali cha kukagua ndani ya nyumba yake, vilevile polisi hao wamesema bado hawawezi elezea kama kweli hizo silaha ni za Brown au la japo zimekutwa ndani ya Mjengo wake.