SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 31 Agosti 2016

T media news

Ukuta: Upinzani waahirisha maandamano Tanzania

Image captionViongozi wa upinzani wakati wa kikao na wanahabari Dar es Salaam

Muungano wa vyama vya upinzani nchini Tanzania umeahirisha maandamano ya kitaifa ambayo yalikuwa yamepangiwa kufanyika kesho.

Viongozi wa upinzani, akiwemo Edward Lowassa wa Chadema, wametangaza hatua hiyo kwenye kikao na wanahabari Dar es Salaam.

Wamesema wameahirisha maandamano hayo kwa kipindi cha mwezi mmoja baada ya kusikia ombi la viongozi wa kidini na wadau wengine waliowaomba kukumbatia na kuyapa muda mazungumzo.

Viongozi wa chama hicho walikuwa wameitisha maandamano na mikutano ya kisiasa Septemba Mosi kupinga walichosema kuwa ni ukandamizaji unaoendelezwa na serikali.

Baada ya mkutano wa kikao cha Kamati Kuu ya chama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mwishoni mwa Julai, viongozi walisema: "Yapo Matukio ambayo yamekua yakifanywa na kukandamiza demokrasia na misingi ikipuuzwa na kudharauliwa."

Viongozi wa upinzani Tanzania kuhojiwa zaidiMaafisa wa Chadema wakamatwa Tanzania

"Si nia ya Chadema kugombana na Serikali bali ni kazi ya Chama Pinzani kuisaidia Serikali iongoze kwa kufuata misingi ya Katiba," chama hicho kilisema.

Maandamano hayo yalipwa jina Ukuta, ikisimamia Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania.

Image captionBw Lowassa, ambaye aliwania urais kupitia Chadema katika uchaguzi mkuu Oktoba mwaka 2015

Serikali ilipiga marufuku mikutano yote ya kisiasa, ya hadhara na ya ukumbini. Baadhi ya viongozi wa upinzani wamekamatwa na kuzuiliwa kwa muda.

BBC