Bunge la Afrika Mashariki limepitisha azimio la kuifanya lugha ya kiswahili kuwa lugha rasmi ya jamii ya Afrika Mashariki.
Wajumbe wa bunge hilo wamekubaliana kwamba mabadiliko hayo yalikuwa yakisubiriwa sana kwa kuwa lugha hiyo imechukua jukumu kubwa la kuwaunganisha wakaazi wa Afrika Mashariki.
Hatua inayofuata ni kwamba mkataba wa EAC utalazimika kufanyiwa marekebisho
Chanzo: BBC