Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili, 2017

Yanga wamevuliwa ubingwa wa FA Cup Mwanza

Picha
Kwa mara ya kwanza kwenye historia ya soka la Tanzania Mbao FC ya mkoani Mwanza imefuzu kucheza fainali ya FA Cup au maarufu kama Azam Sports Federation Cup kwa kuwatoa mabingwa watetezi wa kombe hilo Yanga SC. Wakiwa wamepanda daraja kutoka ligi kuu Tanzania bara kwa mara ya kwanza, wameweza kufuzu kucheza fainali ya kwanza katika historia yao kwa kuifunga Yanga kwa goli 1-0 katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Goli pekee lililoipa ushindi Mbao FC lilitokana na kujifunga kwa beki wa kati wa Yanga Vicent Andrew dakika ya 27 kipindi cha kwanza wakati akiwa katika harakati za kuokoa krosi iliyopigwa na Pius Buswita wa Mbao FC. Matokeo hayo yanaivua Yanga ubingwa wa FA Cup (Azam Sports Federation Cup) ubingwa ambao waliutwaa mwaka uliopita kwa kufunga Azam kwenye mchezo wa fainali. Mbao watakutana na Simba kwenye mchezo wa fainali mechi ambayo Simba ndio wanatarajiwa kuwa wenyeji kwa sababu ndio walikuwa wa kwanza kufuzu kucheza fainali baad...

Tetemeko la ardhi laukumba tena Mkoa wa Kagera usiku

Tetemeko la ardhi limeukumbuka kwa mara nyingine tena Mkoa wa Kagera ya kuzua hofu miongoni mwa wananchi kiasi cha wengine kuamua kulala nje ya nyumba zao wakihofia zinaweza kubomoka ka kuwajeruhi au wakafariki dunia. Kwa mujibu wa wakazi wa mkoa huo wamesema kuwa tukio lilitokea saa saba za usiku wa kumakia leo. Hofu kubwa iliyowaingia wakazi wa eneo hilo imetokana na tetemeko la awali lililoukumba mkoa huo Septembe mwaka jana lenye ukubwa wa 5.7 katika  vipimo vya Ritcher na  kusababisha vifo vya zaidi ya watu 15 na majeruhi zaidi ya 230, huku nyumba na mioundombinu mbalimbali ikiharibiwa vibaya.aHadi sasa hakuna taarifa za maafa yoyote yaliyosababishwa na tetemeko hilo. Tutaendelea kukujuza zaidi.      

Maneno ya Mo baada ya Simba kufuzu fainali ya FA Cup

Picha
Na Zainabu Rajabu KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Mohamed Ibrahim ‘Mo’ amesema kuwa, wamepata ushindi dhidi ya Azam kutokana na jinsi walivyojituma na kusikiliza maelekezo ya kocha wao walipokuwa mapumziko. Mo licha ya kufunga bao pekee na la ushindi kwa upande wa Simba alipewa kadi nyekundu na Mwamuzi Mathew Akrama kutoka Mwanza baada ya kuoneshwa kadi ya njano ya pili kwa kumchezea vibaya Shomari Kapombe. Shaffihdauda.co.tz ilizungumza na Mohamed Ibrahim ambaye amesema kujituma na umoja katika timu ndiyo silaha ya ushindi wao licha ya hali ya hewa kuwazuia kucheza kabumbu zuri. “Tumefurahi kuingia fainali si unajua kila mtu anataka matokeo mazuri kwenye michuano hii ili kuwaikilisha timu katika mashindano ya kimataifa, kama wataingia Yanga au Mbao kwenye hatua ya fainali basi wajipange sana,” amesema Mo. Aidha, Mo amesema kuwa kukosekana kwake kwenye mechi ya fainali hakuto athiri kitu kutokana na mwalimu kuwa na wachezaji wengine ambao atawapa nafasi. ...

ZITTO Kabwe Atumbua Jipya la Ndege Mpya Boeing Iliyonunuliwa na Serikali..Afunguka Makubwa

Picha
Sakala la Serikali kusemekana imenunua ndege ya Boeing ambayo ina walakini imechukua sura mpya baada ya Mbunge Zitto Kufunguka Haya Hapa chini kupitia page yake ya Facebook: "Hizi Ndio Habari za kina kuhusu ndege ya Boeing 787 Dreamliner tuliyokwishalipia. Ni sehemu ya ndege zilizokuwa chini ya kiwango zikiitwa Terrible Teens. Iliundwa mwaka 2009 na kununuliwa na ReandAir Tarehe 21/11/2013. Baada ya Mwaka, tarehe 3/12/2014, Rwanda wakaikataa na kuirudisha. Tanzania imeinunua tarehe 14/12/2016 Kwa dola za kimarekani 224 milioni.  Sasa, mwanzo nilitaka maelezo ya Serikali, wasemaji wa Serikali wakawa wengi Sana kuwa tuliyonunua sisi sio terrible tween. Nimefanya utafiti kidogo na NIMETHIBITISHA kuwa tumenunua ndege zilizokatawaliwa hata na Rwanda rafiki zetu. Kinachofuata ni kikubwa zaidi. Watetezi wa Serikali muwe tayari kuja kutetea pia maana labda mna mgawo. Kifuatacho NCHI ITATIKISIKA" Zitto Kabwe

RAY C -Hapa Kazi Tu, Mapenzi Baadaye..!!!

Picha
Msanii mkongwe wa muziki, Ray C, amedai kwa sasa anapambana kuhakikisha anafanya vizuri katika muziki wake. Muimbaji huyo ambaye aliwahi kufanya vizuri kipindi cha nyuma na wimbo ‘Mapenzi Matamu’, alikuwa kimya kwenye muziki kwa muda mrefu akijaribu kuachana na matumizi ya dawa za kulevya ambazo zlimuathiri kwa kiasi kikubwa. Akiongea  wiki hii akiwa mwenye siha njema, Ray C amedai anachokifikiria kwa sasa katika maisha yake ni muziki na siyo mapenzi. “Mimi sina mpenzi,” alisema Ray C “Kwa sasa nafikiria kuhusu muziki wangu sitaki kujichanganya na mambo mengine. Mashabiki wangu wamenipambania kwa muda mrefu siyo kwaajili ya mpenzi wangu, wao wanataka kazi, muziki mzuri,” Muimbaji huyo ambaye anafanya kazi chini ya Wasafi.Com ya Diamond Platnumz anafanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Unanimaliza’. Katika hatua nyingine muimbaji huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwaajili ya albamu yake mpya.

JPM Awapa za Uso Wananchi wa Jimbo la Hai kwa Kutomchagua Mwaka 2015..Awasamehe..!!!

Picha
Rais John Magufuli  amewaambia wakazi wa mji wa Bomang’ombe katika Jimbo la Hai kuwa amewasamehe. Alitoa kauli hiyo akiwa katika jimbo hilo la Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe baada ya kuwaona baadhi ya wananchi wakiwa wameshika jani la “Sale” ambalo hutumiwa na wenyeji kuomba msamaha. Jani hilo linaloheshimiwa sana na wachaga wa mkoa huo, ndilo ambalo mtu akimpelekea mtu aliyemkosea na kumuomba yaishe, anayeombwa kupitia jani hilo hana jinsi lazima akubali. “Nawashukuru sana wote mliokuja na haya majani ya mti. Nafahamu maana yake na mimi nimewasamehe wote. Najua na ninyi mmenisamehe wote,”amesema Rais Magufuli huku akishangiliwa. Ingawa Rais Magufuli hakuweka bayana walichomkosea, lakini katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015, Rais Magufuli alipata kura 29,341 wakati mpinzani wake wa karibu, Edward Lowassa akipata kura 49,125. “Tushikamane kwa pamoja tujenge nchi yetu. Hakuna Mtanzania anayekula vyama, Mtanzania anataka maendeleo, anatak...

HIVI Ndivyo Maalim Seif Alivyoruka Viunzi na Vigingi vya Kila Aina Katika Siasa za Tanzania..!!!

Picha
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Seif Sharif amekuwa hatoi kauli kali zinazoonyesha uwezo wake wa kukabiliana na misukosuko, lakini hivi karibuni alitoa cheche zake kuonyesha atavuka katika msukosuko unaokikabili chama hicho kwa sasa. Maalim Seif alishafikia kiwango cha kuwa Waziri Kiongozi, nafasi ambayo ilikuwa ya mtendaji mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), lakini akavuliwa uanachama na kupoteza madaraka yake yote, akafunguliwa kesi, akawekwa ndani kwa zaidi ya mwaka mmoja, na baadaye kupambana na migogoro ndani ya chama hicho cha upinzani. Aprili 9 katika mkutano wake na waandishi wa habari, Maalim Seif alionyesha kuwa hata mgogoro uliopo sasa dhidi ya kundi linaloongozwa na Profesa Ibrahim Lipumba utaisha kwa ushindi. “Binafsi nimetumia uwezo wangu wote kupigania haki na demokrasia Zanzibar na Tanzania nzima na wananchi ni mashahidi wangu,” alisema katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Dar es Salaam. “Nimepatishwa taabu na kufanyiwa uovu mwingi, huku wal...

MADAM Flora - Sipendi Maisha ya Ustaa..!!!

Picha
Madam Flora (zamani Flora Mbasha) amesema hayo hivi karibuni ikiwa ni siku chache kuelekea ndoa yake ambapo amefunguka na kudai kuwa baada ya kumpata mwanaume ambaye siyo maarufu anafurahi kwani hata mfumo wa maisha yake utaenda kubadilika na kuishi kama watu wengine ambao siyo maarufu. "Mume wangu mtarajiwa siyo mtu anayejulikana  bali naamini kwenye ulimwengu wa kiroho anajulikana. Namshukuru Mungu maisha mapya ambayo naenda kuyaishi siyo ya umaarufu. Mimi nimemwambia pamoja na ustaa nilionao napenda tuishi maisha ya kawaida ambayo hayahusiani na umaarufu wangu. Unajua kuna wakati natamani kushuka kwenda kula chakula kwa mama n'tilie lakini watu watashangaa hata wewe? sasa najiuliza who is Flora?  kumbe mimi pia ni mtu wa kawaida kabisa. Sitamani maisha ya Ustaa yananinyima uhuru"- Madam Flora. Aidha Flora amefunguka kuhusu mahusiano yake na kwamba kabla ya kukubali kuolewa kwa mara ya pili ilimchukua zaidi ya mwaka mmoja kutafakari ikiwa ni pamoja na kushirikisha fa...

Taarifa Potofu Zinazomuhusisha Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza Dr Asha Rose Migiro

Picha
Ubalozi wa Tanzania London umepokea Habari inayozagaa kwenye ukurasa wa mtandao wa kijamii wa instagram ikiwa na nukuu ifuatayo: ''Binafsi bado sijaona umuhimu na mafanikio ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zaidi ya vingozi kujikusanyia mali na utajiri mkubwa sambamba na kung'an'gania madaraka kwa nguvu. Mfano uchaguzi uliofanyika mwaka 2015 kwa yaliyotokea Zanzibar ni miongoni mwa Athari mbaya kabisa zinazotokona na Muungano,nadhani kila Mtanzania aliyaona" Ukurasa huo wenyewe jina la UKUTA inaihusisha nukuu hiyo na jina la Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dkt Asha Rose Migiro.  Ubalozi wa Tanzania London unapenda kutumia fursa hii, kuwajulisha Watanzania Waishio Uingereza na Watanzania kwa ujumla kuwa Balozi Migiro ahusiki na nukuu hiyo kama inavyosambazwa.Hivyo ni wazi kuwa wanayoisambaza wana malengo ya kulichafua jina la Balozi Migiro kwa sababu wanazozijua wao.  Ubalozi wa Tanzania London unaendelea kutoa wito kwa Watanzania Waishio Uingereza kutu...

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili ya April 30

Picha

‘Tulijua matokeo kabla hata mechi haijaanza’ – Kocha Azam FC

Picha
Kocha msaidizi wa Azam FC, Idd Cheche amesema, walikua wanajua kila kitu kuhusu mechi yao ya nusu fainali ya kombe la FA au Azam Sports Federation Cup dhidi ya Simba kabla hata ya mchezo kuanza. Cheche amesema walishaanza kuona dalili mbaya kwao kuanzia kwenye mkutano kabla ya mechi (Pre-match meeting) na kilichokuja kutokea badae uwanjani hakikuwashangaza sana. Azam wanambebesha mzigo wa lawama mwamuzi Mathew Akrama kwa kushindwa kuumudu mchezo huku kitendo cha mwamuzi huyo kumwonesha kadi nyekundu Salum Abubakar ‘Sure Boy’ dakika ya 16 tangu kuanza kwa mchezo kikipingwa vikali. “Mchezo haukua mzuri kwa sababu ya mvua na maamuzi hayakua ya fair. Tangu tunatoka kambini kwetu tuliwaambia wachezaji wetu kuhusu haya yaliyotokea kwa sababu tulikua tunajua kilakitu kabla hata ya mchezo wenyewe.” “Tangu tukiwa kwenye Pre-match meeting tulijua mchezo utakuaje. Wenyeji wa mpira wa Tanzania wanajua, wale waliokuja kwenye mpira wetu tangu miaka ya 1970 kuja ha...

HAYA Sasa..Upimaji wa Ukimwi wa Nyumba Hadi Nyumba Unaanza Rasmi Kesho..Jiandae Kikamilifu!!

Picha
UTAFITI wa viashiria na matokeo ya Ukimwi wa mwaka 2016 ambao unahusisha upimaji wa ugonjwa huo kaya kwa kaya kwa Mkoa wa Dar es Salaam, utaanza kufanyika Mei mwaka huu, ambapo jumla ya kata 31 kutoka wilaya tatu za mkoa huo ndizo zitakazoshiriki. Utafiti huo pia utahusisha ukusanyaji wa taarifa zisizohusu maambukizi mapya ya Virusi Vya Ukimwi (VVU), kiwango cha VVU mwilini na kwa watu wanaoishi na ugonjwa huo, wastani wa maambukizi kwa watu wa rika zote na wingi wa chembechembe za kinga mwilini (CD4). Hayo yalisemwa jana Dar es Salaam na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema kwa niaba ya Mkuu wa mkoa huo, Paul Makonda wakati wa uzinduzi wa utafiti huo wa mwaka 2016/17 na kusema kuwa wakati wa utafiti huo, baadhi ya vipimo ambavyo wanakaya watapimwa, vitatolewa majibu papo hapo. Utafiti huo umeanza kufanyika Oktoba mwaka jana na unatarajia kukamilika Julai mwaka huu ambao unashirikisha Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar, Shirika la ICAP l...

RASMI..Marekani Watoa Msimamo Wao Kuhusu Zanzibar Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka Juzi..!!!

Picha
SERIKALI ya Marekani imesema itaendelea kutoa misaada ya kiuchumi, ustawi wa jamii na kisiasa kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ili kuimarisha uhusiano wa nchi hizo mbili. Msimamo huo umeelezwa katika ziara ya ujumbe wa Serikali ya Marekani uliotembelea Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kwa ajili ya kuzungumzia masuala ya sera za kiuchumi, kisiasa na kijamii huko Ofisi Kuu Kisiwandui Unguja. Marekani ambayo ni Taifa kubwa lililoendelea kiuchumi, kijamii na kiulinzi, imesema kasi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Saba Zanzibar, linaishawishi taifa hilo kutoa misaada binafsi na inayopitia katika ngazi za kimataifa, ili kuenzi kwa vitendo juhudi hizo. Kiongozi wa msafara huo ambaye ni Ofisa wa kusimamia Masuala ya Sera za Kijamii na Kisiasa katika Ukanda wa Nchi za Afrika zilizomo katika Jangwa la Sahara, Gregory Simpkims alieleza kwamba CCM iimekomaa kisiasa na inaendelea kuimarika, tofauti na vyama vya kisiasa vya nchi nyingine barani Afrika, ambavyo baa...

TRUMP Akejeli Jaribio La Kombora La Korea Kaskazini Jana, ‘Ni Dharau’..!!!

Picha
Rais wa Marekani, Donald Trump amekejeli jaribio la kombora la kinyuklia la Korea Kaskazini lililofanyika jana, akidai kuwa ingawa limeshindwa ni dharau kwa China. Jana, Korea Kaskazini ilidai kufanya jaribio lake la kombora la Nyuklia ambalo Marekani ilidai kuwa lilishindwa hata kuvuka mipaka ya nchi hiyo ndani ya dakika chache tangu lilipofyatuliwa. “Korea Kaskazini imedharau matarajio ya China na ni dharau ya hali ya juu kwa Rais [wa China], ingawa limeshindwa, jaribio la makombora la leo. Mbaya!,” Tafsiri isiyo rasmi ya Tweet ya Rais Trump. Trump alisema kuwa angependa sana kuumaliza mgogoro wa makombora ya kinyuklia wa Korea Kaskazini kwa njia ya kidiplomasia, lakini ni vigumu sana kutumia njia hiyo. Katika mkutano wa Umoja wa Mataifa (UN) uliofanyika jana jijini New York, wajumbe walilitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuiwekea Korea Kaskazini vikwazo zaidi vya kiuchumi na kidiplomasia.

MBUNGE CCM Atuhumiwa Kuhujumu Uchumi..Akwepa Kulipa Kodi ya Milioni 500..!!!

Picha
MBUNGE wa Kwimba, Mwanza, Shannif Mansour (CCM), anatuhumiwa kugoma kulipa kodi ya eneo lake la ardhi lenye ukubwa wa hekta 39,000, kiasi cha zaidi ya Sh. 500 milioni tangu mwaka 2010. Mansour kupitia kampuni yake ya Sineji Tanzania Limited, anatuhumiwa kuigomea serikali kulipa kiasi hicho cha fedha kwa madai yeye hawezi kulipa fedha hizo kwa kuwa anafahamiana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, William Lukuvi. Eneo hilo la Mansour na kampuni yake inayojihusisha na utengenezaji wa malighafi za ujenzi ikiwemo kusaga kokoto, lililopo kata ya Buhongwa, Nyamagana pia baadhi ya wananchi wanalalamika kulaghaiwa fedha za fidia za maeneo yao. Tangu kipindi hicho, mbunge huyo alikuwa anadaiwa kiasi cha Sh. 529 milioni na Halmashauri ya jiji la Mwanza na kwamba wakati alipotakiwa kulipa fedha hizo tangu mwaka 2010 alikuwa akigoma kulipa fedha hizo kwa kutumia mwamvuli wa nafasi yake ya ubunge. Madai ya mbunge huo kuigomea serikali kulipa kodi hiyo, yaliibuliwa jana na Waziri Lukuvi, wakat...

Anthony Joshua Amtwanga Wladimir Klitschko kwa TKO

Picha
Anthony Joshua ameonyesha kuwa yeye ndiye mfalme mpya wa ngumi za kulipwa kwa uzito wa juu baada ya kumshinda mkongwe Wladimir Klitschko kwa TKO katika raundi ya 11. Pambano hilo la raundi 12 kwenye Uwanja wa Wembley jijini London, England lilikuwa kali na la kuvutia.