HISTORIA YA UWANJA WA NYAGANA AU UKOMBOZI STADIUM

*
  Ilikuwa mwaka 1945 mwezi mei (5)uwanja wa nyamagana ulijengwa kwa Mara ya kwanza.ikiwa ni kumbukumbu ya kumalizika kwa ""*vita kuu ya pili ya dunia*.
Uwanja huu ulijengwa na na wakoloni ambao walikabidhi madaraka ya uongozi wa uwanja huo kwenye halmashauri ya mji wa kwa wakati huo.

Mwaka 1950 halmashauri ya  mji iliamua kuzungushia seng'enge na serikali ya wakoloni kufuatia kupokelewa kwa maandamano ya machifu waliokuwa wakipinga serikali ya mseto.

Kwa muda wote huo uwanja wa nyamagana haukuwa na viti kwa ajili ya kukaa,

Mwaka 1960 ground stand ilijengwa kwa msaada wa fedha zilizotolewa na Dr Williamson wa mmiliki kuwa serikali ya mkoa wa Mwanza.

Uwanja wa nyamagana ulijengwa upya mwaka 1972 kwa mchango wa Williamson company michango ya wananchi na serikali chini ya uongozi wa ndugu Omari muhaji aliyekuwa mkuu wa mkoa wa wakati huo.

Matengenezo hayo yalikuwa ni pamoja na.
-ukuta mzuri wa tofali
-viti sehem ya mashariki na magharibi
-Broadcasting studio
-vyoo
Yote hiyo ilikuwa ni maadalizi ya kwa ajili ya TAIFA CUP TOURNAMENT ya mwaka 1972.

Taarifa za kuja Mwanamuziki wa Zaire wakati huo kwa sasa DRC hayati LUAMBO LWANZO MAKIADI.
Nguzo za taa za umeme (mercury vapour lamps)ziliwekwa kwa ajili ya onyesho hilo.

Uwanja wa nyamagana uliendelea kuwa chini ya mkurugenzi wa utamaduni wa taifa.

Tar 14-7-1979 uwanja ulichukuliwa na halmashauri ya mji wa Mwanza na kuwa chini ya Mkurugenzi mji wa Mwanza bila kufuata utaratibu wa kisheria kulingana na sheria na kanuni za BMTza mwaka 1967.

Uwanja wa nyamagana umewahi kuchezwa mechi nyingi zenye kumbukumbu ya kusikitisha na kufurahisha pia.

Timu kutoka Brazil zilifika Mwanza na kucheza kwenye uwanja wa nyamagana.

Wakati huo mkoa wa Mwanza unatimu ambazo zilikuwa zikiujuwa Mpira kweli kweli.

Timu kama pamba ya Mwanza coop united biashara(RTC) zilitamba sana miaka hiyo,

Timu ya Garcia toka Brazil na Colorado pia ya Brazil zilifika nyamagana na kucheza na timu za hapa Mwanza.

Mwaka 1974 nyamagana ilichezwa mechi Kubwa ya Mpira wa miguu kati ya Simba na yanga ambapo mchezo huo uliacha gumzo Kubwa kwa mchezaji wa Simba Sadi Ally kugongana na mchezaji wa Yanga Gibson sembuli na kupelekea sadi kuzimia na kukimbizwa hospitali.hadi dakika ya 87 Simba walikuwa wanaongoza kwa goli moja cha ajabu sasa hadi Mpira unaisha yanga walitoka kufua mbele kwa goli 2 kwa moja la Simba.

Uwanja wa nyamagana umekuwa ukitumika pia kwa kazi za kijamii na kisiasa.

Miongoni mwa mambo ya kijamii ni pale mwaka 1979-80 wakati wanajeshi wetu wakirudi kutoka vitani hiyo ni baada ya kumpiga dikteta Iddi Amin dadaaa wa Uganda.
Wanajeshi walikuwa wanafikia hapo uwanja wa nyamagana na kisha Magari kuwachukuwa na kuwapeleka kwenye vikosi vyao vya kazi.

Ndani ya uwanja wa nyamagana kuna watu walianguka na kuvunjika miguu na mikono na wengine kuanguka na mabati nyumba za jirani na kupelekea vifo

Mmoja wa watu waliovunjika mguu ni Adamu kazembe aliyekuwa mchezaji wa coop united na kuhamia RTC mechi ya kwanza kati ya RTC na Coop united walikutana Adam kazembe na swahiba wake Burhan Hemed na hapo hapo Adam akavunjika mguu.
Tukio Kubwa lingine kufanyika hapo nyamagana ni kuzama kwa MV bukoba.

Baada ya kuzama kwa meli serikali ikasema miili yote ipelekwe nyamagana kwa ajili ya kutambuliwa na ndugu zao.

Aliyekuwa mbunge wa Mwanza na mwanasiasa mkongwe nchini hayati Paul bomani alipo fariki mwili wake uliagwa hapo nyamagana.

Kiongozi mwingine aliyeagwa hapo nyamagana baada ya kufariki ni aliyekuwa RPC wa Mwanza kamanda Liberatus Bhalo .

Halmashauri ya manispaa ya Mwanza ilianza mchakato wa uendelezaji wa uwanja September 1998.
Kupitia kamati ya tenda ya Halmashauri ya manispaa ilitangaza Ya vioksi vya maduka maghala na ofisi katika uwanja huo.tenda hiyo iliwataka waombaji kujenga ndani ya miezi sita.

Nimekukumbusha kidogo kazi za uwanja mkongwe wa nyamagana uliopo katikati ya mji wa Mwanza wilaya ya nyamagana.  


Makala hii ya uwanja wa nyamagana imeandaliwa na:

Katumba Madua
Kutoka redi metro FM 99.3
Mwanza
Email.maduwakatumba@gmail.com

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: UTAMU WA MADAM JESCA

Simulizi; MTOTO WA BOSS WANGU

SIMULIZI FUPI: UCHI WANGU UMENIPONZA