Anthony Joshua ameonyesha kuwa yeye ndiye mfalme mpya wa ngumi za kulipwa kwa uzito wa juu baada ya kumshinda mkongwe Wladimir Klitschko kwa TKO katika raundi ya 11.
Pambano hilo la raundi 12 kwenye Uwanja wa Wembley jijini London, England lilikuwa kali na la kuvutia.