Tetemeko la ardhi limeukumbuka kwa mara nyingine tena Mkoa wa Kagera ya kuzua hofu miongoni mwa wananchi kiasi cha wengine kuamua kulala nje ya nyumba zao wakihofia zinaweza kubomoka ka kuwajeruhi au wakafariki dunia.
Kwa mujibu wa wakazi wa mkoa huo wamesema kuwa tukio lilitokea saa saba za usiku wa kumakia leo.
Hofu kubwa iliyowaingia wakazi wa eneo hilo imetokana na tetemeko la awali lililoukumba mkoa huo Septembe mwaka jana lenye ukubwa wa 5.7 katika vipimo vya Ritcher na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 15 na majeruhi zaidi ya 230, huku nyumba na mioundombinu mbalimbali ikiharibiwa vibaya.aHadi sasa hakuna taarifa za maafa yoyote yaliyosababishwa na tetemeko hilo.
Tutaendelea kukujuza zaidi.