Na Zainabu Rajabu
KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Mohamed Ibrahim ‘Mo’ amesema kuwa, wamepata ushindi dhidi ya Azam kutokana na jinsi walivyojituma na kusikiliza maelekezo ya kocha wao walipokuwa mapumziko.
Mo licha ya kufunga bao pekee na la ushindi kwa upande wa Simba alipewa kadi nyekundu na Mwamuzi Mathew Akrama kutoka Mwanza baada ya kuoneshwa kadi ya njano ya pili kwa kumchezea vibaya Shomari Kapombe.
Shaffihdauda.co.tz ilizungumza na Mohamed Ibrahim ambaye amesema kujituma na umoja katika timu ndiyo silaha ya ushindi wao licha ya hali ya hewa kuwazuia kucheza kabumbu zuri.
“Tumefurahi kuingia fainali si unajua kila mtu anataka matokeo mazuri kwenye michuano hii ili kuwaikilisha timu katika mashindano ya kimataifa, kama wataingia Yanga au Mbao kwenye hatua ya fainali basi wajipange sana,” amesema Mo.
Aidha, Mo amesema kuwa kukosekana kwake kwenye mechi ya fainali hakuto athiri kitu kutokana na mwalimu kuwa na wachezaji wengine ambao atawapa nafasi.
“Siwezi kuzungumzia sana swala ya kadi nyekundu niliyopewa na mwamuzi nawaachia viongozi wangu wa Simba watalishughulikia.”
Mo ambae mchezo wa jana alionekana kubadilisha mtindo wa nywele kwa kunyoa staili ya Kijogoo ambayo anasema ni yeye mwenye kaibuni kimtaani mtaani lakini hajaona mtu akiwa na staili hii.