Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba, 2016

TANGAZO:TAWFIQ MONEY SERVICE WAKALA WA KIBANK BUNDA

Picha
ANAPATIKANA BARABARA YA BOMANI MKABALA NA STENDI YA ZAMANI TUNATOA HUDUMA ZIFATAZO KWAJIA YA BANK: -KUFUNGUA AKAUNTI ZA CRDB,EQUITY ,POST  BANK. -KUWEKA PESA -KUTOA     PESA -KUTUMA  PESA -KULIPIA ADA ZA SHULE -KULIPIA MALIPO MBALIBALI YA SEREKALI. KUWEKA PESA NA KUTUMA NI BURE KABISA.  PIA TUNATOA HUDUMA ZA :- - BIMA ZA MAGARI - MOTOR VAHICLE PIA TUMEFUNGUA OFISI  NYINGINE NYASURA STENDI UPANDE WA GARI ZINAZO KWENDA MWANZA KARIBUNI KUPATA HUDUMA LUKU VING'AMUZI VYA TV SIMU NAMBA 0784699901,0756141420

ZIJUE SABABU ZA MAHAKAMA KUFUTA OMBI LA DAVID KAFULILA LA KUTAKA KUKATA RUFAA UPYA

Picha
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Tabora leo, imefuta ombi la David Kafulila la kuingiza rufaa yake upya,  Kafulila alitaka kuingiza rufaa yake upya ili apate fursa ya kuiingiza katika Mahakama ya Rufaa fomu za tume No 21B za kila kituo kwenye vituo vyote 382 kusomwa matokeo yake kubaini mshindi tofauti na ilivyokuwa katika ngazi ya Mahakama Kuu. Hatua ya kufutwa rufaa hiyo inakuja baada ya Mahakama ya Rufaa tarehe 13 Oktoba mwaka huu mbele ya majaji Luanda Bernad, Mbarouk Salim na Mziray Richard kushindwa kuondoa rufaa hiyo na kuelekeza kuwa, rufaa hiyo inaweza kurejeshwa baada ya marekebisho. Katika ombi hilo, Kafulila alitaka mahakama kuu kwa mujibu wa sheria imruhusu aingize rufaa hiyo upya kwa kuwa ni haki ya kisheria. Hata hivyo Jaji Mrango katika uamuzi wake amesema kwamba, maombi ya Kafulila yamekosa hoja za msingi kuishawishi mahakama kuu kuruhusu rufaa hiyo kuingizaa upya kama alivyoomba. Kwa upande wake Kafulila ameeleza kutoridhika na uamuzi huo kwa hoja kwamba, sababu za kui...

KAULI ya Ruge ni Sahihi na ya Kikubwa, Uongozi Utaifanyia Maamuzi – Lady Jaydee (Audio)

Picha
Laydee amesema kauli aliyoitoa Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba kuhusu kuwa tayari kucheza nyimbo zake akiwaruhusu, ni sahihi na ya kiutuzima. Muimbaji huyo mkongwe ametoa kauli hiyo kwenye mahojiano na mtangazaji wa Nyemo FM, ya Dodoma, Winston Makangale. “Nimeisikia kauli ya Ruge, kwa namna aliyoiongea na nafasi aliyokuwa nayo, sioni kama kuna kitu kibaya chochote alichokifanya kwa jinsi ambavyo amezungumza, naona amezungumza sahihi tu,” alisema. Amesema yeye na Ruge hawajahi kuzungumza kwa miaka minne sasa. “Hajanipigia simu na wala sijampigia simu, kwahiyo sio kwamba tumeongea kitu chochote lakini nayaona tu ni maamuzi ya kikubwa ambayo yamefanyika hapo. Hatujaongea kwasababu tulikuwa na mgogoro,” ameongeza 

BENKI ya CRDB Yafunguka Kuhusu Tetesi ya Kuwa Imepata Hasara Kubwa Mwaka Huu

Picha
Benki ya CRDB imesema haijapata hasara kama tetesi zinavyoenezwa. Imesema kuwa imepata faida ya Bilioni 63 kwa kipindi cha Januari hadi Septemba, 2016.  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Charles Kimei amesema mwaka huu wamepanga kufungua matawi 75 na kuajiri wafanyakazi 460. Dkt. Kimei amesema mwaka jana pekee wamefungua matawi 70 na kuajiri watu 450 jambo ambalo benki nyingi nchini haziwezi kufikia.

WAFUASI wa CUF Wavamia Makao Makuu ya Chama Zanzibar

Picha
MTENDENI, ZANZIBAR: Wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF), Zanzibar leo wamevamia Ofisi za Makao Makuu ya Chama hicho yaliyopo eneo la Mtendeni visiwani humo wakitaka kufahamu hatma ya maamuzi yao ya Okt 25, 2015, ambapo chama hicho kinadai kilishinda uchaguzi kabla ya kufutwa.

NIMEFANYA Video Karibia 10 Lakini ya Diamond Mnaniuliza Kila Saa, Who is Diamond Motherf**** – Tunda

Picha
Tunda amechoka kuulizwa maswali kuhusiana na kuonekana kwenye video ya Diamond ya wimbo Salome aliomshirikisha Ray Vanny. Ni kwasababu anajiuliza, iweje ameshaonekana kwenye video takriban 10, lakini tangu aonekane kwenye video ya Diamond, swali limekuwa lile lile na ni kama vile watu ndio wameanza kumuonea kupitia video hiyo. Kutokana na kuchoshwa na swali hilo, Tunda anayedaiwa kurudiana na mpenzi wake Young Dee, amempa jibu kavu mtangazaji wa Jembe FM, Natty E aliyemrushia swali lile lile limkeralo. “Nimefanya video ngapi? Nimefanya video karibia 10 lakini hii ya Diamond mnanifanyia interview kila saa,” Tunda alimjibu Natty. “Diamond, Diamond, who is Diamond motherf*cker. Weka hiyo kwenye gazeti lako,” aliongeza. Natty alijikaza na kumjibu ‘Anyway, Unaweza acha hilo swali la kuhusu Diamond, it’s not a big deal.’ Tunda alijibu kikauzu zaidi, “Maswali yote jibu lake ndio hilo.” Anachoshindwa kukielewa Tunda ni kuwa kus...

NAFASI za TTCL na Nyingine Nyingi Zilizotangwa Katika Magazeti Leo

Picha
Bonyeza Links Hizi Hapa Chini Kusoma zaidi na Kuapply: Job Opportunity at Tanzania Telecommunication Company Limited, Commercial Executive Job Opportunity at Good Neighbors Tanzania, Programme Assistant Officer Job Opportunity at BRAC International, Program Manager Job Opportunity at Strategis Insurance (Tanzania), Actuarial Executive Job Opportunity at Medecins Sans Frontieres, Supply Supervisor Job Opportunity at The University of Dar es Salaam Computing Centre (UCC) Zaidi Ingia Hapa  www.ajirayako.com

RAPA ROMA AVURUGWA NA MASHABIKI WAKE

Picha
Msanii wa Hip Hop kutoka Bongo, Roma Mkatoliki, amesema anashangazwa na kitendo cha mashabiki kupenda zaidi muziki wa nje kuliko ule wa wasanii wa hapa nyumbani. Roma amesema yeye kama msanii kitu kama hicho kinamuumiza na hajui iwapo ni thamani ya msanii imeshuka hapa nyumbani, au ni kweli muziki wa nje ni mzuri kuliko hapa nyumbani. Kitendo hicho cha Roma kimeungwa mkono kauli ya MC Koba ambaye naye alishawahi kulalamika kitu kama hicho, na kusema kuwa kinaua muziki wa ndani na kupoteza matumaini ya wasnaii wa hapa nyumbani.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Kufanya Ziara Ya Kikazi Mkoani Arusha

Picha
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania MHE. Kassim Majaliwa  anatarajiwa kutembelea Jiji la Arusha kuanzia kesho tarehe 01 hadi 03/12/2016 na kukagua miradi ya maendeleo, kuongea na watumishi wa Jiji, kukutana na wafanyabiashara pamoja na kuzungumza na wananchi. Kwa mujibu wa Afisa habari wa Jiji la Arusha Nteghenjwa Hosseah, kesho tarehe 01/12/2016 Waziri mkuu MHE. KASSIMU MAJALIWA atatembelea National Milling Company (NMC) na pia atakagua ujenzi wa barabara ya Friends Corner - Muriet yenye urefu wa Km 7 inayojengwa kwa kiwango cha Lami kupitia mradi wa Mpango Mji Mkakati (TSCP) na kusimamiwa na Ofisi ya Rais Tamisemi. Hosseah amesema siku ya tarehe 02/12/2016 Waziri Mkuu atakutana na kuzungumza na watumishi pamoja walimu katika Ukumbi wa AICC Arusha na baadae atakutana na wafanyabiashara katika Ukumbi huo. "Katika nsiku ya tatu ya ziara yake Mhe Majaliwa  atatembelea na kukagua viwanda vya Lodhia pamoja na Hans Paul vilivyoko mtaa wa Viwanda – Njiro na baad...

Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Singida Afariki Dunia, Mwili Kuagwa Leo Saa 11 Jioni Muhimbili

Picha
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) EX Peter Kakamba amefariki dunia alfajiri ya tarehe 30/11/2016 katika hospital ya taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu. Kakamba alizaliwa mwaka 1963 katika kijiji cha Kawajense Wilayani Mpanda, mkoa wa Katavi. Alisoma shule ya msingi Shanwe Kawajense  mwaka 1973 hadi 1980, Kidato cha kwanza hadi cha nne katika shule ya Sekondari Kantalamba mwaka 1981 hadi 1984 ambapo kidato cha tano na sita alisoma katika shule ya Sekondari Umbwe mkoani Kilimanjaro mwaka 1985 hadi 1987. Mwaka 1992 hadi 1994 alisoma Astashahada ya Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Marehemu alijiunga na Jeshi la Polisi mwaka 1988 ambapo katika utumishi wake alipandishwa vyeo mbalimbali ikiwemo Konstable wa Polisi (1989), Sagenti wa Polisi (1991), Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (1997), Mkaguzi wa Polisi (2003), Mrakibu Msaidizi wa Polisi (2006), Mrakibu wa Polisi (2008), Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (2011), Kami...

HUYU NDIYO MPENZI WA MSANII RAYVANNY WA WCB

Picha
Ule usemi wa Kiswahili unaosema ‘penzi ni kikohozi kulificha hauwezi’ unazidi kujidhihirisha kwa muimbaji wa WCB, Rayvanny baada ya anayedaiwa kuwa mpenzi wake kuonyesha ni jinsi gani anavyomzimia mkali huyo wa wimbo, Sugu. Mwaka huu mwanzoni Rayvanny alipost picha mtandaoni akiongelea na mrembo huyo hali ambayo iliibua maswali mengi kutokana na picha hiyo kutoonyesha sura ya mrembo huyo. Muimbaji huyo hakuwahi kuzungumza chochote kuhusu mrembo huyo, lakini binti huyo anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake ameamua kufunguka kupitia mtandao wa instagram kuonyesha jinsi gani anampenda mkali huyo wa wimbo, ‘Natafuta kiki’. “Nakupenda sana mumewangu hakuna wakufanana na wewe mm bado sijaona  ,” aliandika instagram mrembo huyo huku akiwa amepost picha hapo chini.

MREMBO JOKATE ATHIBITISHA RASMI UHUSIANO WAKE WA KIMAPENZI NA ALI KIBA

Picha
Uhusiano wa Jokate na Alikiba una takriban miaka miwili sasa lakini hakuna hata mmoja aliyewahi kukiri hadharani. Waswahili husema penzi ni kikohozi, kulificha huwezi. Ndio maana pamoja na kujitahidi sana kuuficha, uzito wa penzi lao umekuwa ukiacha mianya mingi inayodhihirisha uwepo wake mbele ya hadhira. Na sasa huenda Jokate akawa ameuweka wazi zaidi kwa salamu za birthday alizomtumia mpenzi wake huyo aliyesherehekea siku yake ya kuzaliwa, November 29. Akijaribu kutomwaga mchele kwenye kuku wengi, Jojo ametumia lugha ya Kifaransa kuwasilisha ujumbe wake. Shabiki mmoja anayeielewa lugha hiyo ametafsiri post yake kwa Kiingereza inayosema: Baby happy birthday I love you so much,it is paining,I hope that the French has sang you prepare for that, but I want nothing,but the best for you from the bottom of my heart the rest I leave to God for what happens to know that Jojo doesn’t disturb and that am happy to have you as my friend,rest blessed

Pesa aliyoitoa Messi kwa familia za wachezaji waliofia katika ajali ya ndege

Picha
Bado dunia na ulimwengu wa soka kwa ujumla unaomboleza msiba wa msafara wa timu ya  Chapocoense  ya  Brazil  uliyopata ajali ya ndege wakati wakielekea kutua uwanja wa ndege wa  Medellin Colombia,  kwa ajili ya kucheza mchezo wao wa kwanza wa fainali ya Sudamericana  dhidi ya  Atletico Nacional  ya Colombia. Ajali hiyo ya ndege imesababisha vifo vya watu 76 kati ya 81 waliokuwemo ndani ya ndege hiyo huku watu 72 wakitajwa kuwa ni msafara wa timu hiyo, mshambuliaji wa  FC Barcelona  na timu ya taifa ya  Argentina  ambaye pia anatokea bara la  America Kusini   Lionel Messi ameguswa na msiba huo. Kupitia mtandao wa  fcbarca.me  umeripoti kuwa  Lionel Messi  ameamua kutoa euro milioni 5.3 ambazo ni zaidi ya Tsh bilioni 12.2 kwa timu ya   Chapecoensea  na familia za wachezaji wa timu hiyo,  Lionel Messi anaungana na staa mwenzake  Cristiano Ronaldo  ambaye ametoa z...

Chadema: Hatutakubali tena kudhulumiwa 2020

Picha
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) ,Vincent Mashinji amesema hawatakubali tena kudhulumiwa kwa namna yoyote  katika uchaguzi wa mwaka 2020. Dk. Mashinji amesema hayo huku akimtolea mfano wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, na kuongeza kuwa kuna mambo hutokea bila kutarajia lakini watapambana kwa kila hali, “Huu ni uchaguzi kuna mtu alitarajia haya yaliyofanywa na Jecha? hii inaonyesha kwenye nchi yetu bado kuna tatizo la utendaji haki, wewe umefanya mara ya kwanza tukanyamaza,ukafanya tena mara ya pili kibabe,tukalalamika, badala ya kutuita tuongee, unasema nendeni mkaseme kokote kule” alisema Mashinji. Aidha, akiongelea utawala wa Rais Magufuli ,Mashinji amesema kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa utawala bora na matokeo yake yeye ndio amekuwa kila kitu, ameongeza kuwa wakati anaanza  mapambano na rushwa aliamini kwamba angeweza kuliondoa tatizo hilo lakini imekuwa tofauti. Hata hivyo, Mashinji ameongeza kuw...

RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 47 & 48

Picha
Mwandishi: EDDAZARIA G.MSULWA ILIPOISHIA       Akaminya honi zake kwa nguvu ili mtu uyo kuweza kupisha njiani, na mbaya zaidi dokta Maliki aligundua amasimama katikati ya daraja la Sarenda. Kwa haraka akilini mwake akahisi ni majini ambao mara kwa mara inasadikika yanaonekana kwenye daraja hilo. Akawasha gari yake ila haikuwaka akajaribu kuliwasha gari lake ila halikuwaka kabisa. Mtu aliye simama mbele ya gari lake taratibu akaanza kugeuka huku sura yake akiwa ameiinamisha chini. Alipo inyanyua sura yake, macho ya Dokta Maliki yakamuona vizuri Samson akiwa amsimama mbele yake, huku akiwa tumbo wazi, mikononi mwake akiwa amshika bastola mbili zilizo elekea chini.    ENDELEA Samson hakuhitaji kumuacha hai dokta Maliki, akafyatua risasi zipatazo ishirini, zilizo vunja kioo cha gari ya dokta Maliki, na nyingi zikatua kifuani kwake na huo ndio ukawa mwisho wa maisha ya dokta Maliki. Samson akapiga hatua hadi kwenye gari la Dokta Maliki, akafungua...

DONEDEAL: Ngasa kasaini Mbeya City

Picha
Picha inayo-trend kwa sasa kwenye mitandao ya kijamii ni ya Mrisho Ngasa na afisa habari wa Mbeya City Dismas Ten ambayo inaashiria tayari nyota huyo wa zamani wa Yanga ameshakamilisha deal na ‘wagonga nyundo wa Mbeya’ Mbeya City. Mwezi Septemba mwaka huu Ngasa alijiunga na Fanja FC inayoshiriki ligi kuu nchini Oman (Oman Professional League) ikiwa ni wiki tatu baada ya kuvunja mkataba na klabu ya Free State Stars ya South Africa. Nyota huyo wa zamani wa vilabu vya Kagera Sugar, Yanga, Azam FC na Simba vyote vya VPL hajadumu nchi Oman na hatimaye amerejea tena nchini na kusajiliwa na klabu ya Mbeya City ambapo ataungana na kocha wake wa zamani Kinna Phiri aliyemsajili Free State Stars kabla ya kocha huyo kutimuliwa kufatia mfululizo wa matokeo mabovu. Afisa habari wa Mbeya City Dismas Ten amepost picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa pamoja na Mrisho Ngasa na kuandika maneno yanosomeka: “Mnapokamilisha jambo kutakiana heri ndio uungwana. Kila la heri an...

Rwanda yashtumiwa kupanga shambulizi la kutaka kumuua msaidizi wa Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza

Picha
Nchi ya Burundi imeishutumu Rwanda kwa madai ya kupanga kufanya majaribio ya kutaka kumuua msaidizi wa Rais Pierre Nkurunziza, Willy Nyamitwe. Msemaji wa jeshi la polisi kutoka Burundi, Pierre Nkurukiye amesema maagizo ya kufanywa kwa jaribio hilo lililofeli, yalitumwa kutoka nchini Rwanda kwa wapangaji waliotoka kwenye jeshi la Burundi. Nyamitwe alivamiwa alipokuwa akirudi nyumbani mwake Magharibi mwa Kajaga huko Burundi lakini si mara ya kwanza kupatwa na tukio kama hilo.  Mwezi Julai mwaka huu Burundi iliishtumu Rwanda kwa mauaji ya Mbunge wa Bunge la Afrika ya Mashariki, Hafsa Mossi aliyeuawa kwa kupigwa risasi mjini Bujumbura.

Rais wa Afrika Kusini atoa amri ya bendera kupeperushwa nusu mlingoti

Picha
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma atoa amri ya bendera ya taifa kupeperushwa nusu mlingoti ishara ya heshima kwa rais wa zamani wa Cuba Fidel Castro. Fidel Castro aliaga dunia Ijumaa iliyopita akiwa na umri wa miaka 90. Tayari bendera ya Afrika Kusini katika ubalozi wake nchini Cuba inapepea nusu mlingoti na itendelea kuwa hivyo hadi Desemba 4 ambapo mazishi ya Castro yamepangwa kufanyika . Vitabu vya rambi rambi tayari vipo katika jengo la muungano jijini Pretoria,jengo la Tuynhuys mjini Cape Town na taasisi za serikali kote nchini. Msemaji wa rais  Bongani Ngqulunga amefahamisha kuwa rais Zuma tayari ameondoka nchini kuelekea Havanna mapema siku ya Jumanne asubuhi kuhudhuria hafla ya mazishi ya Fidel Castro .

CHECK PESA ALIYOTOA RONALDO KWA FAMILIA ZA WACHEZAJI WALIOFIAKWENYE AJALI YA NDEGE

Picha
Bado dunia na ulimwengu wa soka kwa sasa unaomboleza msiba wa msafara wa timu ya Chapocoense ya Brazil uliyopata ajali wakati wakielekea kutua uwanja wa ndege waMedellin Colombia. Ajali hiyo ya ndege imehusisha watu 81 kati ya hao 76 wamepoteza maisha huku 72 kati ya hao walikuwa ni sehemu ya msafara wa timu hiyo na wachezaji wakielekea kucheza mchezo wao wa fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Atletico Nacionalya Colombia. Ronaldo Cristiano Ronaldo ni mmoja kati ya mastaa wa soka walioguswa kwa kiasi kikubwa na msiba huu, Ronaldo ameamua kuchangia euro milioni 3 ambazo ni zaidi ya Tsh bilioni 9.6 kwa timu ya Chipacoense na familia za wachezaji wa timu hiyo waliyopoteza maisha.

RC Paul Makonda Atuhumiwa Kuwadhalilisha Watumishi wa Umma kwa Kuwaita VICHAA........Tazama Video

Picha
KAULI mbalimbali zilizotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati wa ziara zake zimezua taharuki jijini humo. Kwa nyakati mbalimbali wakati wa ziara zake,  Makonda anadaiwa kutoa kauli za vitisho hasa kwa watumishi wa umma. Kutokana na hali hiyo, Chama cha ACT-Wazalendo kimemshtaki mkuu huyo wa mkoa katika Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Utawala Bora ili imuwajibishe. Katika taarifa yake iliyotumwa jana kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam na Katibu wa Ngome ya Wanawake wa chama hicho, Esther Kyamba alisema kauli alizozitoa Makonda zimewadhalilisha watumishi hao. “Tumesikitishwa na kuhuzunishwa na kauli zisizo za kiuongozi na zisizozingatia kanuni za maadili ya utumishi wa umma zinazoendelea kutolewa na RC Makonda. “Jana (juzi), katika mkutano anaouita wa kutatua kero kwa wakazi wa Dar es Salaam aliendelea kushindwa kutatua kero na badala yake kuongeza kero ya kudhihaki, kudhalilisha kukejeli na kutukana hadharani wananchi anaowaongo...

CHECK VIDEO UNAODAIWA MSAFARA WA AJABU WA RAIS MTEULE WA MAREKANE MH TRUMP

Picha

Jicho la 3: Yanga SC inamuhitaji Said Makapu mpya, si Mbuyu, namsubiri Justine Zulu

Picha
Na Baraka Mbolembole SAID Juma Makapu alianza vizuri majukumu yake kama mchezaji wa Yanga SC msimu wa 2014/15. Japokuwa alikuwa kijana mdogo kiumri, huku akitokea upande wa pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania-namaanisha Zanzibar mchezaji huyo wa nafasi ya kiungo wa kati alikuwa mgumu kupitika. Anajua kukaba, anajua kucheza faulo-jambo muhimu kwa mchezaji wa nafasi ya kiungo, anajua kupiga pasi zenye mwelekeo, pia alikuwa na mbio nzuri ndani ya uwanja. Nilitegemea mambo mengi mazuri kutoka kwa kijana huyu ambaye tayari alishapata nafasi ya kuitwa katika timu ya Taifa ya Tanzania. Msimu wake wa pili Yanga (2015/16) haukuwa mzuri, na sababu kubwa ya kushindwa kupandisha kiwango chake zaidi ni majeraha ya mara kwa mara. Wengi tulidhani Hans van der Pluijm angependekeza kuachwa au kutolewa kwa mkopo kwa mchezaji huyo wa timu ya Taifa ya Zanzibar wakati wa usajili wa dirisha kubwa katikati ya mwaka huu, lakini mkufunzi huyo raia wa Holland aliendelea kulinda imani yake kwa mchezaji...

Selfie ya Diamond akiwa na BOXER Yazua Balaa Mitandaoni

Picha
Diamond Platnumz amezua balaa mtandaoni baada ya Jumanne hii kupost selfie akiwa amevalia kiboxer cheusi. Kwenye picha hiyo, Diamond aliandika: Straight from the Changing room!…I think i need to go back to the gym so that i can be more flexible on m 24th Pre-XMass Parformance in Dar Es Salaam. Licha ya kufunika kwa emoji kwenye eneo la sehemu zake za siri, selfie hiyo imesababisha hisia tofauti huku wengi wakimponda staa huyo kwa kukosa staha. Hizi ni baadhi ya comments: isaac_siame:  @diamondplatnumz sitaki kuamini kama mawaziri kama nape au makamba watatamani kuja tena wcb kuonana namsanii wa namna hii, hii itakucost au imekucost tayari @babutale busara zako azijatumika kushauri hii naanza kuona misingi ya heshima ulioitunza kwa mda mrefu ikipotea tausizehemasaleh:  You ‘ve a beautiful soul but I think sometimes you go over board,remember to much is given .much is expected,I respect the path Mom Tee is taking,don’t neglect her advices,you may need the...

Lipumba Amtaka Maalim Seif Aache Kudanganywa na Waganga wa Kienyeji

Picha
Mgogoro wa uongozi ndani ya Chama cha Wanachi (CUF) unaendelea kuzua mapya ambapo jana, Mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba alimvaa tena Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad. Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Makao Makuu ya chama hicho zilizoko Buguruni jijini Dar es Salaam, Profesa Lipumba alimtahadharisha Maalim Seif akimtaka aachane na ‘waganga’ kwani watamdanganya. Ingawa hakueleza ni waganga wa aina gani, Profesa Lipumba alimtaka Maalim Seif kukubali kuzungumza naye ili wamalize matatizo yao. “Haiwezi kubadilika kwamba Mwenyekiti wa chama hiki nikiwa hai hadi mwaka 2019… Maalim waganga watakudanganya sana, watakudanganya sana,” alisema Profesa Lipumba. “Katika hili lilitakiwa lisifike hapa, huna sababu, njoo tuzungumze, pokea simu yangu unajua namba yangu tuzungumze tuyamalize uje nikupangie kazi,” aliongeza. Mchumi huyo alisisitiza k...

UKIMWI sasa kudhibitiwa kwa njia ya simu

Picha
Tanzania imeingia rasmi kwenye mfumo maalum wa kimataifa wa kupata huduma za afya ya UKIMWI kwa njia ya simu bila malipo mfumo ambao umefadhiliwa na nchi ya Marekani. Akizindua mfumo huo Kaimu Balozi wa Marekani nchini Bi. Virginia Blaser amesema mfumo huo utawafikia zaidi ya watu laki nane huku lengo kuu la mfumo huo likiwa ni kupunguza maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi kutoka asilimia 7.5 mpaka asilimia 5 hadi kufikia asilimia 0.0. Amesema watu wote ambao wanadhaniwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Ukimwi hadi kufikia mwaka 2020 wawe tayari wamepimwa kwa asilimia 90, asilimia 90 waanze kutumia dawa, na asilimia 90 kiwango chao cha maambukizi kiwe kimepungua. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya TAYOA nchini Bw . Peter Masika amesema katika ufadhili wa mfumo huo wao wakiwa ni wasimamizi wa mfumo watahakikisha unawafikia watanzania wote hasa wale wasiofikiwa na huduma muhimu za kiafya na kuwataka watanzania kujitokeza kwa wingi kutumia mfumo huo ili kutokomeza ug...

Kauli ya Jeshi la Polisi Kuhusu Askari wake Aliyefariki Dunia Kwa Kujipiga Risasi

Picha
Jeshi la Polisi mkoani Pwani limezungumzia kifo cha askari wake PC Armand Furaha (33) aliyejipiga risasi kifuani bila kukusudia na kufariki dunia. Askari huyo alijipiga risasi hiyo usiku akiwa anaelekea kwenye lindo nyumbani kwa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha. Tulio hilo lilitokea saa moja usiku eneo la Mailimoja sokoni usiku wa kuamkia jana, wakati askari huyo akiwa njiani kuelekea kwenye kituo cha lindo alichopangiwa. Kaimu Kamanda wa Polisi Pwani, Blasius Chatanda amesema askari huyo alijipiga risasi bahati mbaya kwa bunduki aina ya SMG akiwa amekaa kwenye kiti cha mbele katika gari alilokuwa anasafiria kwenda lindoni. Amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa askari huyo alikuwa tayari ameweka risasi chemba kwenye bunduki hiyo aliyokuwa nayo na kwa bahati mbaya akiwa anashuka kwenye hilo gari ndipo risasi hiyo ikafyatuka na kumpiga kifuani eneo la kushoto na kufa wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Tumbi. “Kabla ya tukio hilo, askari huyu aliwasili kazini jioni na kuk...

Waziri Mkuu aziagiza shule na majeshi kuachana na kuni.........Waziri Maghembe Aahidi Kupandisha Kodi ya Mkaa Maradufu

Picha
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amezitaka taasisi za serikali zinazotumia kuni na mkaa kwa wingi kama vile shule na majeshi kuanza mikakati madhubuti ya kubadili mfumo wa kupikia na kuweka majiko ya gesi ili kupunguza matumizi ya mkaa ambayo yamekuwa chanzo cha uharibifu wa mazingira. Alisema hayo jana Dar es Salaam katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe wakati wa ufunguzi wa warsha ya wadau kujadili namna na njia bora ya kupunguza matumizi ya mkaa kwa usimamizi endelevu wa mazingira nchini. “Nimeelezwa kuwa makampuni yanayouza majiko na gesi ya kupikia aina ya LPG yameonesha nia ya kuweka majiko haya bila gharama yoyote. Tutumie vyombo vyetu vya habari na majukwaa ya mikutano kuhamasisha wananchi kutumia fursa hii ya LPG,” alisema Waziri Mkuu. Aidha, alisema nchi inakabiliwa na changamoto kubwa za uharibifu wa mazingira kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo ufugaji wa kuhamahama, mifugo kuvamia misitu na kuiharib...

Sakata la Kununua Viewers You Tube: Ommy Dimpoz Aumbuliwa na Mwakilishi wa You tube E.Africa

Picha
Baada ya Ommy Dimpoz kumtuhumu wazi wazi Nassibu Abduli kuwa ana nunua views na tunzo bila kuwa na uthibitisho na bila aibu Ommy ili kuwathibitishia watu kuwa kuwa watu hununua views alisema kuwa hata yeye aliwai kutaka kununua... Lakini kabla ya hayo tuhuma hizo dhidi ya Nasibu Abduli zilikuwa zinatolewa kwa uwoga na msanii Ali salehe lakini wengi wafatiliaji walikuwa wanaelewa kuwa anaye tuhumiwa ni Nasibu Abduli.. Wanasema uongo ukiongelewa sana bila kukanushwa au kutolewa ufafanuzi hugeuka kuwa ukweli na wale wsiojua ndio huamini kabisa ni kweli. Leo Clouds Fm waliamua kumtafuta muwakilishi wa You tube East Africa kumuuliza kama kweli watu wanaweza kununua views au viewers na wao wasigundue na kuchukua hatua.. Kwanza Mwakilishi yule aliweka wazi kabisa wao hapa East Afrika wanasimamia na ku control you tube channel za wasanii baadhi East Africa na kwa Tanzania wanasimamia Channel za kina AY,Mwana FA, wasanii wa wasafi wote na Alikiba. Mwakilishi huyo aliendelea kufafanua kuwa...

Magazeti Ya Leo Jumatano ya Novemba 30

Picha