Rais wa Afrika Kusini atoa amri ya bendera kupeperushwa nusu mlingoti


Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma atoa amri ya bendera ya taifa kupeperushwa nusu mlingoti ishara ya heshima kwa rais wa zamani wa Cuba Fidel Castro.

Fidel Castro aliaga dunia Ijumaa iliyopita akiwa na umri wa miaka 90.

Tayari bendera ya Afrika Kusini katika ubalozi wake nchini Cuba inapepea nusu mlingoti na itendelea kuwa hivyo hadi Desemba 4 ambapo mazishi ya Castro yamepangwa kufanyika .

Vitabu vya rambi rambi tayari vipo katika jengo la muungano jijini Pretoria,jengo la Tuynhuys mjini Cape Town na taasisi za serikali kote nchini.

Msemaji wa rais  Bongani Ngqulunga amefahamisha kuwa rais Zuma tayari ameondoka nchini kuelekea Havanna mapema siku ya Jumanne asubuhi kuhudhuria hafla ya mazishi ya Fidel Castro .