Zaidi ya asilimia 91 ya wanafunzi chuo cha Kampala wakosa mikopo.

Waziri wa elimu Prof Joyce Ndalichako ameombwa kuingilia kati sakata la wanafunzi wa chuo kuu cha Kampala cha jijini Dar es Salaam ambao zaidi ya asilimia 91 ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza wamekosa mikopo huku wengi wao wakionekana kukata tamaa ya kuendelea na masomo yao baada ya kukosa mikopo.

Ujumbe wa wanafunzi hao ukiongozwa na waziri wa elimu wa chuo hicho cha Kampala uliwasili katika kituo cha matangazo cha ITV Mikocheni Dar es Salaam majira ya mchana huku wengi wao wakionekana dhahili kukata tamaa kwa kile walichodai ni majibu yasiyoridhisha waliyojibiwa na maafisa wa bodi ya mikopo.

Takwimu zinaonyesha wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliodahiliwa 2016/17 katika chuo cha Kampala ni wanafunzi 1486, ambapo ni wanafunzi 135 pekee ndio waliokwisha kupata mikopo huku wanafunzi 1359 wakiwa hawajui nini cha kufanya ikiwa ni siku chache kabla ya wao kufanya mitihani yao.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: UTAMU WA MADAM JESCA

Simulizi; MTOTO WA BOSS WANGU

SIMULIZI FUPI: UCHI WANGU UMENIPONZA