Kwa mashabiki wa Chelsea wanakumbuka kwa kiasi kikubwa wakati Willian alivyokua anafanya vizuri wakati yupo chini ya Jose. Muda wa Willian chini ya Conte umekua mgumu sana na anashindwa kuonyesha uwezo wake ambao watu wamemzoea.
Kikosi cha Blues kimeonekana kuwa vizuri baada ya kushinda mechi sita na za ligi na Willian akiwa hana mchango mkubwa. Baada ya story kuvuma kwamba Mourinho angependa kuwa na mchezaji huyo ndani ya O.T, waandishi wa habari walimuuliza manager Conte kuhusu future ya Willian ndani ya club hiyo.
Conte alijibu,“Anarudi kwenye kiwango chake, Willy ni mchezaji muhimu kwetu na nina mtegemea sana. Kwa sasa hivi ni muhimu kutafuta mazuri kwake kwa sababu amekua hana bahati kwa muda mrefu na kila mtu anajua kwa nini”.
Mwezi wa kumi Willian alifiwa na mama yake na baada ya hapo hakuwa na kiwango kizuri uwanjani. Chelsea inaelekea kucheza mechi muhimu dhidi ya Tottenham.