Inasemekana kwamba Martial hakufurahishwa na kitendo cha namba 9 kupewa Zlatan wakati yeye akiwa anajiandaa kuanzisha logo yake ya Martial 9. Lakini hayo yote hayamhusu Morihno ambae anataka kila mchezaji acheze kwenye kiwango cha juu.
Jose alisema,“Unapopewa nafasi ya kwanza, ya pili na ya tatu na hauonyeshi makali basi inabidi apewe mtu mwingine aonyeshe hayo makali. Anthony alikua sawa dhidi ya Feyenoord lakini siwezi kucheza wachezaji 12. Wachezaji inabisi wagombani nafasi zao kwenye kikosi. Wao ni mrafiki wakaribu sana lakini lazima washindane wao kwa wao ili wapate nafasi ya kushinda”.
Jose Mourinho aliendelea kwa usema kwamba wana uchaguzi mkubwa wa wachezaji kwenye nafasi za mbele hivyo basi lazima kila mtu acheze vizuri,“Anahitaji kuendelea kufanya vizuri sana hasa kwenye nafasi ambayo tuna uchaguzi mkubwa wa wachezaji kama Mkhitaryan, jesse, depay,Mata,Rashford. Hizi ni nafasi ambazo tuna uchaguzi mkubwa”