SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumapili, 27 Novemba 2016

T media news

MAJIBU YA DC HAPI KUTOKA KWA RAIS MAGUFULI KUHUSU HATIMA SHAMBA LA SUMAYE MABWEPANDE

AMINI NYAUNGO
Wananchi wa Wilaya ya Kinondoni ambao wanaishi Mji mpya Mwabepande walikuwa na hamu kubwa kupata matokeo ya mwisho juu ya sakata la Ardhi ambayo alikuwa anamiliki Waziri mkuu wa zamani wa awamu ya tatu Fredrick Sumaye dhidi ya wananchi.

Majibu aliyokuja nayo Ally Salum Hapi ambayo yametoka kwa Rais John Pombe Magufuli kuwa amefuta hati miliki zote za umiliki wa shamba ambalo alikuwa ana miliki Sumaye na sasa umiliki wa shamba hilo limerudishwa kwa Manispaa ya Kinondoni,Hivyo basi kuanzia sasa shamba hilo la Manispaa ya Kinondoni.
Hapi amesema Manispaa itakaa na kupanga namna ya matumizi ya shamba hilo, lakini pia amewataka wote waliokuwa katika mgogoro huo watafikiriwa kwa masharti ya Manispaa itakavyokaa kigezo kikubwa wanatakiwa wafuate maagizo ambayo Manispaa itakavyoamua.

Katika kuendelea kumuunga mkono Rais Magufuli Hapi amemoumba kuendelea na harakati zake anazo endelea nazo hivi sasa na namna alivyowasaidia wakazi wa Mabwepande

Wakati huo huo Katika ziara fupi aliyoifanya Mkuu wa Wilaya amepitia katika soko la Bunju ambapo ametoa agizo kuanzia jumatatu wafanya biashara wote wanatakiwa kufanyia biashara zao ndani ya soko ambalo Manispaa imelitengeneza kwa ajiri ya kuweka utaratibu uliosahihi ambao Manispaa umeutengeneza. Ama mapungufu katika soko hilo pamoja nakupungua kwa wafanyabiashara katika soko hilo kutokea 1119 hadi kufikia 179 .