Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili, 2018

Manara amfungukia beki wa Yanga aliyemtemea mate Asante Kwasi

Picha
Soka ni burudani na siyo vita. Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano Simba, Haji Manara ametoa povu zito kutokana na kitendo cha beki wa Yanga Kevin Yondani kudaiwa kumtemea mate Asante Kwasi kwenye mchezo uliochezwa jana (Jumapili) katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yondani ameonekana kwenye vipande vya video akimtemea mate Kwasi wakati alipokuwa akimzuia kwenye goli la Yanga wakisubiri kupigwa kwa mpira wa kona. Kupitia mtandao wa Instagram, Manara ameonyesha kukerwa zaidi na tukio hilo kitendo ambacho amemuahidi mchezaji wao Kwasi watalifanyia kazi kuhakikisha mambo kama hayo hayajirudii tena. Huyu jamaa ni mshamba.mtu asiye na ustaarabu. bwege na hastahili kuachwa hv hv..ni tukio la hovyo zaid nchini kwa mwaka huu..nilikuwa namheshimu kama senior player ila kwa sasa namuona ni zaidi ya takataka..usela wa kihayawani..chuki hyo ya nn?nyie mmeshinda mara ngapi mbona hamjatemewa makohozi ?vtendo hv lazma vilaaniwe na kila mmoja…..kwasi nakuahidi hili jambo tutali...

Harusi ya Alikiba Kiboko Viongozi wa Serikali Wamiminika Ukumbini ..... Mama Salma Kikwete Ummy Mwalimu Waudhuria Kigwangala Atoa Zawadi Hii

Picha
Usiku wa jana imefanyika sherehe nyingine ya harusi ya Alikiba na mkewe Aminah Rikesh Ahmed na mdogo wake Abdu Kiba na Ruwayda katika ukumbi wa Serena Hotel jijini Dar es Salaam. Sherehe hiyo ilifaana zaidi baada ya kuhudhuriwa na watu lukuki wakiwemo wazazi wa wana ndoa wote na watu maarufu pamoja na viongozi wa serikali akiwemo mke wa rais wa awamu ya nne, Mama Salma Kikwete, Waziri wa Àfya, Ummy Mwalimu, Naibu Waziri wa Kazi, Anthony Mavunde, Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangalla na Gavana wa mji wa Mombosa, Hassan Joho ambaye pia ni mtu wa karibu wa msanii Kiba. Mama Salma KKikwete (kushoto) akiwa na Waziri wa Àfya, Ummy Mwalimu Katika sherehe hiyo Waziri Kigwangala amewataka maharusi wote kuchagua sehemu yoyote ya kitalii ndani ya Tanzania kwenda kufanyia fungate yao na yeye atagharamia kila kitu.

Ali Kiba azindua kinywaji chake MOFAYA

Picha
Msanii wa Bongo Fleva, Alikiba ametumia sherehe ya harusi yake kuzindua rasmi kinywaji chake kinachofahamika kwa jina la Mofaya katika ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambako harusi hiyo ilikuwa ikifanyika usiku wa kuamkia leo Jumatatu. Kinywaji hicho cha Mofaya hakina kilevi.

Manara afunguka kipigo walichokipata Yanga jana ni cha heshima

Picha
Afisa Habari wa vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba SC, Haji Manara amefunguka na kudai kipigo walichokipata Yanga jana Aprili 29, 2018 cha bao 1-0 ni cha heshima kutokana na wao kuwa mabingwa watetezi hivyo isingekuwa vizuri kuwadharaulisha mbele ya umati wa mashabiki. Manara ametoa kauli hiyo mara baada ya 'Kariakoo Derby' kumalizika katika uwanja vya Taifa Jijini Dar es Salaam huku timu yake ikiwa imetoka na ushindi wa bao 1 lililofungwa mnamo mwa dakika 38 kupitia Erasto Nyoni kwa kutumia kichwa akiunganisha krosi ya Kichuya. "Tunamshukuru Mwenyezi Mungu tumepata matokeo ila hatujaridhika bado mpaka tuwe mabingwa, 'perfomance' yetu kwa ujumla ilikuwa nzuri ndio maana hata 'corner' moja wenzetu hawakuweza kupata lakini sisi vilevile tulicheza kwa heshima", amesema Manara. Pamoja na hayo, Manara ameendelea kwa kusema "kipindi cha kwanza kilipomalizika nilishuka chini nikazungumza na wachezaji wangu kuwa waende wakawafunge Yanga kwa heshim...

Mwameja ataja sababu iliyowaangusha Yanga

Picha
Mlinda mlango wa zamani wa Simba, Mohamed Mwameja, ameeleza furaha yake kutokana na timu yake kuibuka na ushindi dhidi ya watani zao wa jadi, Yanga. Mwameja aliyewahi kung'ara na kikosi hicho cha wekundu wa Msimbazi miaka ya nyuma na kujiwekea rekodi ya kuwa mmoja wa makipa bora kwenye soka la Tanzania hapa nchini, amefurahi ushindi huo akisema Simba walikuwa na kikosi kipana. Mbali na furaha ya ushindi, Mwameja ametaja sababu iliyowaangusha Yanga dhidi ya Simba jina ni majeruhi walionao kwenye kikosi chao. Kipa huyo wa zamani ameeleza kukosekana kwa baadhi ya wachezaji kama Donald Ngoma, Thaban Kamusoko, Amis Tambwe ambao ndiyo mhimili wa timu kumesababisha kikosi cha Yanga kuwa dhaifu kwenye mchezo wa jana.

Rais wa Nigeria kuwa kiongozi wa kwanza wa Afrika kulakiwa na Donald Trump Marekani

Picha
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari atakuwa kiongozi wa kwanza wa taifa la kutoka bara Afrika kulakiwa na Rais wa Marekani Donald Trump White House atakapokutana na kiongozi huo kwa mashauriano rasmi mjini Washington baadaye leo. Marais wengine wa Afrika wamewahi kukutana na Bw Trump akiwa rais, wakiwemo Paul Kagame wa Rwanda na Uhuru Kenyatta wa Kenya, lakini nje ya Marekani. Rais Kenyatta alikutana na Trump pambizoni mwa mkutano wa G7 nchini Italia mwezi Mei mwaka jana, naye Rais Kagame akakutana na kiongozi huyo wa Marekani Januari mwaka huu mjini Davos, Uswizi pambizoni mwa mkutano mkuu kuhusu uchumi wa dunia. Septemba mwaka jana, Rais wa Uganda Yoweri Museveni pia alikutana na kupigwa picha na Rais Trump kwenye dhifa iliyoandaliwa wakati wa mkutano wa viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa jijini New York. Hakukuwa na mazungumzo yoyote hata hivyo na haikuwa ziara ya kikazi kwa Bw Museveni. Wawili hao wanatarajiwa kujadiliana kuhusu masuala ya kiuchumi na kiusalama wataka...

Adhabu iliyotangazwa kwa watakaokamatwa wametupa takataka hovyo Jijini Dodoma

Siku tatu baada ya Rais Dkt Magufuli kuipandisha hadhi Manispaa ya Dodoma kuwa Jiji, Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi amesema kuwa, mtu yeyote atakayekamatwa akitupa takataka hovyo, atakamatwa na kutozwa faini ya TZS 50 milioni, ikiwa ni kwa mujibu wa sheria ndogo za usafi. Mkurugenzi Kunambi ameyasema hayo jana Aprili 29 wakati akizungumza na wafanya usafi ndani ya jiji hilo ambapo alizundua mchakato wa kuwapati kadi za matibabu (bima za afya) ambazo wataweza kuzitumia wao na wategemezi wao wanne. Katika mkutano huo, alitoa kadi 10 kama kuonesha kuanza kwa mchakato huo. Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Binilith Satano Mahenge   alisema kuwa, baada ya Rais Dkt Magufuli kupandisha hadhi manispaa hiyo, zawadi ya kwanza watakayotoa kwake, ni kuhakikisha kuwa jiji hilo linakuwa safi muda wote. Amesema jiji hilo lazima liwe mfano kutokana na shughuli zinazofanyika hapo, na watu wengine waje kujifunza kutoka kwao. Katika hatua za wali, RC Mahen...

Msafara wa Rais Magufuli Wasimamishwa Barabarani.,.......Atoa Ujumbe Mzito Kwa Wakazi Iringa

Picha
Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, umesimamishwa na wananchi wa eneo la Migori mkoani Iringa ili kutoa kero zao zinazowakabili, kwa kiongozi huyo mkubwa wa nchi. Msafara huo ambao ulikuwa ukipita kuelekea mkoani Irnga kwa ajili ya tukio la uzinduzi wa barabara ya Iringa Migori  yenye urefu wa km 189, umelalamikiwa kero mbali mbali zinazowakabili wananchi wa eneo hilo pamoja na changamoto zinazoikabili shule ya sekondari Nyerere iliyopo mkoani Iringa, na kutoa fedha taslim shilingi milioni 5 ili kusaidia ujenzi wa madarasa na nyumba za walimu. Baada ya Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Walend Manga kuelezea hatua walizofikia za ujenzi wa nyumba za walimu wanazojenga kwa nguvu yao na wananchi, pamoja na kumshukuru Rais Magufuli kwa fedha zinazopelekwa mashuleni, Rais Magufuli alisikika akisema ..."Ahsante sana Mwalimu Mkuu, shule yenu ina jina zuri, jina la Nyerere, na mimi nitawaongezea milioni 5, sina milioni tano hapa!!? Hebu nisaidie hapa hap...

Breaking News:Mahakama Yatoa Amri Hans Pop wa Simba Akamatwe

Picha
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa amri kwamba mwenyekiti wa usajili wa Simba SC, Zacharia Hans Poppe na Franklin Lauwo wakamatwe na wafikishwe mahakamani kuunganishwa katika kesi inayomkabili Rais wa Klabu hiyo, Evans Aveva na Makamu wake Kaburu. Amri hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba baada ya Wakili wa TAKUKURU, Leonard Swai kubadilisha hati ya mashtaka na kuwaongeza watuhumiwa hao. Swai amedai amewatafuta washtakiwa hao toka mwezi wa tatu bila mafanikio na kuomba hati ya kuwakamata washtakiwa hao ambao hawakuepo mahakamani. Washtakiwa hao wameongezwa katika kesi ya utakatishaji fedha na kugushi inayomkabili Rais wa Simba, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ .

Bunge Lakanusha Kumtimua Cyprian Musiba Bungeni

Picha
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limekanusha taarifa zilizodai kuwa Mkurugenzi wa CZI, Cyprian Musiba amefukuzwa Bungeni. Taarifa hizo ziliibuka mara baada ya kuwepo picha mtandaoni ikimuonyesha Musiba ‘akizozona’ na baadhi ya watumishi wa Bunge. Kupitia ukurasa wa Twitter wa Bunge wamefafanua kuhusiana na hilo; Picha zinazosambaa kwenye mitandao zikidai kuwa Mkurugenzi wa CZI Ndg. Cyprian Musiba amefukuzwa Bungeni si kweli. Musiba amekidhi vigezo vya kusajiliwa kuripoti habari za Bunge na kwamba alikuwa akihamishwa kwenda katika jukwaa mahsusi ambalo Waandishi hukaa wawapo Bungeni. Musiba ni Mhariri wa Gazeti la Tanzanite na Mwanasheria, hivi karibuni alifunguliwa kesi na Mjasiriamali/Mwanahabari na Mkurugenzi wa Compass Communications, Maria Sarungi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa madai ya kumkashifu na kuchafua jina lake kupitia mkutano wake na Waandishi wa Habari uliyofanyika February 25, 2018.

Faida Tanzania iliyopata baada ya kupokea ndege kubwa ya Emirates

Picha
Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Hamza Johari amesema, kufuatia huduma waliyoitoa kwa ndege ya Emirates iliyotua nchini kwa dharura, Tanzania sasa imepanda katika viwango vya kimataifa na kufikia asilimia 64 kutoka asilimia 37 vilivyowekwa na Shirika la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO). Ndege hiyo ya gharofa iliyotua kwa dharura nchini, ilikuwa na abiria zaidi ya 400 na wote walihudumiwa katika hoteli mbalimbali jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi huyo amesema, kufuatia hatua hiyo sasa Shirika la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) limeandaa tuzo maalum itakayotolewa na Rais wa shirika hilo kwa kumkabidhi Rais John Magufuli na mawasiliano yanafanyika kufuatia ujio huo wa Rais wa ICAO. Akizungumza na waandishi katika Ofisi za Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), mkurugenzi huyo amesema, kutua kwa ndege hiyo kubwa ya ghorofa aina ya A380 ya Shirika la Ndege la Fly Emirates kumedhihirisha kuwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere na vyombo vyake ...

Familia 208 za watoto waliotelekezwa na baba zao, zaanza kupata huduma

Picha
Zaidi ya familia 208 za watoto waliotelekezwa na baba zao, zimepatanishwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Paul Makonda. Hayo yamebainishwa jana Aprili 27 na Makonda wakati akitoa majumuisho ya zoezi la kuwasikiliza wanawake waliotelekezwa na wenza wao wakiwa na watoto. Kadhalika Makonda, hakuacha kuwashukuru waandishi wa habari kwa kufanya kazi kubwa katika kuhabarisha umma kuhusu kampeni yake. “Kwanza niwashukuru waandishi wa habari kwa kazi nzuri mliyofanya, lakini pia niwashukuru wote walionitukana kwa kuanzisha zoezi hili wakiwamo wabunge,"alisema. Alisema zoezi hilo limefanikiwa kwani  familia 208 zimeanza kupata huduma kutoka kwa baba zao. Kadhalika amesema, kati ya watu 17,000 waliofika ofisini kwake, 90 wamefanikiwa kupimwa uhalali wa baba kwa mtoto ( DNA) na watoto 2971 wakifanikiwa kupata  bima ya afya. "Tumeunda tume ya watu 15 watakaofuatilia kwa kina matatizo ya kiutawala katika kushughulikia masuala  yanayohusu jamii kwani imeonekana kuna shida kubw...

Rais achukua hatua hizi dhidi ya waliohujumu fedha za mradi wa maji Dodoma

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amevitaka vyombo vya dola kuwatafuta  na kuwafikisha mbele ya  vyombo vya sheria wahusika waliohujumu kiasi cha shilingi bilioni 2 katika mradi wa maji wa Ntomoko ulioko wilayani Kondoa. Rais Magufuli aliyasema hayo jana wilayani Kondoa alipokuwa akifungua Barabara ya Dodoma hadi Babati yenye kilomita 251. “Wahusika watafutwe ili warudishe fedha walizochukua au wahakikishe mradi unakamilika. Ni lazima watu waogope mali ya watu masikini,” alisema Rais Magufuli. Ameendelea kwa kusema, kama viongozi wanawajibu wa kuchukua hatua hata kama zinauma lakini ni kwa manufaa ya Watanzania milioni 55. Wakati huo huo, Rais Magufuli amewataka wananchi wa wilaya ya Kondoa kuitunza miundo mbinu ya barabara ambayo ameizindua. Aidha amesema wapo Wananchi ambao wamekuwa wakiondoa alama za barabarani na kwenda kutengenezea tela za ng’ombe au kujengea vyoo.

Makonda Mgeni Rasmi Simba Vs Yanga Jumapili April 29

Picha
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Paul Makonda atakua mgeni rasmi wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara utakaowakutanisha Simba na Yanga utakaochezwa Jumapili Aprili 29,2018 Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam. Ndugu Makonda atawaongoza maelfu ya mashabiki wa mpira wa miguu watakaojitokeza kweye Uwanja wa Taifa kushuhudia mchezo huo namba 178 utakaoanza saa 10 jioni. Tayari tiketi za mchezo huo zinaendelea kuuzwa ambapo VIP A ni shilingi 30,000,VIP B na C 20,000 na Mzunguko(Jukwaa la rangi ya Chungwa,Kijani na Bluu) 7,000. Tiketi zinapatikana kupitia Selcom. Katika mchezo huo Simba wanaingia uwanjani wakiwa wanaongoza ligi baada ya kujikusanyia pointi 59 ikicheza michezo 25 wakati Yanga wana pointi 48 wakiwa nafasi ya pili baada ya kucheza michezo 23.

Waziri Mkuu Awaonya Viongozi wa Vyama vya Siasa

Picha
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwaamewataka viongozi wa vyama vya siasa wajitahidi kuwa makini na namna wanavyoendesha vyama vyao kwa sababu wananchi wanaowaongoza ni wa vyama vyote. Pia amewaasa viongozi wa Baraza la Vyama vya Siasa waendelee kushikamana ili waweze kulifikisha Taifa mahali ambapo Watanzania wanapatarajia ikiwa ni pamoja na kupunguza umaskini. Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Aprili 27, 2018) wakati akizungumza na Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa katika ukumbi wa mikutano wa Waziri Mkuu ulioko Mlimwa jijini Dodoma. “Viongozi wa vyama vya siasa wanatakiwa wajitahidi kuwa makini na namna ambavyo wanaendesha siasa katika vyama vyao, wananchi wanaowaongoza ni wa vyama vyote hivyo tupeleke ujumbe ambao utawaongoza kujileta maendeleo.” Waziri Mkuu amesema kuwa mazungumzo yaliyofanyika leo baina ya Serikali na viongozi hao yameonesha nia ya pamoja ya kuendeleza ushirikiano. Pia amesema wana wajibu wa kuendeleza historia nzuri kwani siasa ni moja ya nyenzo zi...

Gigy Money ajifungua Mtoto wa Kike

Picha
Msanii wa muziki wa bongo fleva nchini  Gift Stanford maarufu kama  Gigy Money, amefanikiwa kujifungua salama mtoto wa kike na kumpatia jina la  Myra. Gigy Money anatoka kimapenzi na mtangazaji wa Choice FM, Mo J ambaye pia ni baba mzazi wa mtoto huyo aliyezaliwa jana. Gigy na Mo J kabla ya kuzaliwa kwa mtoto huyo walikuwa wakijiita Baba Candy na Mama Candy ila mara baada ya kuzaliwa kwa mtoto huyo wamesema hawatatumia tena jina hilo na tayari wamempa mtoto wao jina la  Myra.

Yasome hapa magazeti ya leo Jumamosi Aprili 28, 2018

Picha

Majonzi Yatawala, Kuagwa Kwa Mwili Wa Mtoto Aliyechomwa Kisu Na Dada Yake

Picha
Mtotro Joshua Michael (2) aliyeuawa na dada yake Delta Kalambo (19) kwa kuchomwa kisu kwenye kitovu na mwili wake kufichwa uvunguni unazikwa leo Sengerema mkoani Mwanza. Simanzi ilitawala watu waliojitokeza kuuaga mwili wa mtoto huyo nyumbani kwao Kigamboni jana huku baadhi wakieleza kuumizwa na unyama uliofanyika kwa mtoto huyo. Tukio la kuuliwa kwa mtoto huyo lilitokea Jumatatu katika eneo la Tungi Mwembepoa, Kigamboni jijini Dar es Salaam wakati mama wa mtoto ambaye ni muuguzi wa Hospitali ya Mkuranga, Magreth Kasedi, akiwa kazini. Msemaji wa familia ambaye ni baba mkubwa wa marehemu, Deus Philipo, jana alisema marehemu huyo atazikwa leo mkoani Mwanza. Alisema mazishi yatafanyika katika kijiji cha Nyabila endapo wasingekutana na changamoto barabarani. "Nashindwa kusema tutazika kesho (leo) kwa sababu hatujui huko njiani safari itakuwaje ila tukifika mapema tutazika," alisema. Kasedi alisema  juzi kuwa Jumatatu aliamka asubuhi kama kawaida na kumuacha mtoto wake na D...

Boti Yapinduka Ziwa Victoria na Kuua Wawili

Picha
Watu wawili wamefariki dunia baada ya boti waliyokuwa wakitumia kusafiria kupinduka. Ilipokumbwa na dhoruba kali katika ziwa Victoria, Sengerema jijini Mwanza. Akizungumza  kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi, amesema boti hiyo ilikuwa na jumla ya watu watano ambao walikuwa wa wakisafiri kutoka Sengerema kuja Mwanza, na ndipo ilipokumbwa na dhoruba wakiwa njiani, na kusababisha boti hiyo kupinduka na watu hao kufariki. “Kuna boti ilikuwa inatoka Sengerema kuja huku Mwanza, ilikuwa imebeba mkaa pamoja na udaga, walivyokwenda kama robo safari yao hali ya hewa ikawa mbaya kukawa na dhoruba, wakiwa wanageuza wanarudi ikawa shida ikapinduka, ndani ya hiyo boti kulikwa na watu watano, wanaume wanne mwanamke mmoja, watatu waliweza kuogelea lakini hawa wawili walishindwa, mwanamke na mwanaume mmoja, majina bado sijayapata”, amesema Kamanda Msangi. Kamanda Msangi amesema miili ya watu hao imepatikana, na wanafanya utaratibu wa k...

KUNA MBEGU IMEOTESHWA JANA, TUSIIDHARAU.

Picha
Na Thadei Ole Mushi Kuna tofauti kati ya terminologies hizi mbili. 1. Rebellion 2. Revolts Rebellion ni kukataa kufuata sheria za nchi huku revolts ni kutaka kufanya mapinduzi. Usipoweza kutofautofautisha vitu hivi viwili utajikuta matatizoni. Jana kilichotaka kufanyika ni Rebellion bila kujua lakini akilini kwa wanaotaka kufanya hivyo walifikiri ni kufanya revolts.  Kwa sheria za Tanzania si rahisi kama mnavyofikiria kufikia level za revolts mtaishia kufanya rebellion na mtaishia kufungwa. Hivyo kabla ya kufikiria kufanya mapinduzi angalia sheria za nchi, angalia nani anaongoza mapinduzi hayo, sababu za kuyafanya, Mtizamo wa jamii, uimara wa vyombo vya ulinzi na usalama. KWA SERIKALI Crane Brinton ni katika nadharia yake ya mapinduzi aliyoiandika kwenye kitabu chake cha " Anatomy of revolution" anafananisha mapinduzi na homa. Katika mazingira hayo Brinton anasema homa si jambo la kufurahia na linapaswa kuepukika au kutibiwa kwa mapema pindi dalili za homa...

Kanuni 4 Za kujenga Mahusiano Bora ya Kimapenzi

Picha
Hakuna binadamu asiyefahamu nini maana ya mapenzi na kama wapo basi ni wachache sana na wanaweza kuwa hawafahamu kwa maneno lakini kivitendo wanakuwa wanafahamu aidha kwa kuona, kusikia na hata kwa wao wenyewe kushiriki kwenye mapenzi hayo. Na hakuna binadamu yeyote asiyependa kupenda au kupendwa, wote tunapenda kupenda na pia tunapenda kupendwa in . Na siku zote ukipenda na usipopendwa pale unapopenda huwa inakuwa ni huzuni sana na wengine hufikia hatua mbaya sana za kufikiria mengine mengi tu ya hatari pale mapenzi yanapokuwa machungu kwao. Hii ndio sababu wengi wetu huwa tunakaa pale tunapoona kweli kuna mapenzi na si kukaa pale ambapo unaona unadanganywa au kuzungushwa kila siku. Lakini kuna wakati tunaweza kujikuta hata pale tunapopenda na kupendwa pia panaharibika baada ya muda na kunakuwa na ugomvi na kukosa maelewano baina yenu na wakati mwingine usifahamu kwa nini hamuelewani au ukaelewa lakini ukakosa njia za kutatua. Zifuatazo ni baadhi tu ya njia mbalimbali za kufanya u...

Kim Jong Un afanya ziara ya kihistoria Korea Kusini

Picha
Rais Kim Jong-Un wa Korea Kaskazini amekuwa kiongozi wa kwanza wa taifa hilo kuvuka mpaka wa kijeshi uliowekwa kuzitenganisha nchi hizo mbili baada ya vita ya mataifa hayo mawili mwaka 1953. Akiwa ni mwenye tabasamu rais Korea kusini Moon Jae-in amempokea mgeni wake katika eneo la mpakani. Ni miaka 65 hadi sasa kwa kiongozi wa Korea Kaskazini kuwahi kuvuka mpaka wa kijeshi uliowekwa kuzitenganisha Korea Kaskazini na Korea Kusini tangu kumalizika kwa vita vya mataifa hayo mawili mwaka 1953. Eneo la mpaka huo aliouvuka Kim Jong Un wakati akielekea Korea kusini ni lenye kilomita 250 na upana wa kilomita nne,ambapo mara baada ya kuuvuka tu watu walipiga makofi kwa kuandikwa kwa historia. Mkutano huo wa tatu baada ya mkutano wa mwaka 2000 na 2007 ni matokeo ya jitihada zilizofanyika miezi kadhaa kuimarisha mahusiano kati ya Korea hizi mbili na kufungua milango ya mkutano kati ya Kim na Rais wa Marekani Donald Trump. Kim alitangaza juma lililopita kuwa angesitisha zoezi la majaribio ya ...

Wema Sepetu: - Sitaki salamu ya Hamisa Mobeto

Picha
Nyota wa filamu nchini, Wema Sepetu amesema, hana bifu na Hamisa Mobetto, ila pia si rafiki yake. Wasichana hao walikuwa marafiki lakini hivi karibuni zilienea taarifa kuwa wamegombana. Wema ambaye ni Miss Tanzania 2006 amesema hana tatizo na msichana huyo ila alimchukia baada ya kupata taarifa kuwa alikuwa akimuongelea vibaya kwa watu. "Sina bifu na Hamisa ila siyo rafiki yangu kabisa kuna maneno aliniongelea mabaya… tena sio kwa kuhadithiwa, nilimsikia akiwa amerekodiwa… sasa nikaona huo ni unafiki kwa hiyo nikaona kila mtu achukue muda wake,"amesema Wema. Amesema, akikutana na Hamisa hataki salamu na mwanamitindo huyo, kila mtu afanye mambo yake. Hamisa amezaa na Naseeb Abdul ‘Diamond’ na hivi karibuni mwanamuziki huyo alitupia video ya wawili hao wakiwa kwenye mikao ya kimahaba. Wema na Diamond walikuwa wapenzi, waliachana na kurudiana takribani mara mbili kabla ya kuachana tena kwa ugomvi mpaka kufikia hatua ya kutosalimiana. Takriban miezi miwili iliyopita, ...

MremboTunda Acharuka na Kufunguka Haya "Mimi ni Mtu Mzima Najua Nachofanya"

Picha
Mlimbwende Tunda ambaye ni gumzo kwenye mitandao ya kijamii kutokana na urembo wake, amefunguka na kuwataka watu waache tabia ya kumfuatilia juu ya maisha yake binafsi anayoishi bali waangalie na kufuatilia kile anachokuwa amekiweka katika mitandao nasio vinginevyo. Tunda ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya watu wengi kujiuliza maswali mengi vichwani mwao huku wengine wakienda moja kwa moja kumuuliza yeye mwenyewe kuhusiana na kazi gani ambayo anaifanya kubwa ambayo kila uchao inamfanya ale bata sehemu zenye hadhi kubwa kila uchao. "Mimi napenda kuwaambia hao watu, wafuatilie vile ambavyo nimeamua kuviweka wazi na vile ambavyo sijaamua kuviweka bayana basi waachane navyo. Msitake kumuingia mtu kiundani sana 'some times' inakuwa ina boa, endapo nitaona sasa biashara yangu inafaa kuiweka kwenye mitandao nitaweka na kama sijaiweka waache na wanyamaze wanifuatilie mimi ninachokifanya", amesema Tunda. Pamoja n...