KUNA MBEGU IMEOTESHWA JANA, TUSIIDHARAU.



Na Thadei Ole Mushi

Kuna tofauti kati ya terminologies hizi mbili.

1. Rebellion
2. Revolts

Rebellion ni kukataa kufuata sheria za nchi huku revolts ni kutaka kufanya mapinduzi. Usipoweza kutofautofautisha vitu hivi viwili utajikuta matatizoni.

Jana kilichotaka kufanyika ni Rebellion bila kujua lakini akilini kwa wanaotaka kufanya hivyo walifikiri ni kufanya revolts.

 Kwa sheria za Tanzania si rahisi kama mnavyofikiria kufikia level za revolts mtaishia kufanya rebellion na mtaishia kufungwa. Hivyo kabla ya kufikiria kufanya mapinduzi angalia sheria za nchi, angalia nani anaongoza mapinduzi hayo, sababu za kuyafanya, Mtizamo wa jamii, uimara wa vyombo vya ulinzi na usalama.

KWA SERIKALI

Crane Brinton ni katika nadharia yake ya mapinduzi aliyoiandika kwenye kitabu chake cha " Anatomy of revolution" anafananisha mapinduzi na homa. Katika mazingira hayo Brinton anasema homa si jambo la kufurahia na linapaswa kuepukika au kutibiwa kwa mapema pindi dalili za homa hiyo zinapojitokeza.

Kwa maana hiyo tuingie maabara tuchunguze kama hii ni dalili ya homa kweli au lah. Majibu hayo tuyatuimie kutibu homa hiyo ili isijitokeze tena siku za usoni. Kutibu homa hiyo ni kurekebisha yote ambayo vijana walikuwa wanahubiriwa ili waandamane. Wanadai wana madai yao ambayo yalikuwa yakiwasukuma kufanya walichotaka kukifanya. Hebu tusome petition na permit Yao tuyajue waliyokuwa wanayataka. Serikali yetu ni Sikivu sana nadhani apamoja na udogo wa kundi hili mnaweza kuangalia nini wanakililia kama kina mantiki mkishughulikie ili Tanzania iendelee kuwa mahali salama na kisiwa cha amani.

Kuna wanaotaka kubeza jaribio hili ila ni jambo ambalo litavifanya vyombo vyetu vya kiutawala kila kimoja kwa nafasi yake kufanya tathimini ya jaribio hili. Hii ni mbegu imeoteshwa itategemea tutaifukua ardhini na kuitupa au TUTAINYESHELEA MAJI ili ichipue.

TUSIDHARAU CHOCHOTE KINACHOJITOKEZA MBELE YETU LAZMA KISHUGHULIKIWE KWA UKAMILIFU WAKE.

Ole Mushi.
0712702602