Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei, 2017

Mbunge wa CCM Ashangiliwa na Upinzani Bungeni Baada ya Kuhoji Zilipo Milioni 50 Kila Kijiji...!!!

Picha
Katika hali ya kushangaza mbunge wa CCM ameshangiliwa na upinzani bungeni mara baada ya kuhoji zilipo Milioni 50 ambazo katika Ilani ya Chana cha mapinduzi zilitajwa kugaiwa kwa kila kijiji nchi Tanzania... Alipongezwa na wabunge ambao wengi wao ni kutoka upinzani Nini maoni yako katika hili?

Kuna Ufisadi Kwenye T. Shirt Zilizotumika Wakati wa Baraza Kuu la CHADEMA Lililofanyika Dodoma..!!!!

Picha
Nimepata habari kuwa kuna ufisadi mkubwa umefanyika ndani ya CHADEMA kwa kutumia fedha za ruzuku. Kwamba, T. Shirt moja iliyovaliwa wakati wa Kamati Kuu na Baraza Kuu la CHADEMA lililofanyika Doeoma hivi karibuni imetengenezwa kwa shilingi 120,000 na kwamba kila aliyevaa ametakiwa kulipa nusu ya bei na nusu nyingine kimegharamia chama. Taarifa hizo zinasema kuwa baadhi ya wajumbe wamegoma kulipa gharama hizo kwa madai kuwa bei ni kubwa mnooooo! Inadaiwa pia kuwa wajumbe wengine waligoma kuzivaa ili wasiwe sehemu ya ufisadi huo. Kama habari hizi ni za kweli basi kale kaugonjwa kalikokimbia CCM kametaga mayai CHADEMA Chanzo JF

Tetesi..CCM Kuwafukuza Nape Nnauye na Bashe kwa Kuwa Wanatumika na Chadema..!!!

Picha
Taarifa kutoka chanzo cha ndani kabisa ndani ya CCM zinasema kwamba kuna uwezekano mkubwa katika Kikao kijacho cha CCM takribani Wanachama 11 wakafutiwa Uanachama ambapo ndani yao wapo Vigogo Watatu ambao ni Nape Nauye, Hussein Bashe na Msukuma. Nape na Bashe wanafukuzwa baada ya kugundulika kuwa wanatumika na Chama cha Upinzani CHADEMA huku Msukuma anafukuzwa kwa kosa la kuwa mropokaji, mweneza chuki na mtu asiye mkweli kwa Wanachama wenzie. Chanz JF

Utata Waibuka Kuhusu Maziko ya Mzee Ngosha Aliyebuni Nembo ya Taifa..!!!

Picha
“HATUNA jibu mzee huyu atazikwa lini na wapi, lakini mwili wake bado tumeuhifadhi hapa na Serikali inaendelea kuwatafuta ndugu zake halisi ili kujua taratibu za mazishi,” amesema Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH). Mkurugenzi huyo wa Hospitali ya Muhimbili, Profesa Lawrence Mseru alisema hayo jana alipozungumza na HabariLeo na kusisitiza kuwa, mwili wa Mzee Francis Kanyasu maarufu kama Ngosha (86) aliyefahamika hivi karibuni kuwa ndiye aliyebuni Nembo ya Taifa, kwa sasa umehifadhiwa katika Hospitali hiyo hadi watakapopatikana ndugu zake halisi tayari kwa mazishi. Katika mazungumzo hayo, Profesa Mseru alisema ndugu wa marehemu Ngosha wanatafutwa na serikali kwa kushirikiana na jamaa waliokuwa wakiishi na mzee huyo Buguruni Dar es Salaam. Alisema kwa mujibu wa taarifa alizozitoa Ngosha katika uhai wake, baadhi ya ndugu zake wanaishi Sengerema, hivyo watatafutwa ili watoe kauli kuhusu mazishi ya ndugu yao. “Wale walioishi na Mzee Ngosha ni jamaa tu wa...

IGP Sirro Atangaza Vita Pwani..Adai Ubaya Wataulipa kwa Ubaya..!!!

Picha
IGP Simon Sirro amewaonya wahalifu wanaojishughulisha na mauaji mkoani Pwani kuacha mara moja kwani ndani ya muda mfupi ataenda kuwafichua kwa kutumia vyombo vyake vya dola ili kulinda amani ambayo imepotezwa na kikundi cha watu wachache. IGP Siro ametoa onyo hilo wakati akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es salaam na kusema kuwa haki lazima iende kutoa majibu ya watu wanaofanya mauaji maeneo ya  kibiti, mkuranga, Ikwiriri kwa ndani ya muda mfupi huku akiongeza hakuna sababu ya watu wema kufanyiwa ubaya na kama jeshi ni wajibu kuilinda amani. "Hakuna haja ya watu kufanya ukatili na ubaya kwa watu wasiostahili. Sisi tutawajibu ubaya wanaofanya ubaya. Watanzania pamoja na vuiongozi wangu wanataka maji ya nani anayefanya haya mauaji, lakini tayari tumeshapata kujua ni kikundi cha watu wachache niwahakikishie mimi pamoja na vyombo vya dola tutawapatia majibu ndani ya muda mfupi"- IGP Sirro aliwaambia wanahabari. Pamoja na hayo katika mkutano huo na wanahabari IGP Sirro ...

HABARI ZA WANGONI NA VITA VYA KWANZA VYA DUNIA

Picha
SEHEMU YA KWANZA Tunapozungumzia vita vya kwanza vya dunia tunazungumzia vita vya mataifa makubwa yaliokuwa yakipigana kuanzia miaka ya 1914-1918. Vita hivi vilianzia huko Barani Ulaya, lakini baadae vita hivyo viliweza kufika hadi Afrika. Kwani nchi zilizokuwa zikipigana kwenye vita hivyo, zilikuwa na makoloni yake barani Afrika. Hivyo kwa namna Fulani bara la Afrika liliathiriwa na vita hivyo. Ukweli ni kwamba takribani bara zima la Afrika lilihusika kwenye vita hivi vya dunia. Lakini kwa leo tuangalia kwa undani habari na historia ya vita vya dunia kwa upande wa kabila la Wangoni.  Kwani wakati vita hivi vinatokea miaka iliyotajwa hapo juu,  Tanganyika ilikuwa chini ya Wajerumani walioanza kutawala miaka ya 1890-1920. Hivyo basi kwa kuwa kwenye vita hii Wajerumani walihusika, basi kuna baadhi ya makabila ya Tanganyika yalihusika pia. Kama inavyofahamika kuwa Wangoni walitokea Afrika kusini mwanzoni mwa miaka ya 1830. Na walipotoka huko waliweza kusambaa maeneo ya A...

UKUMBUSHO:Mmehalalishiwa usiku wa swaumu kuingiliana na wake zenu

Picha
Mmehalalishiwa usiku wa swaumu kuingiliana na wake zenu. Wao ni vazi kwenu na nyinyi ni vazi kwao. Mwenyezi mungu anajua kwamba mlikuwa mkizikhini nafsi zenu. Kwa hivyo amekukubalieni toba yenu na amekusameheni. Basi sasa changanyikeni nao na takeni aliyo kuandikieni mwenyezi mungu. Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni saumu mpaka usiku. Wala msichanganyike nao, na halim nakaa Itikafu msikitini .Hiyo ni mipaka ya mwenyezi mungu, basi msikaribie. Namna hivi mwenyezi mungu anabainisha ishara zake kwa watu ili wapate kumcha. Qur'an  (suratul baqarah 2:187 )

Alichosema Rais Magufuli baada ya kupokea taarifa za kifo cha Ndesamburo

“Kwa masikitiko nimepokea taarifa za kifo cha Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Moshi Mjini, Mzee wangu Philemon Ndesamburo kilichotokea leo tarehe 31 Mei, 2017 katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC iliyopo Moshi Mkoani Kilimanjaro, Namkumbuka Mzee Ndesamburo kwa hekima zake na uongozi wake uliozingatia siasa za kistaarabu” Hii ni kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa katika salamu zake za rambirambi kwa familia ya Marehemu Philemon Ndesamburo, Viongozi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA ) pamoja na ndugu, jamaa na marafiki wote walioguswa na kifo hicho. Mhe. Rais Magufuli amesema alifanya kazi na Marehemu Philemon Ndesamburo wakati wote wakiwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wakati wote walishirikiana, kutaniana na anamkumbuka kwa namna ambavyo alitumia muda wake bungeni kupigania mambo yenye maslai kwa wananchi wa jimbo lake la Moshi Mjini. Mhe. Dkt. Magufuli ameitaka familia ya Mar...

Kauli ya IGP Simon Sirro kuhusu mauaji Mkoani Pwani

Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro leo amezungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ikiwa ni mkutano wake wa kwanza na vyombo vya habari tangu alipoteuliwa na kuapishwa kushika wadhifa huo. IGP Sirro amezungumzia mambo mengi lakini akijita zaidi katika masuala ya ulinzi na usalama wa raia, hasa mkoa wa Pwani ambapo mauaji ya raia yamekuwa yakitekelezwa na watu wasiojulikana. Sirro amesema kuwa nchi kwa sasa iko shwari kwa sababu hakuna matukio makubwa yaliyoripotiwa isipokuwa katika Wilaya za Rufiji, Mkuranga na Kibiti mkoani Pwani ambapo matukio kadha wa kadha ya mauaji yamekuwa yakitokea. Akizungumzia mauaji hayo yanayodaiwa ndiyo kilikuwa chanzo kikubwa cha Ernest Mangu kuondolewa madarakani, alisema kuwa hakuna kikundi chochote cha watu kilichopo juu ya sheria, na kuwa, mtu yeyote akitenda kosa ajue adhabu itamfuata. Sirro amesisistiza kuwa suala la uhalifu mkoani Pwani ni la muda mfupi na kwamba, yeye na timu yake watalipatia majibu hivi karibuni. Aidha, Sir...

Taarifa ya Bunge kuhusu kifo cha Mbunge Mstaafu, Philemon Ndesamburo

Picha

Edo Kumwembe ' Simba inahitaji wanaume watatu wa nguvu'

Picha
Edo Kumwembe afunguka haya: Makala ambayo msemaji wa Simba kasema ni mbovu...shabiki wa Simba uisome hapa na utafakari akili za msemaji wako  . JICHO LA MWEWE: Simba inahitaji wanaume watatu wa nguvu By EDO KUMWEMBE TUKUTANE uwanja wa ndege. Simba itakuwa inasafiri labda kwenda Rwanda, Yanga itakuwa inasafiri kwenda Misri. Kule kwa Yanga kiasi wametimia, huku kwa Simba kunahitajika wanaume watatu wengine kabla ya kupanda ndege kwenda hiyo safari yao. Simba inahitaji kuingia sokoni kwa umakini na kununua wachezaji watatu wa kigeni wa maana ambao, kwa hapa nchini sijawaona mpaka sasa. Mgongo wa timu ni mlinzi wa kati kiongozi mwenye uzoefu. Kisha kiungo mahiri mwenye nguvu na uzoefu, halafu mshambuliaji wa nguvu anayeweza kufunga mabao 20 ya msimu. Kwa kuanzia katika ushambuliaji Simba wamekwenda kwa John Bocco. Siyo mbaya. Kwa kulinganisha washambuliaji ambao wanao sasa hivi, Bocco ni bora zaidi. Bocco aliye fiti bila ya majeraha ni bora kuliko Laudit Mavugo au shujaa wa ju...

Mbunge - Dunia Nzima Itamwiga Rais Magufuli..Hadi Trump Ipo Siku Atamwiga Tu..!!!

Picha
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CCM), Peter Serukamba amefunguka na kusema jambo alilofanya Rais Magufuli kuzuia mchanga litakwenda kuigwa duniani kote na kuleta mapinduzi katika "Extractive Industries" (sekta za uchimbaji madini) Serukamba alisema hayo jana bungeni na kusema ukiona mpinzani wako anakupinga katika jambo lolote lile basi ujue umefanya jambo ambalo ni sahihi ila ukiona mpinzani wako anakusifu ujue umefanya jambo baya, hivyo kwa kuwa wapinzani wanalalamika basi Rais amepatia katika maamuzi yake, na anatakiwa kupewa ushirikiano wa wananchi na wabunge. "Mimi kama mwanasiasa ukiona mtu ambaye ni adui yako umefanya jambo akakusifia ujue lipo tatizo, ila ukiona umefanya jambo adui yako akasema umekosea maana yake umepatia sana. Mimi naomba nimpongeze Rais Magufuli kwa kazi kubwa aliyofanya na niwaambie waheshimiwa wabunge, duniani kote 'Extractive Industries' inaenda kubadilika atakaye kuwa kwenye historia ya kubadilisha Extractive Industries ni Rais Magu...

Lema Amtabiria Mwigulu Kusimamishwa Uwaziri Muda Wowote Kuanzia Sasa

Picha
Mbunge Godbless Lema kupitia account yake ya Twitter Amtabiria Mwigulu Kusimamishwa Uwaziri Muda Wowote Kuanzia Sasa ikiwa ni siku chache zimepita baada ya Prof Muhongo Kutumbuliwa.... . Mdau Una maoni gani?

Kwa Mara ya Kwanza Nchi  Imekuwa na ma-IGP Wawili..!!!

Picha
Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu tumekuwa na maIGP wawili. Mmoja amepewa madaraka ya kuwa mkuu wa jeshi la polisi na mwingine amevuliwa madaraka hayo lakini amebaki na cheo chake. Wengi hawajui kuwa IGP ni cheo na sawa na vyeo vingine kama Inspekta wa polisi au Mrakibu wa polisi au Koplo. Tofauti ni kwamba vyeo vya chini vinaweza kushikwa na watu wengi lakini cheo cha juu kabisa ambacho ni IGP hushikwa na mtu mmoja tu. Yani makoplo wanaweza kuwa wengi, makamishna wengi, mainspekta wengi lakini IGP mmoja. Huyo IGP mmoja ndo hupewa madaraka ya kuongoza jeshi la polisi. Kumbuka kuna tofauti kati ya CHEO na MADARAKA. Mtu mwenye cheo cha IGP ndio hupewa madaraka ya kuongoza jeshi la polisi. Sasa kwa mara ya kwanza tumekua na watu wawili wenye cheo kimoja cha IGP. Tofauti ni kwamba mmoja ameondolewa madaraka ya kuongoza jeshi la polisi, na mwingine kapewa madaraka hayo. Huyu aliyeondolewa madaraka, ameambiwa atapangiwa kazi nyingine. Lakini bado amebaki na cheo chake cha ...

Duh..Hivi Ndivyo Magari ya Kifahari Yalivyotawala Msiba wa Ivan..Matajiri Waliokuja Nayo Wamwaga Pesa za 'Sadaka Lawe' kwa Masikini..!!!

Picha
 Magari ya kifahari yameonekana jana katika mazishi ya bilionea Ivan Ssemwanga yaliyofanyika nyumbani kwao Kayunga jijini Kampala. Ivan aliyekuwa mume wa Zari Hassan maarufu ‘Zarithebosslady’ ambaye kwa sasa ni mpenzi wa Diamond Platnumz, alifariki dunia wiki iliyopita baada ya kupata kiharusi na kuwa katika hali ya koma kwa wiki mbili mfululizo katika hospitali ya Steven Biko huko Pretoria nchini Afrika Kusini. Gazeti la Uganda, Daily monitor linaripoti kuwa miongoni mwa magari hayo ni pamoja na yale ya marehemu likiwemo Hammer lenye jina la Ivan 9, yale ya vizito mbalimbali wa jiji la Kampala waliohudhuria mazishi hayo pamoja na gari la tajiri wa Tanzania Jack Pemba aina ya Audi lenye jina la A Pemba ambalo lilionekana kuwa la kifahari zaidi. Katika hali ambayo haikuonekana kuwa ya kushangaza, baadhi ya waombolezaji walionekana wakiomba na kupewa fedha kutoka kwa matajiri mbalimbali waliohudhuria. Hata hivyo kaburi la Ivan liliwekwa mafungu ya fedha chini ikiwa n...

Wakati Joto la Mchanga wa Madini Likiendelea Kuvuma..Zitto Kabwe Akoleza Moto kwa Kusema Haya..!!!

Picha
MBUNGE wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, amesema Tanzania inapaswa kuhakikisha sheria na sera za madini zinalazimisha rasilimali madini kuwa mali ya Watanzania ndipo nchini itanufaika. Aidha, amesema ni wakati muafaka kwa Taifa kujitoa katika mfumo wa kodi za Kimataifa akiuelezea kuwa umeonesha kunyonya nchi maskini zaidi na kunufaisha zile  tajiri. Zitto alisema hayo jana wakati akizungumza kwenye kipindi cha Mizani ya Wiki kinachorushwa na televisheni ya Azam Dar es Salaam. Alisema kwa kuwa Rais John Magufuli ameamua kupigania vita hiyo ni jukumu la kila Mtanzania kupigana hadi kuhakikisha kuwa madini yanakuwa ni mali ya wananchi wa Kitanzania. Zitto alisema kwa mujibu wa sheria iliyopo inaanisha kuwa baada ya mwekezaji kuingia mkataba na Serikali madini ni mali yake jambo ambalo halikubaliki. “Hii vita ni vita ngumu ila kwa sababu Rais ameamua kuipigana pamoja na ukweli kuwa anajua jitihada za Serikali iliyopita tunapaswa kumuunga mkono ili tuweze kunufaika. “Mimi...

Huyu Ndiye Bilionea Dangote ..Apanga Kununua Kiwanda Hiki Kikubwa cha Kutengeneza Magari Afrika..!!!

Picha
Mfanyabiashara tajiri Afrika, Aliko Dangote anasubiri idhini ya Benki Kuu ya Nigeria ili anunue kiwanda cha kuunda magari aina ya Peugeot akishirikiana na majimbo mawili. Kampuni ya Usimamizi wa Mali ya Nigeria (AMCON), iliyoundwa wakati wa kuyumba kwa benki, inakaribia kuuza Kiwanda cha Magari cha Peugeot cha Nigeria (PAN). “Tumeshakamilisha mchakato wote wa zabuni miezi miwili iliyopita na sasa tunasubiri idhini ya Benki Kuu,” alisema ofisa mtendaji mkuu wa AMCON, Ahmed Kuru alipoongea na Reuters. PAN, kiwanda cha kuunda magari kilichopo jimbo la Kaduna, kina ubia wa kiufundi na PSA Peugeot Citroen na kikiwa na uwezo wa kuunganisha magari 90,000 kwa mwaka. Dangote, kwa kushirikiana na majimbo ya Kaduna na Kebbi na Benki ya Viwanda (BOI) waliomba zabuni ya kuwa wamiliki wakubwa wa hisa za PAN mwaka jana kutokana na AMCON kutaka kuuza baadhi ya mali zake ilizozichukua wakati wa matatizo ya taasisi za kifedha.

Nane Waidhinishwa Kuwania Urais Kenya...!!!!

Picha
Tume ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya, IEBC, imeidhinisha majina ya wagombea nane kuwania Urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti mwaka huu Kati ya wagombea hao, ushindani mkubwa unatarajiwa kuwa kati ya Rais Uhuru Kenyatta anayewania muhula wa pili na mgombea wa muungano wa vyama vya upinzani NASA Raila Odinga. Hata hivyo, zoezi la mchujo liliwaacha wengine zaidi ya 10 nje ya kinya'nga'nyiro hicho akiwemo Peter Solomon Gichira aliyefikishwa Mahakamani kwa madai ya kutaka kujiua baada ya kuondolewa katika orodha hiyo kwa kutokidhi vigezo. Ushindani unaotarajiwa kati ya Rais Kenyatta na Bw. Odinga, unarejesha nchi hiyo katika historia ya siasa kati ya baba zao, Jomo Kenyatta aliyekuwa Rais wa kwanza na Jaramogi Oginga Odinga aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais baada ya Uhuru mwaka 1963. Wagombea wengine sita ambao wanawania Urais ni pamoja na Cyrus Jirongo (UDP), Ekuru Aukot kutoka chama cha Thirdway Alliance, Abduba Dida (ARC). Wagombea binafsi ni pamoja na Josep...

Dola ya Marekani Yatikisika Katika Soko la Dunia..Trump Adaiwa Kuwa ni Chanzo..!!

Picha
WATUNGA sera kutoka Benki Kuu ya Marekani, wamesema wanafuatilia kilichoko katika uchumi wa taifa, kutokana na kuongezeka kiwango cha riba za benki nchini humo na imefanya thamani ya fedha za dola kushuka. Mchumi wa nchi hiyo, Gus Faucher, anasema ni hali ya kushangaa kuonekana Dola za Marekani, inashuka thamani hivi sasa. "Nadhani takwimu tulizopata kutoka mkutanoni inaonyesha vigezo," anasema Faucher, huku wachumi wakieleza shaka yao dhidi ya hali halisi ya sera za Rais mpya, Donald Trump. Inaelezwa kwamba katika kipindi kifupi kilichopita, tangu Machi mwaka huu, serikali iliongeza kiwango cha riba zake mara tatu. Pia, katika sura nyingine, inaelezwa kuwa benki zimeendelea kuwa imara katika majukumu yake ya kila siku. Kwa miaka mingi na katika sehemu nyingi, Dola ya Marekani imekuwa marejeo cha kiwango cha mabadilishano katika fedha za dunia. Pia, kuna fedha kama za Euro ambazo ni za Jumuiya ya Ulaya (EU) na Pauni za Uingereza, nazo zimeshika nafasi hiyo .

Wenger Alamba Mkataba Mpya Arsenal..Apewa Miaka Miwili ya Matumaini..!!!!

Picha
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amekubalia kusaini mkataba wa miaka mwili wa kuendelea kuifundisha klabu hiyo kuendeleza utawala wake wa miaka 21 ndani ya Emirates. Wenger na mmiliki wa klabu hiyo Stan Kroenke walikutana Jumatatu kuzungumzia hatma yake na uamuzi huo ukacheleweshwa kutolewa na bodi leo Jumanne. Arsenal imepanga kesho kumtangaza rasmini Mfaransa huyo kuendelea na jukumu lake. Arsenal 'The Gunners' imemaliza katika nafasi ya tano msimu huu wa Ligi Kuu ikiwa ni mara ya kwanza tangu Wenger alipochukua jukumu la kuifundisha timu hiyo mwaka 1996. Imemaliza ikiwa nyuma kwa pointi 18, kwa mabingwa Chelsea,  lakini ilifanikiwa kuifunga Blues mabao 2-1 katika fainali ya Kombe la FA iliyofanyika Wembley Jumamosi iliyopita. Mkataba wa Wenger uliokuwa unamalizika mwisho wa msimu huu. Wenger ameiongoza Gunners kutwaa mataji matatu ya Ligi Kuu England na makombe manne ya FA katika misimu yake tisa ya kwanza. Msimu wa 2003-04, alikuwa kocha wa kwanza tangu 1888-89, kuio...

Picha: Mume wa Zari alivyofukiwa na fedha kwenye kaburi lake

Picha
Jana jioni mwili wa mfanyabiashara maarufu na mume wa Zarinah Hassan (Zari The Boss Lady) ulizikwa nchini Uganda baada ya kufariki wiki iliyopita nchini Afrika Kusini alipokuwa akiishi. Watu mbalimbali walihudhuria mazishi hayo kutokana na Ivan Semwanga kuwa alikuwa ni mtu tajiri na aliyefahamika na wengi. Katika maziko hayo, kilichowashangaza wengi ni jinsi matajiri wenzake walivyoamua kumuenzi mwenzao huyo kwa kumwaga fedha ndani ya kaburi hilo kabla jeneza halijawekwa. Kitendo hicho kiliwashangaza wengi kwa sababu si utamaduni wa kiafrika kwani itaonekana kana kwamba mnasherehekea kifo chake jambo ambalo ni mwiko. Mbali na tukio hilo, watoto wa marehemu, Ivan Semwanga walionyesha masikitio yao baada ya kuondokewa na baba yao, ambapo walisema kuwa maisha kwao hayawezi kuwa sawa tena sababu ya pengo hilo. “Dad, so many thoughts come to our mind whenever we speak of your name; it seems without you in our lives things will never be the same. We think of the good old days when...

Kapombe kuhusu Bocco kuondoka Azam na tetesi za kurudi Simba

Kumekuwa na mitazamo tofauti kuhusu kuondoka kwa nahodha na mchezaji wa muda mrefu wa Azam FC John Bocco ‘Adebayor’ ndani ya kikosi hicho chenye maskani yake Chamazi, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Shomari Kapombe ni mchezaji mwenzake Bocco waliyepata kucheza pamoja kwa muda mrefu kwenye kikosi cha Azam na timu ya taifa, Kapombe amesema kuondoka kwa Bocco ndani ya Azam ni kitu cha kaiwaida kwenye maisha ya soka. Kuondoka kwa Bocco ndani ya Azam ni kita cha kawaida kwenye maisha ya soka, tumeona hata Ulaya wachezaji wenye heshima kama Bocco wameondoka kwenye vilabu vyao na maisha yameendelea. “Bocco alikuwa bado ni mchezaji muhimu ndani ya Azam kutokana na uwezo wake lakini ameshaondoka anaenda sehemu nyingine kuangalia maisha yake kwa hiyo hilo limeshapita tuache maisha mengine yaendelee.” Kapombe amezungumzia pia kuhusu tetesi ambazo zinamhusisha yeye kurudi kwenye klabu yake ya zamani Simba kwa ajili ya kuitumikia kuanzia msimu ujao. “Nikitoka ...

Habari zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya May 31

Picha

Faida 4 za Kufunga Mwezi Huu Mtukufu wa Ramadhan..!!!

Picha
Kwa mujibu wa dini ya kiislam tunakumbushwa kuwa kila muislam mzima na mwenye afya njema anatakiwa kushiriki katika swaumu ambayo ni ibada ya kufunga chakula na kinywaji mcahana na kutwa sambamba na kujizuia kushiriki toka alfajiri hadi magharibi. Pamoja na hayo, matendo hayo yatoba hupaswa kuendana na kuswali sana pamoja na kusoma quran kwa wingi. Katika mwezi huu wa Ramadhani kadhalika inatakiwa kwa muislam kuwa mengi ya maneno yake yawe katika kumtaja Allah (Subhaanahu wa Ta’ala), kwani ni jambo ambalo linasaidia katika kuusafisha moyo  wake na kuiboresha funga yake. Mbali na hayo zipo pia faida nyingine za kufunga kama zifuatazo 1. Ni kutekeleza mojawapo ya amri za Mwenyezi Mungu alizotuteremshia na faida ya utekelezaji huu ni kuingia peponi siku ya mwisho. 2. Faida ya pili ya mfungaji wa swaumu ni kujizoesha kuwa na subira, yaani katika mwezi Mtukufu wa Ramadhan, mtu anajifunza jinsi ya kuwa mvumilivu na kustahamili njaa, kiu na matamanio ya kimwili. 3. Faida nyin...

Mchanga wa Madini Walivuruga Bunge....... Tundu Lissu na Godbless Lema Wanapinga Kitendo cha Serikali Kuuzuia

Picha
Mchanga  wa dhahabu uliozuiwa katika makontena Bandari ya Dar es Salaam, umezua mjadala bungeni baada ya wabunge wa CCM na Chadema kupingana juu ya uamuzi wa Rais Dk. John Magufuli kuyazuia kusafirishwa nje ya nchi. Hayo yalitokea jana wabunge walipokuwa wakichangia hotuba ya mapato na matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje, Kikanda na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa mwaka wa fedha 2017/18, iliyowasilishwa na Waziri Balozi Augustine Mahiga. Wakichangia bajeti hiyo, wabunge wawili wa Chadema, Tundu Lissu (Singida Mashariki) na Godbless Lema (Arusha Mjini), walisema uamuzi wa Rais Magufuli utalisababishia taifa hasara na kuwafukuza wawekezaji wa nje. Naye Lema alisema amepata taarifa kwamba wamiliki wa mgodi wa Acacia ambao makontena yao yamezuiwa, wamefungua kesi katika Mahakama ya London, Uingereza, kulalamikia uamuzi huo wa Serikali. “Katika hatua ya kulinda rasilimali ya nchi, ni mwendawazimu anayeweza asipongeze, lakini lazima tujue ni namna gani unalinda rasilimali h...

Ivan Kuzikwa leo, Zari aahidi Kuwaangalia Watoto

Picha
Baada ya Jumatatu hii mwili wa Ivan Ssemwanga kuagwa na kufanyiwa ibada takatifu, aliyekuwa mke wa zamani wa marehemu, Zari Hassan alipata fursa ya kuzungumza kwa mara ya kwanza. Katika misa ya mazishi iliyofanyika kwenye kanisa la Namirembe mijini Kampala, Uganda Jumatatu hii, Zari alionekana akiwa ametulia na akizungumza na wanae. Alipoitwa kuzungumza madhabahuni, watu waliohudhuria walijianda kumsikiliza atakachosema. “Sitomhuzunikia Ivan,” alisema. “Nitasherehekea maisha yake. Muda mrefu, tulitengana kwasababu ya tofauti ambazo sote tulizijua. Nilisonga mbele na maisha yangu, lakini si Ivan. Ivan alijua kile nilichoweza kufanya. Alijua kile nilichoweza kufanya na kile nisichoweza. Alijua kuwa ningewaangalia vijana vyema na aliniamini. Kwa hali hiyo, naahidi ntawaangalia vijana hadi nitakapoungana naye.” Ivan anatarajiwa kuzikwa leo ambapo Diamond aliyezaa na Zari watoto wawili naye aliahidi atahudhuria.

Simba na Yanga Wahamishia Bifu lao Kimataifa

Picha
BAADA ya kushuhudia upinzani mkali kwenye kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na Kombe la FA, ushindani na upinzani wa Simba na Yanga sasa umehamia kwenye michuano ya kimataifa. Hatua hiyo inakuja baada ya Yanga kufanikiwa kukata tiketi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, huku Simba ikikata tiketi ya kushiriki Kombe Shirikisho barani Afrika. Kocha msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja, aliliambia Nipashe jana kuwa kukata tiketi ya kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika haitoshi na badala yake wanataka kuhakikisha wanafanya vizuri zaidi. "Lazima Simba ionyeshe utofauti... tunataka kurejea kwa kishindo kwenye michuano ya kimataifa kwa kuhakikisha tunafika mbali," alisema Mayanja ambaye juzi alikuwa pamoja na kikosi cha timu hiyo Bungeni mjini Dodoma. Aidha, Meneja wa Yanga, Hafidh Salehe akizungumza na Nipashe juzi, alisema ushiriki wa Simba na Yanga utaleta ushindani mkubwa kwao kwenye michuano ya kimataifa. Alisema kila timu itataka kuizidi nyingin...

Prof. Muhongo Awaondoa Hofu Wapiga Kura Wake Baada ya Kufutwa Kazi

Picha
MARA: Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini na Mbunge wa Musoma Vijiji Prof. Sospeter Muhongo amewasihi wakazi wa jimbo hilo kutokuingiwa na hofu kufuatia uamuzi wa Rais Dkt Magufuli kumfuta kazi. Prof. Muhongo amewataka wapigakura wake na rafiki zake kutokuwa na hofu kwani kwa pamoja watafanikiwa. Kwa mujibu wa taarifa za ofisi yake, amewaahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha kuwa wanafikia malengo yao ya kimaendeleo kwa kutimiza ahadi zake. Taarifa hiyo ilitolewa na Katibu wa Mbunge huyo, Juma Ramadhan ambaye alisema kuwa kilichotokea ni cha kawaida kwenye siasa na inawapasa kusahau hayo ili waweze kusonga mbele katika kutekeleza miradi ya maendeleo. Kwa sasa tunajielekeza kujenga vyumba vya madarasa na miradi mingine ya maendeleo, hivyo ni vyema tukaungana pamoja ili kuweza kutekeleza majukumu haya, alisema msaidizi huo. Wakazi wa jimbo hilo waliahidi kutoa ushirikiano kwa mbunge wao katika kutekeleza miradi hiyo kwani yeye si kiongozi wa kwanza kuondolewa kwenye wadh...

Jambazi Mwingine wa Kike Kenya Atunguliwa Risasi na Kuuwawa...Alikuwa Rafiki wa Yule Alieuwawa Mwanzo

Picha
Police on Sunday gunned down two suspected gangsters believed to be members of the same gang as slain gangster, Claire Njoki Mwaniki, famously known as “Clea Adi Vybz.” One of the suspects, known by her alias- “Marsha Minaj”, is said to have been the best friend of the late Claire Njoki. Marsha Minaj (left) with her friend Clea Adi Vybz “Minaj” was shot dead together with a male suspect believed to be her boyfriend on Sunday afternoon at a house in Migingo, in Patanisho area. The suspects were gunned down following a tip-off from members of the public on the whereabouts of the wanted criminals. Confirming the shooting, Nairobi County Police Commander Japheth Koome said when the police went to the house they were in, they found the two and attempted to arrest them but they engaged them in a shoot out. “The officers were forced to return fire and they managed to fatally injure the two and recovered a pistol, five rounds of ammunition and t...