Kwa nini Mtume rehma na amani ziwe Juu Yake alitembea kutumia vidole vyake vya mbele kwenye mazishi ya Tha'alabah; Soma kisa:
Tha'alabah likuwa mtumishi wa mtume rehma na amani ziwe Juu Yake, siku moja Mtume alimtuma sehemu, akapita ktk uwa wa mtu miongoni mwa maansari, akamuona mwanamke anaoga, akasimama kumuangalia na kumkazia macho.; Ghafla akashtuka na kutambua kuwa amefanya kosa ,na Allaah amemuona, akajua kuwa ni lazima habari ile itamfikia Mtume kupitia wahyi Tha'alabah hakurudi tena kwa mtume bali alikwenda kujificha kwenye pango liliopo baina ya Makka na Madina kwa siku 40, Jibril Alaihi Salaam akatumwa na Allaah kwa Mtume na kumwambia; Ewe mjumbe wa Allaah, Allaah anakusalimu na anakwambia ya kuwa kuna mja wako amejifjcha pangoni na ananiomba ulinzi, Mtume akamwambia Omar bin Al khatwab na Salman Al faarisiy nendeni mkamlete Tha'alabah . Walimpomleta, Mtume akamuuliza Tha'alabah kipi kilichokufanya ughibu? akasema ; kwa sababu ya Dhambi zangu ewe mjumbe wa Allaah. Mtume akamwambia je nikufahamishe aya itakayofuta madhambi yako?Tha'alabah akasema nifundishe ewe mjumbe wa Allaah, Mtume akamwambia sema; "EWE MOLA WETU TUPE HAPA DUNIANI MEMA NA AKHERA MEMA NA UTUEPUSHE NA ADHABU YA MOTO" Tha'alabah akasema Bali dhambi zangu ni kubwa zaidi. Mtume akamwambia bali maneno ya Allaah ni makubwa zaidi, kisha mtume akamuarisha aende nyumbani kwake akaendelee na maisha Yake, lakini Tha'alabah akajifungia tena kwa muda siku 8, Mtume akawaambia baadhi ya maswahaba zake, twendeni tukamtembelee Tha'alabah , wakamkuta mgonjwa, Mtume akachukua kichwa cha Tha'alabah na kukipakata, lakini Tha'alabah akaondosha kichwa chake kwenye miguu ya Mtume, Mtume akamuuliza, kwa nini umeondosha kichwa chako kwenye mapaja yangu? Tha'alabah akasema kimejaa madhambi ewe mjumbe wa Allaah, Mtume akamuuliza, unahisi nini? Tha'alabah akasema nahisi maumivu mwili nzima, Mtume akamuuliza tena, unatamani nini? Tha'alabah akasema, natamani kupata msamaha wa Allaah. Jibril Alaihi Salaam akashuka na kumwambia Mtume; Allaah anakusalimia na anasema; Lau mja huyu angekutana na mimi na madhambi hadi mbinguni, angekutana na msamaha wangu mfano wa madhambi yake. Mtume akamfahamisha Tha'alabah ujumbe huo, na Tha'alabah akapiga kelele za furaha na kufariki hapo hapo. Mtume akaamrisha aoshwe na akafiniwe na wakati wa mazishi yake Mtume alionekana akitembea kwa kunyata kwa kutumia vidole vyake vya mbele, baada ya mazishi, maswahaba wakamuuliza Mtume sababu za kutembelea ncha za vidole vyake wakati wa mazishi, Mtume rehma na amani ziwe Juu Yake akasema; NA APA KWA YULE AMBAE AMENITUMA, SIKUWEZA KUPATA NAFASI YA KUWEKA UNYAYO WANGU KWA JINSI AMBAVYO MALAIKA WALIVYOKUWA WENGI WALIOKUJA KUMZIKA THA'ALABAH .
Ndugu yangu muislamu, umejifunza nini ktk kisa hiki adhimu, na je, kinagusa maisha yako? Changia sambaza .
