Mwigulu Nchemba kaufuata ubingwa Simba?

Hakuna asiyejua kwamba Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Mh. Mwigulu Nchemba ni shabiki wa Yanga ‘lialia.’

Kamera yatu ilifanikiwa kumnasa Nchemba akiwa anaitinga jezi ya ‘mnyama’ Simba kwenye uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Mh. Nchemba anafahamika kuwa ni mpenzi wa Yanga na mara kadhaa ameonekana akiwa katika uzi wa klabu hiyo na pia amekuwa akionekana kuwa karibu na klabu hiyo kama kuhudhuria mazoezi na kusuluhisha baadhi ya migogoro pale inapotokea mambo hayaendi sawa.

Kabla ya mchezo wa fainali ya kombe la Azam Sports Federation Cup kati ya Simba dhidi ya Mbao, ulipigwa mchezo wa utangulizi kati ya Azam Media dhidi ya Bunge FC ambapo Bunge FC walishinda 2-1. Baada ya mchezo huo, Mwigulu alionekana jukwaani akipigilia uzi mwekundu wa Simba wenye jina la Ajibu.

Si kitendo cha kawaida kwa shabiki au mpenzi wa timu hizo mbili kuvaa jezi ya mpinzani wake lakini pia si vibaya kuvaa kuonesha ushabiki na utani wa kweli kati ya timu hizo.

Haikujulikana mara moja kwa nini Mwigulu aliamua kuvaa jezi ya Simba dakika chache kabla ya game ya fainali kuanza kupigwa ambapo mechi ilimalizika kwa Simba kushinda 2-1 na kutwaa ubingwa wa ASFC unaowapa tiketi ya kufuzu kushiriki michuano ya kimataifa ya Afrika.

Mwigulu amekuwa akitumia vizuri ushawishi wake katika kuweka mambo sawa ndani ya klabu ya Yanga, kama unakumbuka ni yeye ndiye alipambana kumshawishi Hans van Pluijm kurejea Yanga mara baada ya kuandika barua ya kujiuzulu aliposia klabu hiyo inamleta George Lwandamina kuchukua nafasi yake bila yeye kujua.

Alionekana pia hotelini akihamasisha wachezaji wa Yanga siku moja kabla ya mchezo wa raundi ya pili kati ya Simba na Yanga na hata wachezaji walipotaka kugoma kucheza kutokana na kutolipwa mishahara, alikua mstari wa mbele kuwashawishi wacheze kwa maslahi ya klabu yao.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: UTAMU WA MADAM JESCA

Simulizi; MTOTO WA BOSS WANGU

SIMULIZI FUPI: UCHI WANGU UMENIPONZA