PATRICE LUMUMBA :MMOJA WA WAZALENDO MAARUFU BARANI AFRIKA


Mwanaharakati wa Marekani aliyekuwa akitetea haki za watu weusi Malcolm X alipata kusema “Hakuna kiongozi jasiri na mwenye msimamo kupata kutembea katika Ardhi ya Afrika kama Patrice Lumumba”.

Mwanaharakati kutoka Amerika ya Kusini Ernesto Che Guevara alipata kusema “Kuuawa kwa Lumumba ni pigo kubwa kwani alikuwa nguzo imara na muhimu sana aliyekuwa anapingana kabisa mabepari waliokuwa wanyonyaji hivyo basi tuungane pamoja kuupinga kwa nguvu kabisa ubepari.

Alikuwa mwanasiasa na mwanamapinduzi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mwaka 1958 alikuwa miongoni mwa waanzilishi wa Chama cha Taifa cha Kongo (kwa Kifaransa:Mouvement National Congolais). Mwaka 1960 alikuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya kuongoza harakati za kupigania uhuru kutoka kwenye utawala wa kikoloni wa Wabelgiji. Baada ya miezi miwili tu ya kuwa Waziri Mkuu, Lumumba alipinduliwa na baadaye kutiwa ndani kabla ya kuuawa katika mazingira ya kutatanisha katika eneo la Katanga upande wa kusini wa Kongo.

Aliuawa kikatili sana baada ya mateso mengi ya kikatili aliyopewa baada ya kuonekana mwenye msimamo na asiyetaka kuruhusu namna yoyote ya unyonyaji na ukoloni mamboleo.

Mwaka 2002 serikali ya Ubelgiji iliomba msamaha kwa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kuhusika katika kifo cha Patrice Lumumba

Kwa stori zaidi,Like page yetu kama bado.
Unaweza kushare na kusambaza zaidi post hii ili kupanua wigo wa Ukurasa kuwafikia watu wengi zaidi.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: UTAMU WA MADAM JESCA

Simulizi; MTOTO WA BOSS WANGU

SIMULIZI FUPI: UCHI WANGU UMENIPONZA