SEHEMU YA KWANZA
Tunapozungumzia vita vya kwanza vya dunia tunazungumzia vita vya mataifa makubwa yaliokuwa yakipigana kuanzia miaka ya 1914-1918. Vita hivi vilianzia huko Barani Ulaya, lakini baadae vita hivyo viliweza kufika hadi Afrika. Kwani nchi zilizokuwa zikipigana kwenye vita hivyo, zilikuwa na makoloni yake barani Afrika. Hivyo kwa namna Fulani bara la Afrika liliathiriwa na vita hivyo.
Ukweli ni kwamba takribani bara zima la Afrika lilihusika kwenye vita hivi vya dunia. Lakini kwa leo tuangalia kwa undani habari na historia ya vita vya dunia kwa upande wa kabila la Wangoni. Kwani wakati vita hivi vinatokea miaka iliyotajwa hapo juu, Tanganyika ilikuwa chini ya Wajerumani walioanza kutawala miaka ya 1890-1920. Hivyo basi kwa kuwa kwenye vita hii Wajerumani walihusika, basi kuna baadhi ya makabila ya Tanganyika yalihusika pia.
Kama inavyofahamika kuwa Wangoni walitokea Afrika kusini mwanzoni mwa miaka ya 1830. Na walipotoka huko waliweza kusambaa maeneo ya Afrika mashariki na kukaa maeneoa kama Unyamwezi, Ubena na Uhehe. Na walipokuwa wanakuja maeneo hayo walikuwa wakipambana sana na wenyeji hao. Lakini wakati wakoloni wanakuja miaka ya 1880, Wangoni waliamua kuungana na makabila wenyeji kama Wahehe kwa lengo la kupinga ukoloni. Na mwisho wa siku watu hawa wakawa chini ya Wajerumani.
Inasemakana kuwa Wangoni walishiriki kwenye vita vya dunia kwa kiasi kikubwa sana.na Unaambiwa kuwa Wangoni waliamua kujitolea tu kwa Wajerumani kwa lengo la kushinda vita. Na sababu ya kujitolea ni kwamba, Wangoni hawakuwa na nguvu sana, kwani wakati vita inaanza, kulishatokea vita vya Maji Maji(1905/1907 ambavyo Wangoni wengi walikufa pamoja na viongozi wao kama wakina Mzee Songea Mbano. Kwa hiyo hawakuwa wabishi katika kujitolea na kujiunga kwenye jeshi la mjerumani. Masimulizi ya vita hiyo yapo kama ifuatavyo.
NA MWAL.MAYUNI JOSEPH: 0654546353/0755671568
