Mmehalalishiwa usiku wa swaumu kuingiliana na wake zenu. Wao ni vazi kwenu na nyinyi ni vazi kwao. Mwenyezi mungu anajua kwamba mlikuwa mkizikhini nafsi zenu. Kwa hivyo amekukubalieni toba yenu na amekusameheni. Basi sasa changanyikeni nao na takeni aliyo kuandikieni mwenyezi mungu. Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni saumu mpaka usiku. Wala msichanganyike nao, na halim nakaa Itikafu msikitini .Hiyo ni mipaka ya mwenyezi mungu, basi msikaribie. Namna hivi mwenyezi mungu anabainisha ishara zake kwa watu ili wapate kumcha.
Qur'an (suratul baqarah 2:187 )
