Spika wa Bunge Job Ndugai ameieleza Serikali kwamba inaenda kulifikisha taifa mahali pagumu sana kwa kushindwa kumaliza tatizo la ongezeko la bei ya mafuta ya kula nchini na wakati huo amemuagiza Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage kuja na majibu ya tatizo hilo Bungeni haraka iwezekanavyo.
Kauli hiyo ya Spika imekuja baada ya Mbunge wa Nzega mjini Hussein Bashe aliyetaka kupata majibu ya Serikali kuhusu kupanda kwa bei ya mafuta hayo ambapo Waziri Charles Mwijage alimjibu kwamba jambo hilo linashugulikiwa ingawa kwa sasa kuna mvutano umeibuka baada ya meli mbili zenye mafuta kuzuiwa bandarini. VIDEO: