SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 3 Mei 2018

T media news

Maji yaifika shingoni Sudan, yatafakari kuhusu uwepo wa askari wake Yemen

Siku chache baada ya wabunge wa upinzani nchini Sudan kumtaka rais wa nchi hiyo Omar al Bashir awaondoe wanajeshi wa nchi hiyo huko Yemen, Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo ya amesema wanatafakari kuhusu uwezekano wa kuwarejesha nyumba wanajeshi wa nchi hiyo walioko Yemen.

 Ali Salem, Waziri wa Ulinzi wa Sudan alisema hayo jana Jumatano katika kikao na waandishi wa habari na kuongeza kuwa, vyombo vya dola vya nchi hiyo vinatathmini na kutafakari kuhusu suala la kushiriki wanajeshi wake katika vita dhidi ya Yemen.

Salem amenukuliwa na shirika la habari la Reuters akisema kuwa, "Tunafanya tathmini na tafiti katika siku hizi juu ya uwepo wa wanajeshi wetu nchini Yemen. Tumeweka kwenye mizani taathira za kushiriki kwetu kwenye vita dhidi ya Yemen, na karibuni hivi tutatoa uamuzi ambao utakuwa na manufaa kwa taifa letu na utulivu wake."

Baadhi ya mamluki wa Sudan waliouawa huko Yemen

Wabunge wa Muungano wa 'At-Taghyir' katika Bunge la Sudan unaojumuisha wabunge huru walitoa taarifa hivi karibuni na kusema: "Kushiriki Sudan katika vita vya Yemen ni kinyume cha katiba ya nchi na kwamba Bunge la nchi hiyo halikuafiki suala hilo la kutuma wanajeshi wake nchini Yemen."

Mamia ya mamluki wa Sudan wameshauawa huko Yemen wakati wakishiriki katika mashambulizi ya muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia, dhidi ya wananchi maskini wa Yemen uvamizi ambao ulianza mwishoni mwa mwezi Machi 2015, kwa lengo la kumrejesha madarakani Abdrabbuh Mansour Hadi, rais wa zamani wa nchi hiyo aliyejiuzulu na kutoroka nchi lengo ambalo hadi hivi sasa limekuwa ndoto kufikiwa