Rais Magufuli Atoa Maagizo Mazito kwa Kamishina wq Uhamiaji
Rais John Magufuli ameitaka Idara ya Uhamiaji kuhakikisha inapambana na wahamiaji haramu pasipo kumwogopa mtu. Amemwagiza Kamishna wa Uhamiaji, Dk Anna Makakala kuwachukulia hatua kali watumishi wake watakaoshindwa kutekeleza wajibu wao ipasavyo. Dk Magufuli akizungumza leo Jumatano Januari 31,2018 akizindua hati ya kusafiria ya kielektroniki jijini Dar es Salaam, amesema utambuzi wa wananchi wanaoishi bila vibali na wenye vibali vilivyoisha ni muhimu. Amesema uhamiaji ina jukumu kubwa katika kutekeleza hayo. "Haiwezekani wahamiaji haramu wanakamatwa Mbeya halafu wamepita Kilimanjaro, Manyara. Kamishna (Dk Makakala) ifike mahali unapoona hili washushe vyeo, mwondoe nyota moja ili wajue wajibu wao," ameagiza Rais Magufuli. Amesema awali Uhamiaji iligubikwa na matatizo yakiwamo ya utoaji hovyo wa vibali vya uraia, hata kwa watu ambao walikuwa hawana sifa. "Kuna raia wengi walipata uraia bila sifa na wapo waliopata uraia na vyeo vya juu kabisa serikalini wakati si ...