Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba, 2017

Ushahidi wa Picha Kuwa Irene Uwoya Kweli Kaolewa na Dogo Janja Huu Hapa

Picha
Picha ya kwanza ya kuthibitisha harusi ya DOGO JANJA na IRENE UWOYA!! Babu Tale ameipost kwenye page yake ya Instagram kumkaribisha Uwoya kwenye familia ya TIPTOP. Nadhani mpaka hapo mdau wangu utakuwa umeamini kuwa wameoana kweli

PICHA: Ofisi ya Rais-Utumishi wahamia Dodoma

Picha
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imeendelea na utekelezaji wa agizo la Rais Dkt Magufuli la kuhamia Dodoma ambapo jana, jumla ya wafanyakazi 143 wa ofisi hiyo walihamia rasmi Makao Makuu ya Nchi, Dodoma. Akizungumza wakati wa uhamaji, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Bi. Jane Kajiru alisema kuwa, hii ni awamu ya pili na kuhama na katika awamu hii wameigawanya katika makundi mawili. Alisema watumishi hao 143 wameondoka pamoja na vifaa vyao na kwamba katika awamu ya kwanza, watumishi 78 walihamia Dodoma. Bi. Kajiru alisema kwamba, awamu ya mwisho ya zoezi la kuhamia Dodoma ni mwaka ujao wa fedha 2018/19 au mara tu fedha za kuhama zitakapopatikana. Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bibi. Dorothy Aidan Mwaluko akiagana na Kiongozi wa msafara wa magari yaliyobeba mizigo ya ofisi hiyo WOII Mohamed Bakar ikiwa ni muendelezo wa zoezi la kuhamia Dodoma leo Jijini Dar es Salaam. Jumla ya wafanyakazi 143...

Uhuru Kenyatta Atangazwa Mshindi Wa Urais Nchini Kenya Kwa Asilimia 98

Picha
Hatimaye Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC) imemtangaza Uhuru Kenyatta kuwa mshindi wa kinyang’anyiro cha urais baada ya kujikingia kura 7,483, 895 sawa na asilimia 98 katika uchaguzi wa marudio uliosusiwa na mpinzani wake mkuu, Raila Odinga.   Kwa matokeo hayo, Rais Kenyatta na makamu wake William Ruto walikabidhiwa vyeti vya ushindi na sasa Uhuru anasubiri kuapishwa kuiongoza nchi kwa miaka mitano ikiwa matokeo hayo hayatapingwa na kufutwa.   Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati alitangaza matokeo hayo bila kura kutoka majimbo 25 ya eneo la Nyanza ambalo wafuasi wa Odinga walifanya vurugu na kusababisha uchaguzi kuahirishwa.   Chebukati alisema mazingira yaliyokuwa yameandaliwa kwa ajili ya uchaguzi wa marudio yaliwezesha kuwa wa kuaminika, huru na wa haki.   Akizungumza mapema, Makamu mwenyekiti wa IEBC Consolata Nkatha alisema kura za maeneo ambayo hayakufanya uchaguzi hayawezi kuathiri matokeo ya mwisho. Nkatha alisema mchakato ulikamilika katika m...

Wizara Ya Afya Yatoa Tahadhari Ya Ugonjwa Wa Marburg

Picha
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepokea taarifa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO), mnamo tarehe 19 Oktoba 2017 kuhusu ugonjwa wa Marburg ambao umejitokeza katika nchi jirani ya Uganda tangu tarehe 17 Octoba, 2017. Maeneo yaliyoathirika  na ugonjwa huo ni Wilaya ya Kween, Kanda ya Mashariki ya nchi, ambayo  inapakana n nchi ya  Kenya. Hadi kufikia  tarehe 19 Oktoba 2017, watu 4 walikwishapata maambukizo ya ugonjwa huo, ambapo wawili kati yao   wamepoteza maisha. Wizara  inatoa tahadhari ya Ugonjwa huu kwa wananchi  katika mikoa yote ya Tanzania, hususan kwa wale wanaoishi  katika mikoa ambayo inapakana na na nchi  ya Uganda (Mikoa ya Mara, Mwanza na Kagera). Ugonjwa wa Marburg  unafanana sana na ugonjwa wa Ebola. Virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Marburg vinajulikana kama  “Marburg Virus”, navyo vipo katika jamii moja na virusi vinavyosababisha Ebola (Ebola virus). Ugonjwa huu ni m...

Serikali yamjibu Zitto Kabwe......Yampa ONYO Kali

Picha
Na.Jacquiline Mrisho – MAELEZO. Serikali imetoa onyo kali kwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Mh. Zitto Kabwe juu ya taarifa za upotoshaji wa takwimu za Pato la Taifa alizozitoa hivi karibuni. Taarifa hizo za Mh. Zitto zimeripoti kuwa ukuaji wa Pato la Taifa kwa robo ya pili ya mwaka 2017 kuwa ni asilimia 5.7 badala ya asilimia 7.8. Kasi ya ukuaji ya asilimia 5.7 ilikuwa ni kwa robo ya kwanza ya Januari hadi Machi 2017. Onyo hilo limetolewa jana Jijini Dar es Salaam na Bw. Daniel Masolwa Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa kutoka Ofisi ya Taifa za Takwimu (NBS),kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NBS,pamoja na  Mkurugenzi wa Sera na Tafiti za Uchumi wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw.Johnson Nyella wakati wakizungumza na Waandishi wa Habari. Masolwa alisema kuwa upotoshaji huo uliofanywa na Mh. Zitto ni wa makusudi na unalenga kuonesha kuwa juhudi znazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano hazina manufaa kwa Wananchi. “Napenda kukanusha kauli ya Mh. Zitto kuhusu taarifa zake ...

Mdee amtahadharisha Nyalandu kuhusu CHADEMA

Picha
Mbunge wa Kawe jijini Dar es salaam, Halima Mdee amemkaribisha na kumtahadharisha aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu akimtaka ajiandae kisaikolojia kupambana na changamoto wanazokumbana nazo viongozi wa Chadema. Ameyasema hayo kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter kumkaribisha ndani ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mara baada ya kutangaza kukihama Chama cha Mapinduzi (CCM) na kujiuzulu nafasi ya Ubunge. “Mhe. Nyalandu karibu sana CHADEMA. Naamini utakuwa imara kukabiliana na siasa za chuki, ubaguzi na visasi zinazolikabili taifa letu, hivyo naimani umechukua maamuzi mazuri ila jiandae kukabiliana na changamoto,” amesema Mdee Jana  Nyalandu ambaye alikuwa Mbunge wa Singida Kaskazini na Mjumbe wa Halmashauri ya Kamati  Kuu CCM alitangaza kujiuzulu nafasi zake hizo kwa kile alichodai kwamba hafurahishwi na mambo ya kisiasa yanayoendelea nchini na kuwaomba wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kama wataridhia wampe na...

Rais Magufuli Aeleza Sababu za Kutokugawa Milion 50 Alizoahidi Kwa Kila Kijiji

Picha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, ameeleza sababu zinazomfanya achelewe kutimiza ahadi ya milioni 50 kwa kila kijiji alizoziajidi wakati wa kampeni za kugombea urais kuwa ni kutokana na kuwepo kwa mambo mengi nchini yanayohitaji utekelezaji wa haraka. Rais Magufuli ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Mwanza katika mkutano wa hadhara ikiwa ni moja ya vitu alivyopanga kuvifanya katika ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani hapo. Ameeleza kuwa ameona ni sahihi kuanza na mambo ya muhimu zaidi kama vile miundombinu ya barabara, huduma za afya pamoja na elimu kabla ya kutoa fedha hizo ambazo aliziahidi katika iilani ya uchaguzi wa mwaka 2015. “Halitokuwa jambo jema mimi kutoa milioni 50 kwa kila kijiji nchini wakati huduma mbalimbali kama vile elimu, afya na miundombinu ya barabara na usafirishaji haijakaa vizuri. lakini niwahakikishie kuwa hizo fedha zipo na zitakabidhiwa kwa kila kijiji kama nilivyosema,”...

Nape Akanusha Kuita Waandishi wa Habari Leo

Picha
Mbunge wa jimbo la Mtama kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi  (CCM) Nape Nnauye amefunguka na kuweka sawa kuwa leo  Oktoba 31, 2017 hatakuwa na mkutano wowote na vyombo vya habari na kusema kuwa watu wanatunga hizo taarifa. Nape Nnauye ametoa kauli hiyo kupitia mtandao wake wa kijamii na kuwataka watu waache kumzushia mambo wakiwa na lengo la kutafuta nafasi na vyeo serikalini. "Acheni kupiga ramli juu ya kesho yangu!! Kisa mnatafuta vyeo na hamuwezi kutumia akili kufikiri! Sina 'press conference' kesho"  aliandika Nape Nnauye Jana mchana watu wasio na nia nzuri na Nape Nnauye walizusha taarifa kuwa kiongozi huyo  leo Jumanne atakuwa na mkutano na waandishi wa habari jambo ambalo yeye mwenyewe amelipinga na kusema watu wanazusha taarifa hizo kwa maslahi yao wenyewe.

Mbowe Amkaribisha Nyalandu CHADEMA

Picha
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Freeman Aikael Mbowe, amemkaribisha aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM , Lazaro Nyalandu baada ya kuweka wazi matamanio yake wapi pa kwenda baada ya kujiuzulu.  Mwenyekiti Mbowe ametoa fursa ya kumkaribisha ndani ya chama hicho Mhe. Nyalandu kupitia ukurasa wake wa Twitter na kumwambia kuwa hata masuala aliyoyaibua yalikuwa ni ajenda ya chama chao kwa muda mrefu. "Milango iko wazi kwako Lazaro Nyalandu  kujiunga na CHADEMA. Masuala uliyoyaibua yamekuwa ajenda yetu kuu kwa muda mrefu"  ameandika Mh. Mbowe. Mh. Nyalandu ambaye alikuwa Mbunge wa Singida Kaskazini na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM jana  alitangaza kujiuzulu nafasi zake hizo kwa kile alichodai kwamba hafurahishwi na mambo ya kisiasa yanayoendelea nchini na kuwaomba wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kama wataridhia wampe nafasi ili kuweza kuleta mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi kupitia chama hicho.

BREAKING: Zitto Kabwe akamatwa na Polisi asubuhi

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, amekamatwa na Jeshi la Polisi mapema leo asubuhi akiwa nyumbani kwake jijini Dar es salaam  na kupelekwa katika Kituo cha Polisi Chang’ombe. Jeshi la Polisi bado halijaeleza sababu ya kumakamata, lakini Chama cha ACT Wazalendo, kupitia kwa Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Yeremiah Kulwa Maganja  wamesema kwamba, sababu ya kukamatwa kwa Zitto Kabwe ni kutokana na mkutano wao wa uzinduzi wa kampeni uliofanyika Kijichi mwishoni mwa juma. Aidha, ACT Wazalendo wameeleza kwamba, wanasheria wa Chama wanashughulikia kujua sababu za ukamatajwi huo Zitto ambaye pia ni kiongozi wa chama hicho.

Akamatwa na risasi 356 akienda kuua Faru Hifadhi ya Serengeti

Picha
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamisi Kigwangalla ameweka wazi kuwa moja ya mikakati ya Wizara yake hiyo ni kuhakikisha wanachukua hatua za haraka katika kulinda rasilimali za Taifa kwa kutumia mbinu za kisasa zaidi za intelijensia kudhibiti ujangili nchini. Dkt. Kigwangalla amesema hayoi mapema leo mjini Dodoma wakati wa akielezea namna walivyojipanga kukamata majangili kabla hawajhafanya ujangili. “Tumekusudia kukamata majangili kabla hawajafanya ujangili kuliko kukamata nyara. Tutaisambaratisha na kuifumua kabisa mitandao ya biashara haramu ya ujangili nchini, “   ameeleza Dkt.Kigwangalla Aidha, ameendelea kutuma salamu kwa majingili wote kuachana na baishara hiyo kwa kujisalimisha ama kukimbia kwani kwa sasa wanaendelea na uchunguzi wa mtandao mpana wa majingili. “Jana tumefanikiwa kumkamata Ndg. Masalu Wella Nangale wa Kijiji cha Mwasengela, Meatu, akijipanga kuelekea Moru, ndani ya Hifadhi ya Serengeti kwa malengo ya kuua Faru. Amekutwa na risasi 356,...

Zitto Kabwe ampongeza Nyalandu

Picha
Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT Wazalendo), Zitto Kabwe amempa tano Mbunge wa Singida Kaskazini(CCM), Lazaro Nyalandu kuwa ameonyesha uongozi. Zitto ametoa maoni yake hayo baada ya Nyalandu kuamua kujiondoa CCM na kuachia nafasi yake ya ubunge. Zitto ameandika, "Lazaro Nyalandu, umeonyesha uongozi. Kwa namna haki za watu zinavyovunjwa na uchumi wa nchi unavyoporomoka, unahitaji roho ngumu sana kuwa CCM. Umefanya maamuzi sahihi, wakati sahihi na kwa sababu sahihi. Kila la kheri." Lazaro Nyalandu leo ametangaza kujivua nafasi zake ndani ya Chama Cha Mapinduzi na kuandika barua yake ya kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge kwa kile alichodai kuwa Chama Cha Mapinduzi na Bunge vimekuwa vikishindwa kuisimamia serikali na badala yake kutumiwa na serikali jambo ambalo yeye anaona halina afya katika maendeleo ya nchi na linadidimiza haki mbalimbali. 

Mzazi Mwenzie na Joti Ampa Makavu Steve Nyerere 'Wewe ni Mkubwaa Jielewe Ufupi Usikufanye Ukajiona Bado Mdogo'

Picha
Mwanamama aliyezaa na msanii wa vichekeshomaarufu kama Merisa Bushoke amemtolea povu Steve Nyerere baada ya kumpongeza Joti kwa kufanikisha kufunga ndoa . Kupitia ukrasa wake wa instagram steve Nyerere alianza kwa kuandika hivi  "Hii ni familia mpya ndugu yangu Joti ' hakuangalia ule usemi mama wa kambo si mtu mzuri ameangalia mapenzi na utu wa anayemuoa kwa watoto wake na familia yake si wamama wakambo wote wana roho mbaya apana, bali mazingira ya hiyo roho inawekwa na wewe baba kama huna misimamo ya familia yako kwa mwanamke mwenyewe mwenye kukupenda wewe  atapenda na watoto wako na familia yako. Joti jana ulilia ukumbini nikajiuliza kwanini ulilia  nikapewa jibu mtoto wako amepata mtoto bora  huo nao ni ujasiri  sana kuhakikisha  mama huyo mnayeingia naye  mkataba wa kidini anakuwa mama bora, tumekuwa watu wa kukalili unayezaa naye ndio mama bora  kumbe si kweli  Joti umetengua kauli Joti wewe ni shujaaaa,,,,," aliandika steve Nyerere ...

Chadema Yamjibu Lazaro Nyarandu Yakubali Ombi Lake la Kuamia Chama Hicho

Picha
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimejibu ombi la aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu ambaye leo amejiuzulu wadhifa huo na kukihama chama cha CCM na kuomba kujiunga CHADEMA. Akiongea na mwandishi wa East Africa Television, Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema, amesema CHADEMA inamkaribisha mtu yeyote anayetaka kujiunga na chama hicho, kwani chama cha siasa ni watu.

Meya wa Jiji la Mwanza, James Bwire Anashikiliwa na Polisi

Picha
 Meya wa Jiji la Mwanza, James Bwire anashikiliwa na Polisi huku ikidaiwa kuwa amri ya kukamatwa kwake ni agizo la mkuu wa mkoa huo, John Mongella. Hayo yamesemwa na Mariam Lima ambaye ni katibu wa mitandao ya taasisi ya Alliance inayomilikiwa na Meya Bwire ambaye ameeleza kuwa kuwekwa kwake sentro ni kunatokana na agizo la mkuu wa mkoa. Hata hivyo, Mongella amekana kuamuru kukamatwa kwa kiongozi huyo anayeshikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Jiji la Mwanza. “Nimepata taarifa za meya kuwekwa mahabusu; mimi sihusiki na ninazifuatilia kujua kinachoendelea,” amesema Mongella leo Jumatatu Oktoba 30,2017. Taarifa zinasema meya Bwire amekamatwa katika Uwanja wa Ndege Mwanza wakati wa mapokezi ya Rais John Magufuli ambaye ziko ziarani mkoani humo. Lima amesema, “Tunafanya jitihada za kumwekea dhamana ingawa tunakabiliana na changamoto nyingi.” Tangu Aprili, Bwire na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba wamekuwa katika mgogoro kila upande ukiu...

NI KWELI CCM HII IMEPOTEZA MWELEKEO.....! NI KWELI CCM HII SIYO ILE CCM YA AKINA NYALANDU!!

Picha
CCM hii siyo ile ya kupakia Twiga kwenye ndege....! CCM hii siyo ile ya viongozi kujigawia vitalu vya uwindaji........! CCM hii siyo ile ya kufanya biashara ya pembe za ndovu. CCM hii siyo ile ya kufanya biashara ya pembe za faru... CCM hii siyo ile ya Richmond..... CCM hii siyo ile ya Escrow........ CCM hii siyo ile ya kugawana kodi zetu kwenye migodi..... CCM hii siyo ile ya EPA wala siyo ile CCM ya wapiga dili.. KWELI HII SIYO CCM ILIYOKUWA MOYONI KWA NYALANDU!!

Breaking News: Lazaro Nyalandu Amejiuzulu Nafasi Yake Ndani ya CCM na Kuomba Kuungana na Chadema

Picha
Mbunge wa Singida Kaskazini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Lazaro Nyalandu amejiuzulu nafasi yake ndani ya CCM na kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge kupitia (CCM) kwa kile alichodai hafurahishwa na mambo ya kisiasa yanayoendelea nchini. Taarifa ambayo ameitoa leo Nyalandu amesema kuwa ameamua kuachana na CCM na sasa anaomba kuungana na CHADEMA kama watapendezwa na yeye kujiunga huko. Nimeamua kujiuzulu nafasi yangu ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, pamoja na nafasi zote za Uongozi ndani ya Chama kuanzia leo, Oktoba 30, 2017. halikadhalika, asubuhi ya leo nimemwandikia Spika wa Bunge, Mh. Job Ndugai, Mb., barua ya kujiuzulu nafasi yangu ya Ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia tiketi ya CCM, nafasi ambayo nimeitumikia kwa vipindi vinne mfululizo tangu nilipochaguliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2000 hadi Sasa" aliandika Nyalandu "Nimechukua uamuzi huo kutokana na kutorishwa kwangu na mwenendo wa hali ya Kisiasa nchini, ikiwa ni pamoj...

Raila Odinga Kujitangaza Rais wa Kenya

Picha
Muungano wa upinzani wa National Super Alliance (NASA) unakusudia kutamtangaza Raila Odinga, kuwa Rais wa Kenya iwapo Rais Uhuru Kenyatta ataapishwa. NASA umetoa changamoto kwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), isithubutu kumtangaza Rais Kenyatta mshindi wa uchaguzi wa urais wa marudio uliofanyika Oktoba 26, ambao Odinga alisusia kushiriki. Dhamira hiyo ya NASA ilitangazwa mwishoni mwa wiki iliyopita na Seneta wa Siaya, James Orengo katika mkutano wa hadhara iliofanyika huko Machokos. Seneta Orengo alisema viongozi wa NASA wameapa kutumia matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Agosti 8, kumtangaza Odinga kuwa Rais wa Kenya. “Tutatumia matokeo ya Agosti 8 kumuapisha mgombea urais wa NASA, Raila Odinga kuwa rais iwapo Uhuru Kenyatta atajaribu kutumia matokeo ya uchaguzi wa urais wa Oktoba 26 kuapishwa,” alionya Orengo. Alisema kwa mujibu wa Katiba, Wakenya wana mamlaka huru na sauti zao lazima zisikilizwe. “Mamlaka ya utendaji ya Jamhuri ya Kenya iko mikononi mwa watu ...

Kidato cha Nne Waanza Kufanya Mtihani wa Taifa Leo

Picha
WATAHINIWA wapatao 385,938 wameanza kutafanya mitihani ya Taifa ya Kidato cha Nne leo Jumatatu, Oktoba 30, 2017 kote nchini. Akizungumza jana Jumapili, Oktoba 29,2017 Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde alisema kati ya watahiniwa hao, 323,513 (School candidates) ni wa shule na 62,425 ni wa kujitegemea (Private candidates). Dk Msonde alisema mitihani hiyo itaanza leo Oktoba 30, 2017 na kumalizika Novemba 17, 2017 huku akieleza kuwa maandalizi ya mitihani yameshakamilika na mitihani imeshafika kwenye vituo. Aidha Msonde alizitaka kamati za mitihani za mikoa na halmashauri kuhakikisha utaratibu wa uendeshaji wa mitihani hiyo unafuatwa huku akiwataka wanafunzi kuacha vitendo vya udanganyifu wakati wa kufanya mitihani kwa kuwa wanaweza kufaulu bila kufanya hivyo. “Mliyojifunza yanatosha fanyeni mitihani kwa kufuata utaratibu uliowekwa, baraza halitasita kuwafutia mitihani wote watakaojihusisha na udanganyifu, wasimamizi wa mitihani wajiepush...

CUF Wagoma Maalim Seif Kupimwa Akili

Picha
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi, Ahmed Nassor Mazrui amesema Katibu Mkuu wa CUF hatopimwa akili na wale wanaosema Maalim Seif Shariff Hamadi akafanyiwe uchunguzi huo ni vyema wakaenda wao. Mazrui alisema Maalim Seif hawezi kupimwa akili kwa kuwa yupo ngangari na ana akili timamu kwa kila anachokifanya; kwa maslahi ya chama na Wazanzibari kwa ujumla. Akizungumza katika mkutano mkuu wa wilaya ya Mjini wa chama hicho hapa Zanzibar juzi, Mazrui alisema Maalim Seif ni mwenye akili timamu na kutaka wote wanaotoa madai hayo ya kupima akili wapuuzwe. Alisema kuonyesha katibu huyo ni mwenye akili timamu amekuwa akigombea nafasi ya urais ndani ya chama hicho kwa kipindi cha miaka 25 bila ya kuchoka, kutetereka wala kukata tamaa. Alisema katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, Maalim Seif ndiyo nguli wa siasa na kuwataka wafuasi wa chama hicho kutovunjika moyo kwani kiongozi wao huyo yupo makini na anaendelea kuidai haki ya Wazanzibari "iliyoporwa" Oktoba 25, 2015. Mat...

Mbivu Mbichi Leo Hatima ya Ubomoaji Mjengo wa Mchungaji Getrude Rwakatale

Picha
HATIMA ya ubomoaji wa nyumba ya kifahari ya Mchungaji wa kanisa la TAG Mikocheni, Getrude Rwakatare, inatarajiwa kuanza kujulikana leo wakati Naibu Waziri mpya wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Kangi Lugola atakapotoa ripoti. Wiki iliyopita Lugola aliomba Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kumpatia taarifa ya kukwama mwaka jana kwa ubomoaji wa 'hekalu' hilo lililopo Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam. Rais John Magufuli alifanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri Oktoba 7 ambapo miongoni mwa sura mpya ni Naibu Waziri Lugola ambaye amechukua nafasi ya Luhaga Mpina aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi. "Taarifa tayari ipo ofisini kwangu (tayari) nitaipitia Jumatatu (leo)," alisema Lugola ambaye alikuwa kwenye ziara mikoani wakati akizungumza na Nipashe mwishoni mwa wiki. "Umma unataka kujua, hivyo siyo jambo la kucheleweshwa." "Niliagiza nipatiwe taarifa ya tangu (sakata) ilivyoanza ili nijue ugumu (wa kubomoa) u...

Hatimaye Mmoja wa Watoto Pacha Waliotenganishwa India Afungua Macho

Picha
Mmoja wa watoto pacha ambao walizaliwa wakiwa wameshikana kwenye vichwa amefungua macho yake siku nne baada ya upasuaji wa kuwatenganisha nchini India. Jaga, mwenye umri wa miaka miwili aliweza kuitikia ishara ndogo kama kusongesha mikono yake. Watoto hao walizaliwa wakiwa wanatumia kwa pamoja mishiba na nyama za ubongo na upasuaji uliochukua saa 16 uliwatenganisha. Watoto hao wote wako hali nzuri na madaktari wameridhishwa na vile wanavyoendelea hadi sasa, Pacha hao wanaotokea kijiji kilicho mashariki mwa jimbo la Orissa nchin India, walishikana kwenye kichwa hali inayofahamika kama craniopagus. Craniopagus hukumba mtoto mmoja kati ya watoto milioni 3 wanaozaliwa na asilimia 50 ya wale wanaopatwa na hali hiyo hufariki saa 24 baada ya kuzaliwa.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un Ametembelea Kiwanda cha Bidhaa za Urembo

Picha
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un ametembelea kiwanda ya bidhaa za urembo mjini Pyongyan akiandamana na mke wake Ri Sol-ju na dada yake Kim Yo-jing. Kuoneka hadharani kwa Kim Yo-jong, kunakuja muda mfupi baada ya kupandishwa cheo ndani serikali ya Korea Kaskazini. Bidhaa za urembo kutoka nchi za kigeni zimekuwa adimu nchini Korea Kaskani kutokana na vikwazo. Korea Kaskazini inaonekana kujenga sekta yake ya bidhaa za urembo ambapo bidhaa kama Bomhyanggi na Unhasu vimepata umaarufu. Licha ya umaarufu wake wa kupigwa picha akiwa katika vituo vya kijeshi na maeneo ya kufanyia majiribio makombora, ziara ya Kim katika kiwanda cha bidhaa za urembo ni moja ya propaganda ya kuhalalisha utawake wake kwa watu wa Korea Kaskazini. Ziara hiyo "ni ya kuonyesha kuwa Korea Kaskazini inaweza kuwatunza watu wake na kuleta maendeleo kwa kiwango sawa na cha China na Korea Kusini," mdadisi wa masuala ya Korea Kaskazini Ankit Panda aliiambia BBC. "Licha ya sisi kujua kuwa sio ukwe...

Mtibwa Suga Yashindwa Kuonyesha Ubavu Wake kwa Singida United

Picha
Mechi tano za raundi ya nane ligi kuu soka Tanzania bara zimemalizika  huku Mtibwa Sugar ikishindwa kupaa kileleni baada ya kulazimishwa sare tasa na Singida United. Mtibwa Sugar imelazimishwa sare hiyo kwenye uwanja wake wa nyumbani hivyo kushindwa kukaa kileleni baada ya kufikisha alama 16 na kulingana na timu za Simba, Yanga na Azam FC. Mechi nyingine za jana ni ile kati ya Kagera Sugar dhidi ya Ndanda FC ambapo Kagera Sugar imepata ushindi wake wa kwanza baada ya mechi 7, ikishinda mabao 2-1. Lipuli FC imeshinda mabao 2-1 dhidi ya Mbao FC. Njombe Mji ikiwa nyumbani imelazimishwa sare tasa na Stand United huku Majimaji ikitoka sare ya bao 1-1 na Mwadui FC. Kesho kutakuwa na mchezo mmoja wa kukamilisha raundi ya nane kati ya Tanzania Prisons dhidi ya Ruvu Shooting.Nafasi tano za juu kwenye msimamo zinashikiliwa na Simba yenye alama 16 ikifuatiwa na Yanga SC, Mtibwa Sugar na Azam FC zenye alama 16 pia. Singida United wanashika nafasi ya tano wakiwa na alama 13. Nafasi tatu za ...

Hizi Hapa Faida na Maajabu Yanayotokana na Kunywa Maji ya Uvuguvugu Kila Asubuhi

Picha
Inawezekana unatumia kikombe cha chai  au kikombe cha  kahawa kila siku asubuhi, wengi wao hutumia maji ya kawaida ili kuanza siku vizuri. Hivi vitu vimekuwa ndio tabia ya kila siku , hata hivyo wachunguzi wanasema kunywa maji ya uvuguvugu  asubuhi wakati tumbo halina kitu unapata faida  za kiafya zaidi. Madactari wanashauri kutumia maji ya uvuguvugu   yaliotiwa  liau au ndimu ili  kupunguza radical ndani ya mwili. Kutumia maji ya moto  inaongeza na kufungua utumbo ili kukufanya wewe upate haja kubwa kwa urahisi Na hapa kuna faida 7  za vitu vinavyotokea katika mwili wako utakapoanza kutumia maji ya moto kila asubuhi. 1.Yanasaidia kuondoa Mikunjo. Kunywa maji inakusaidia usizeeke mapema,hakuna mtu anaependa kuzeeka mapema.hata hivyo  sumu ndani ya mwili inaweza kukufanya uzeeke mapema. Wakati mwili wako unapotoa sumu  utapunguza magonjwa   na uzee. Maji ya  moto usaidia kuondoa sumu na yanasafisha kabisa. ...

LIVE: Fautilia hapa matangazo ya ziara ya Rais Magufuli mkoani Mwanza

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 30 Oktoba 2017, amewasili mkoani Mwanza, ambapo pamoja na mambo mengine atafungua Mradi wa Ujenzi wa daraja la watembea kwa miguu lililopo eneo la Furahisha. Baadae Rais Magufuli atafungua Kiwanda cha Vinywaji baridi cha Sayona kilichopo Nyakato mkoani humo na kufanya Mkutano wa Hadhara. Fuatilia moja kwa moja matangazo ya ziara ya Rais Magufuli hapa chini;

Zitto Kabwe Amwaga 'Sumu' Mbagala, Dsm

Picha
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amezindua kampeni za chama hicho za uchaguzi mdogo wa udiwani akiahidi iwapo kitachaguliwa kitaondoa hali ngumu ya uchumi na ukiukwaji wa haki. Zitto akizungumza katika Kata ya Kijichi mkoani Dar es Salaam leo Jumapili Oktoba 29,2017 amesema wananchi watumie uchaguzi mdogo katika kata 43 nchini utakaofanyika Novemba 26,2017 kutuma salamu kwa CCM kwamba hawaridhishwi na jinsi nchi inavyoendeshwa. Amesema mtu akitaka kujua uchumi unasinyaa, aangalie alikuwa akipata shilingi ngapi na sasa anapata ngapi. Zitto amewaomba wananchi wa Kijichi kumchagua mgombea udiwani wa ACT Wazalendo, Edgar Mkosamali ili kuwe na mabadiliko kwenye baraza la madiwani la Halmashauri ya Temeke. Kiongozi huyo amelalamikia kuzuiwa kwa mikutano ya hadhara akidai ni ukiukwaji wa Katiba na sheria za nchi na pia kuwanyima wananchi haki ya kukusanyika kwenye vyama vyao. "Leo hii tunasubiri uchaguzi mdogo ndiyo tufanye mikutano ya hadhara. Kama hupendezwi na ha...

Gharama za Kumtunza Faru Fausta Kupunguzwa

Picha
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), imeanza kulima majani aina ya lusini ambayo ni chakula cha Faru Fausta ili kupunguza gharama za kumtunza mnyama huyo. Faru Fausta mwenye miaka 54 anahifadhiwa kwenye banda ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro ikiwa ni hatua ya kumlinda asiliwe na wanyama wengine kutokana na jicho lake kutoona. Amekuwa akitumia bandali 250 za majani kila baada ya miezi minne yanayoigharimu mamlaka hiyo Sh5 milioni. Majani hayo hununuliwa kutoka nchi jirani ya  Kenya. Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Idara ya Malisho na Usimamizi wa Wanyama NCAA, Hillary Mushi amesema mamlaka imeandaa shamba lenye ukubwa wa eka mbili na imepanda mbege za lusini. Amesema ndani ya miezi saba majani hayo yataanza kuvunwa. Mushi amesema NCAA imechukua hatua hiyo ili kupunguza gharama za kumtunza faru huyo, ambaye amekuwa moja ya kivutio cha watalii na watafiti kutokana na kuwa ndiye faru mwenye umri mkubwa kuliko wote duniani kati ya wanaoishi maeneo ya wazi hifadhini. A...

RC Makonda 'Sitaki Kusikia Viongozi wa Dini Wakisumbuliwa'

Picha
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda amewataka Viongozi wa Dini  zote Waislam na Wakristo wenye matatizo yanayohitaji msaada wa Serikali ikiwemo Migogoro na Kesi kufika Ofisi kwake ili yaweze kupatiwa ufumbuzi. RC Makonda amesema hayo wakati wa Ibada ya uzinduzi wa Kanisa la KKKT Ubungo iliyoenda sambamba na Jubilee ya Miaka 500 ya Ujenzi wa Kanisa. Amesema kuwa Viongozi wa Dini wanafanya kazi kubwa ya kiroho katika kuijenga Jamii Bora hivyo hawapaswi kuzungushwa na Watendaji wa Serikali pale wanapohitaji kuhudumiwa kwakuwa thamani ya kazi wanayoifanya ni kubwa. "Mimi sio Mkuu wa Mkoa bali mimi ni Mtumishi wa Mungu katika Ofisi ya Mkoa wa Dar es salaam, Niwaombe Viongozi wote wa Dini Dar es Salaam sasa hivi msiangaike mkiwa na kesi kwenda kwa Wenyeviti wa Mtaa au Watendaji wa Mtaa, mkiwa na tatizo lolote njooni Ofisin kwangu, mimi ndio nitawatafuta hao, nisingependa kuona Kanisa au Msikiti wanasumbuliwa na Migogoro isiyoeleweka kwa misingi ya watu fulani, njoo...

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya Octoba 30

Picha