Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Mh.Zitto Kabwe amesema kuwa wanasikia pato la taifa linakuwa na ni miongoni kati ya nchi 20 ambalo pato la taifa lina kuwa kwa kasi wakati anasikia malalamiko ya wananchi wanasema hali mbaya na vyuma vimekaza.
Zitto ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari, kuhusu Takwimu za pato la Taifa amesema kuwa ni wajibu wa mchumi kujiuliza inakuaje tuna pato la taifa linalokuwa yani miongoni mwa nchi 20 duniani ambazo uchumi wake unakuwa kwa kasi sana lakini wakati huo huo wananchi wanalia.
“Tunasikia pato la taifa linakuwa na ni miongoni kati ya nchi 20 ambalo pato la taifa linakuwa kwa kasi kuliko nchi zingine lakini wakati huo huo mnasikia malalamiko ya wananchi wanasema hali mbaya, vyuma vimekaza sasa ni wajibu wa mchumi kujiuliza inakuaje tuna pato la taifa linalokuwa yani miongoni mwa nchi 20 duniani ambazo uchumi wake unakuwa kwa kasi sana lakini wakati huo huo wananchi wanalia kwamba vyuma vimekaza kwamba hali ni mbaya,” amesema Zitto.
“Kwanini sasa miaka ya nyuma tulikuwa hatutazami na kwakweli hata tulipotazama safari hii tumekuta miaka ya nyuma hakuna shida yani mpaka mwezi Machi 2017 takwimu zilizokuwa zinatolewa na serikali na takwimu ambazo unazikokotoa kutokana na hali ya uchumi na kanuni za uchumi hazina utofauti zilikuwa sawa kabisa lakini takwimu za mwezi AprilI,Mei,June zimeonyesha tofauti kubwa sana na ndicho kilicho tuletea mashaka.”