Je umewahi kutuma ujumbe, picha au video kimakosa katika mtandao wa whatsapp?
Fikiria umetuma ujumbe kimakosa kwa baba yako wakati ulilenga kumtumia mpenzi wako, utajisikiaje? huwa unakuwa na hali gani? je utamuelezaje kuwa hukulenga kumtumia yeye?
Kumekuwa na kesi kadha wa kadha ambazo watu wanaoheshimika kukosea kutuma jumbe kimakosa jambo ambalo linawafanya wapoteze heshima mbele ya jamii inayowazunguka.
Mwaka mmoja uliopita mchungaji wa kanisa moja huko Afrika Kusini alijinyonga baada ya kutuma kimakosa picha za utupu katika kundi la WhatsApp (WhatsApp group) la waumini wake, aliyolenga kumtumia mpenzi wake (mchepuko) kumtaarifu kuwa mke wake hayupo.
Mtandao wa WhatsApp umeleta chaguo ambalo sasa watumiaji wanaweza kufuta ujumbe walioutuma kimakosa ambao mpokeaji hatauona, ila atapata taarifa kuwa ujumbe huo umefutwa.
Utaweza kuufuta ujumbe ulioutuma kimakosa kabla ya dakika saba kuisha tokea ujumbe ulipotumwa. Baada ya dakika saba kuisha haitowezekana tena kuufuta.
Ili kuweza kufuta ujumbe ulioutuma kimakosa inabidi uwe una programu ya WhatsApp iliyoboreshwa (Updated)
Baada ya kutuma ujumbe kimakosa, bonyeza na shikilia kwa muda (Press and hold) ujumbe huo, kisha nenda kwenye alama ya kufuta (delete)Utapata machaguo matatu kama hivi
Chagua ‘delete for everyone’Baada ya kufuta ujumbe huo mpokeaji, iwe ni binafsi ama kundi la WhatsApp atapata taarifa kuwa ujumbe uliotumwa umefutwa na hatoweza kuusoma.
Hivii ndivyo itakavyoonekana kwa mpokeaji, baada ya ujumbe kufutwa katika simu ya mtumaji.
Katika simu ya mtumaji hivi ndivyo itakavyoonekana baada ya ujumbe kufutwa.