Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Luhaga Mpina ameahidi kuachia madaraka endapo tatizo la uvuvi haramu litaendelea kuwa sugu nchini.
Waziri Mpina amethibitisha hilo wakati akiteketeza nyavu zinazotumika katika uvuvi haramu zilizokamatwa mkoani Kigoma zenye thamani ya shilingi Milioni thelathini na moja.
Kama nitashindwa kushughulia suala zima la uvuvi haramu, nitaachia dhamana hii niliyopewa na Mheshimiwa Rais, lakini hadi nafikia hatua hiyo lazima wengi watakuwa wamejuruhiwa”, amesema Mpina.
Zoezi hilo la kuchoma nyavu haramu ni mwendelezo wa hatua ambazo amewahi kuzichukua rais wa jamahuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jonh Magufuli kipindi akiwa waziri wa wizara hiyo. Mpina ameahidi kuwa huo ni mwanzo tu wa zoezi hilo katika serikali ya awamu ya tano ambapo hatua zaidi zitaendelea kuchukuliwa ili kukomesha uvuvi haramu.
Aidha waziri Mpina ametoa maelekezo kwa viongozi wa Mikoa ambayo shughuli hizo zinafanyika kwa kuwataka wahakikishe wanasimamia na kulinda rasilimali za taifa ikiwa ni mapoja na Mito, Ziwa na Bahari.