Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imeendelea na utekelezaji wa agizo la Rais Dkt Magufuli la kuhamia Dodoma ambapo jana, jumla ya wafanyakazi 143 wa ofisi hiyo walihamia rasmi Makao Makuu ya Nchi, Dodoma.
Akizungumza wakati wa uhamaji, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Bi. Jane Kajiru alisema kuwa, hii ni awamu ya pili na kuhama na katika awamu hii wameigawanya katika makundi mawili.
Alisema watumishi hao 143 wameondoka pamoja na vifaa vyao na kwamba katika awamu ya kwanza, watumishi 78 walihamia Dodoma.
Bi. Kajiru alisema kwamba, awamu ya mwisho ya zoezi la kuhamia Dodoma ni mwaka ujao wa fedha 2018/19 au mara tu fedha za kuhama zitakapopatikana.
Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bibi. Dorothy Aidan Mwaluko akiagana na Kiongozi wa msafara wa magari yaliyobeba mizigo ya ofisi hiyo WOII Mohamed Bakar ikiwa ni muendelezo wa zoezi la kuhamia Dodoma leo Jijini Dar es Salaam. Jumla ya wafanyakazi 143 wameagwa katika awamu hii ya pili, ambapo awamu ya kwanza waliondoka wafanyakazi 78. Katikati mwenye miwani Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Bibi. Jane Kajiru.
Gari lililobeba nyaraka na vifaa vya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora likijiandaa kuondoka katika viwanja vya ofisi hiyo iliyopo Magogoni leo jijini Dar es Salaam. Jumla ya wafanyakazi 143 wameagwa katika awamu hii ya pili, ambapo awamu ya kwanza waliondoka wafanyakazi 78.
Baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwapungia mikono ya kwaheri madereva wa magari yaliyobeba mizigo ya ofisi hiyo ikiwa ni muendelezo wa zoezi la kuhamia Dodoma leo Jijini Dar es Salaam. Jumla ya wafanyakazi 143 wameagwa katika awamu hii ya pili, ambapo awamu ya kwanza waliondoka wafanyakazi 78. (Picha na: Frank Shija)