Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai, 2017

AUWAWA IKIWA ZIMEBAKI SIKU SABA KWAJILI YA UCHAGUZI NCHINI KENYA;

Picha
Aliyekuwa meneja wa mifumo ya mawasiliano ya kompyuta wa tume ya uchaguzi nchini Kenya (IEBC) CHRIS MSANDO auwawa na mwili wake umepatikana ukiwa umeharibika huku mkono mmoja ukiwa haupo. Ikumbukwe Tume hiyo ilitoa taarifa Jana police juu ya kutoweka gafla kwa meneja Huyo  toka siku ya ijumaa ya julai 28 mwaka huu na hakujulikana alipo. CHRIS MSANDO, ndio aliyekua msimamiza wa mfumo wa kielekroniki wa watokeo ya uchaguzi. Hii inamaana kwamba yeye ndio alikua mhakiki wa kwanza wa matokeo kabla hayajatangazwa na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi. Sababu za kifo chake hazijajulikana bado uchunguzi unaendelea RIP CHRIS MSANDO .

UJUE UMBALI WA KWENDA KWENU

Picha
UJUE UMBALI WA KWENDA KWENU 1. DAR - ARUSHA *646* KM 2. DAR - KAHAMA *1012* KM 3. DAR - BABATI via moro *876* KM 4. DAR - BARIADI *1127* KM 5. DAR - BUKOBA via kahama *1433* KM 6. DAR - DODOMA *451* KM 7. DAR - GEITA *1228* KM 8. DAR - IRINGA *492* KM 9. DAR - KIBAHA *35* KM 10. DAR - KIGOMA via itigi *1258* KM 11. DAR - KIGOMA via kahama *1476* KM 12. DAR - LINDI *452* KM 13. DAR - MBEYA *822* KM 14. DAR - MOROGORO *192* KM 15. DAR - USANGI *577*KM 15. DAR - MOSHI *566* KM 16. DAR - MPANDA via itigi *1383* KM 17. DAR - MTWARA *556* KM 18. DAR - MUSOMA *1370* KM 19. DAR - MWANZA *1152* KM 20. DAR - NJOMBE *710* KM 21. DAR - SHINYANGA *989* KM 22. DAR - SINGINDA *696* KM 23. DAR - SONGEA via moro *949* KM 24. DAR - SONGEA via lindi *1054* KM 25. DAR - SUMBAWANGA *1150* KM 26. DAR - TABORA *829* KM 27. DAR - TANGA *354* KM

Odinga atumia mgongo wa Magufuli kuomba kura Kenya

Mgombea anayepeperusha bendera ya Muungano wa NASA (National Super Alliance) katika uchaguzi mkuu wa Kenya, Raila Odinga amesema kuwa Rais Dkt Magufuli wa Tanzania atamsikiliza yeye zaidi kuliko atakavyomsikiliza Rais Uhuru Kenyatta. Akizungumza na wananchi wa Mji wa Namanga katika eneo la Kajiado Ijumaa Julai 28, alisema kuwa yeye ni rafiki wa karibu wa Rais Magufuli na hivyo atatumia urafiki huo kuhakikisha kuwa anaimarisha uhusiano baina ya Tanzania na Kenya ambao kwa sasa umeyumba kidogo kuhusu masuala ya kibiashara. Alisema pia, mara tu atakapochaguliwa kuwa Rais, Tanzania itaiondolea Kenya vikwazo ilivyoiwekea katika usafirishaji wa bidhaa. “Magufuli ni rafiki yangu, nitazungumza nae kuhakikisha kuwa mpaka huu (Namanga) unafunguliwa,”  alinikuliwa Raila ambaye amewahi kuwa Waziri Mkuu wa Kenya katika kipindi cha serikali ya mpito. Raila Odinga na Magufuli wamekuwa marafiki kwa muda mrefu sasa kitendo kilichopelekea kuwapo kwa madai kuwa Tanzania imeiruhusu NAS...

Mazoezi ya Kijeshi ya Kihistoria Kufanyika Nchini......Yanahusisha Majeshi ya Nchi 7 za SADC

Picha
Vikosi maalumu vya majeshi ya nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) vimepiga kambi kwenye eneo la mapango ya Amboni, Tanga kwa ajili ya mazoez ya kijeshi. Katika mapango hayo, mwaka jana yalitokea mauaji yaliyofanywa na watu wasiojulikana na kuzua hofu kwa wakazi wa eneo hilo ambao mwishowe walihamishwa na Serikali. Akizungumza na waandishi wa habari   jana, Mkuu wa mpango huo, Meja Jenerali Harrison Msebo, alisema vikosi hivyo vitakuwa vikifanya mazoezi katika eneo hilo kama sehemu ya kupambana na ugaidi na uharamia baharini. Kwa mujibu wa Meja Jenerali Msebo, mazoezi hayo yajulikanayo kwa jina la EX Matumbawe, yanatarajia kuanza Agosti 2 hadi Septemba mosi mwaka huu. “Mazoezi hayo yanafanyika kwa mara ya kwanza  Tanzania baada ya vikosi vya majeshi ya nchi washirika kuanza kufanya mazoezi ya pamoja kwa ajili ya kujihami dhidi ya matukio mbalimbali ya uhalifu tangu mwaka 2015. “Pamoja na mambo mengine, lengo letu ni kuhakikisha vikosi vy...

Askofu Josephat Gwajima Kashindwa Kufika Mahakamani Leo Kusikiliza Hukumu ya Kesi Yake

Picha
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Agosti 30, 2017 itatoa hukumu katika kesi ya kushindwa kuhifadhi silaha na risasi inayomkabili Askofu wa Kanisa la ufufuo na uzima, Josephat Gwajima na wenzake watatu. Hukumu hiyo ilipaswa kutolewa leo Jumatatu, Julai 31 kwa Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha lakini ilishindikana kwa sababu hakimu huyo alikuwa na udhuru. Hata hivyo, Wakili Peter Kibatala amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa wakati kesi ilipoitwa mbele yake kuwa Askofu Gwajima ni mgonjwa na mahakamani hapo amewakilishwa na mdhamini wake. Hayo yametokea baada wakili wa Serikali, Shedrack Kimaro kuiambia mahakama kuwa washtakiwa George Mzava, Msaidizi wa Askofu Gwajima, Yekonia Bihagaze (39) na Georgey Milulu wapo mahakamani lakini Askofu Gwajima hayupo. Pia, amedai kesi ilipangwa kwa ajili ya washtakiwa hao kusomewa hukumu lakini wamepata taarifa Hakimu Mfawidhi, Mkeha anayeisikiliza kesi hiyo anaudhuru. Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo kesi imeahirishwa hadi Agosti 30, 2017 ...

Malinzi na Mwesigwa Mambo Magumu.....Warudishwa Tena Rumande

Picha
Kesi inayomkabili Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, TFF, Jamali Malinzi na wenzake imeendelea leo July 31, 2017 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusogezwa tena mbele hadi August 11, 2017 kwa sababu upelelezi haujakamilika. Wakili wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi haujakamilika ambapo hata hivyo, Mawakili wa washtakiwa, James Bwana na Abraham Senguji hawakuwa na pingamizi na suala la upelelezi. Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi August 11, 2017.

Waziri Mkuu Aagiza kukamatwa kwa viongozi 12 wa Jiji la Mbeya kwa kusabaisha hasara ya Bilioni 63

Picha
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) iwakamate watendaji 12 wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya wakiwamo aliyekuwa mstahiki meya Athanas Kapuga. Amesema pia wakamatwe, wakurugenzi watatu, kaimu mkurugenzi, wahasibu wawili na wajumbe wa bodi wanne kwa kuisababishia hasara jiji hilo kiasi cha Sh63 bilioni katika ujenzi wa Soko la Mwanjelwa. Amewataka makamanda wa Takukuru kuanzia leo wawakamate watuhumiwa hao na kwamba anatuma timu kutoka ofisi ya waziri mkuu kwa ajili ya kuandaa mashtaka hayo ambapo itatua Mbeya  Jumatano.

Rais wa Simba SC, Evans Aveva na Makamu wake Geofrey Nyange ‘Kaburu’ Wapigwa Kalenda na Kurudi Rumande

Picha
Mahakama  ya Hakimu Mkazi Kisutu leo July 31, 2017 imetoa siku saba kwa upande wa mashtaka ufanye jitihada za kukamilisha upelelezi wa kesi inayowakabili Rais wa Simba SC, Evans Aveva na Makamu wake Geofrey Nyange ‘Kaburu’. Hatua hiyo imekuja baada ya Mwendesha Mashitaka wa TAKUKURU, Leonard Swai  kudai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa kuwa upelelezi wa shauri hilo haujakamilika. Upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili Mtakyamirwa Philemon ulidai mara ya nne sasa upande wa mashitaka unadai upelelezi haujakamilika na kudai wanatakiwa kuhakikisha wanakuwa makini na shauri hilo ili wakamilishe upelelezi kwani washitakiwa wako ndani kwa kosa lisilo na dhamana. Hata hivyo, Swai alidai kuwa mashitaka ya kughushi wanahitaji upelelezi wa kina hivyo anaomba Mahakama kuwapa siku 14. Hakimu Nongwa alisema Mahakama imezingatia hoja za pande zote mbili kwamba mashitaka ya kughushi yanachukua muda mrefu kukamilika na kusisitiza kuwa licha ya sheria kutaka kuahirishwa kwa kes...

Rais wa Urusi, Vladimir Putin Kawafukuza wanadiplomasia 755 wa Marekani

Picha
Rais wa Urusi, Vladimir Putin ameagiza kuondolewa wanadiplomasia na wafanyakazi 755 wa Marekani waliopo nchini humo na anafikiria kuchukua hatua za nyongeza kulipiza kisasi kwa vikwazo vya uchumi ilivyowekewa nchini hiyo. Putin alisema jana katika mahojiano ya moja kwa moja kwenye televisheni ya taifa kwamba aliagiza hatua hizo kwa sababu “alifikiri ulikuwa wakati wa kuonyesha kwamba hawawezi kubaki bila kujibu mapigo." Utekelezwaji wa agizo la usitishwaji shughuli za wafanyakazi hao wa ubalozi wa Marekani nchini Urusi unatarajiwa kuwa Septemba Mosi mwaka huu. Watabaki wafanyakazi 455. Desemba 2016, aliyekuwa rais wa Marekani, Barack Obama aliamuru kutimuliwa wanadiplomaisa 35 wa Urusi kutokana na tuhuma za Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani kupitia njia ya mtandao. Jumanne iliyopita mabunge yote mawili ya Congress ya Marekani yaliidhinisha kwa wingi wa kura vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Urusi. Mashirika ya ujasusi nchini Marekani yanaamini kuwa Urusi ilijaribu kuingilia u...

CHADEMA Yalia na Ugumu wa Maisha kwa Wananchi.....Yadai Serikali Imewatupa Wakulima

Picha
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema Serikali imeshindwa kusimamia mfumuko wa bei ya chakula nchini kwa sababu haitambui umuhimu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA). Mbowe amesema mwakà 2015, NFRA ilihifadhi tani 446,000 za chakula lakini kufikia mwaka huu wakala huyo amehifadhi tani 74,826 za chakula. Mbowe amesema chakula kinapanda bei kwa sababu hakuna mkakati wowote wa Serikali kuwainua wakulima kwa kuwapatia pembejeo za kilimo. "Usalama wa taifa ni usalama wa chakula, kama hakuna usalama wa chakula hakuna usalama wa Taifa. "Mtakubaliana na mimi kuwa kwa miaka hii miwili vitu vimepanda bei lakini kipato cha wananchi hakijaongezeka "Bei ya mahindi kwa mwakà 2015 ilikuwa ndogo lakini mwaka huu imefika zaidi ya 90,000. Wananchi wanapata shida kwa sababu Serikali yao imewatupa wakulima."  Amesema Mbowe

KIBITI Mambo Shwari: Gesti na Viwanja Vyapanda Bei

Picha
Maisha ya Kibiti sasa ni shwari hamna shari na tayari bei za vitu kama viwanja na huduma kama za nyumba za kulala wageni (gesti) zimeanza kupanda bei upya kama ilivyokuwa awali. Taarifa hiyo yenye kuashiria dalili njema za kurejea kwa amani na utulivu kwa wakazi wa wilaya hiyo iliyopo mkoani Pwani, ilithibitishwa na jeshi la Polisi kupitia kwa msemaji wake, Barnabas Mwakalukwa. Hivi karibuni, wilaya za Kibiti, Mkuranga na Rufiji mkoani Pwani, zilielekea kuwa tishio jipya la ulinzi na usalama nchini baada ya kuwapo kwa taarifa za mauaji ya kila mara ya watu wasio na hatia, wakiwamo viongozi wa vijiji, vitongoji, polisi na hata raia wa kawaida. Jumla ya watu zaidi ya 30 waliripotiwa kuuawa katika matukio tofauti ya kipindi cha takribani mwaka mmoja tu uliopita. Tishio hilo la usalama Kibiti lilisababisha baadhi ya wakazi wa wilaya hiyo kukimbia na kwenda kuishi maeneo mengine nchini na pia, taarifa zilisambaa hata kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusiana na athari za kiuchumi ...

Mtandao mpya wa vyombo vya habari vya kijamii wasajiliwa nchini

Picha
Mtandao mpya unaoundwa na Radio na vyombo vya habari vya kijamii Tanzania chini ya shirika la vyombo vya habari vya maudhui ya kijamii uliosajiliwa kwa jina la TANZANIA DEVELOPMENT INFORMATION ORGANIZATION-TADIO umeanzishwa rasmi baada ya kuvunjika kwa mtandao wa zamani wa COMNETA. Tukio hilo limetokea Julai 28, 2017 katika mkutano mkuu wa kwanza ambao pamoja na mambo mengine ulichagua safu mpya ya viongozi wa mtandao huo. Shirika la mtandao wa vyombo vya habari jamii Tanzania uliokuwa na jina la COMMUNITY MEDIA NETWORK OF TANZANIA – COMNETA, limevunjika rasmi mwezi machi mwaka huu. Katika mkutano huo kuwa kuundwa kwa shirika hilo jipya kunalenga kuhakikisha kunakuwa na mtandao makini wa Radio na vyombo vingine vilivyojikita katika kuibua kwa kuandika na kutangaza masuala ya kijamii kwa ajili ya maendeleo. Mwenyekiti mpya wa TADIO, Prosper Kwigize akizungumza jambo na wajumbe wakati wa mkutano huo. Akihutubia katika mkutano huu kaimu mkuu wa ofisi ya UNESCO Tanzania, ambao ni...

Taarifa ya serikali kuhusu filamu iliyozuiwa kuzinduliwa mkoani Geita

Picha

Idara ya Uhamiaji Yatoa Ufafanuzi Kuhusu Kukamatwa na Kuhojiwa kwa Kigogo wa Kampuni ya ACACIA Akiwa Uwanja wa Ndege

Picha

ACT Wazalendo yawakingia kifua wakulima wa korosho ......Yamtaka Waziri wa Kilimo ajiuzulu

Picha
Chama cha ACT-Wazalendo kimemtaka Waziri wa Kilimo, Dk Charles Tizeba kujiuzulu kwa kushindwa kuwapelekea wakulima wa korosho pembejeo kama alivyoahidi. Akizungumza na Waandishi wa habari, jana Julai 30, 2017 jijini Dar es Salaam, Katibu wa Itikadi na Uenezi ACT, Ado Shaibu alisema Serikali iliahidi kuwapa wakulima wa korosho dawa ya kuua wadudu sulpher bure ili waongeze uzalishaji, hivyo chama hicho kinaitaka serikali kutimiza wajibu wake kuhakikisha upatikanaji wa pembejeo na kama haiwezi kufanya hivyo itangaze taarifa halisi za upatikanaji wa pembejeo hizo kwa wakulima.    ”Sisi kama chama cha siasa kwa kuzingatia falsafa ya chama chetu cha siasa ni maendeleo tunaendelea kusisitiza kuwa serikali ni lazima itimize wajibu wake wa kulinda maisha na hali za wananchi kwa kuhakikisha hakuna uhaba wa pembejeo kwa wakulima hawa wa korosho nchini, kuhakikisha kuwa pembejeo husika zinapatikana kwa bei ambayo watanzania wanaimudu na zinapatikana kwa wakati.  "Ni mu...

CHADEMA Kumshughulikia Aliyemfukuza Mwandishi wa TBC Kwenye Mkutano wa Tundu Lissu

Picha
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kuwa, kimepokea kupitia vyombo vya habari taarifa za tukio la mwandishi wa habari wa TBC kushindwa kutimiza wajibu wake katika ofisi za Makao Makuu yake zilizopo Kinondoni, jijini Dar es Salaam. CHADEMA imesemema, tukio hilo halikufanywa kwa maelekezo ya kiongozi yeyote na kama chama, hawajawahi na hawana sera wala msimamo wa kubagua chombo chochote cha habari. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema wamesema kwamba, katika hatua za awali wanafanyia uchunguzi tukio hilo ili kuweza kubainisha nini hasa kilitokea katika siku hiyo na wanategemea kupata ushirikiano kutoka kwa mwandishi husika katika uchunguzi wao. Aidha, taarifa hiyo kutoka CHADEMA aliwahakikishia waandishi wote wa habari kuwa wataendelea kuwa salama katika matukio yote ambayo yatakuwa yakifanywa na chama hicho na watapata ushirikiano unaostahili. “Baada ya uchunguzi wetu kukamilika tutatoa...

CHADEMA Kutoa Tamko Zito Leo

Picha
Kamati Kuu ya CHADEMA   imekutana kwa siku mbili, tarehe 29 hadi 30 Julai, 2017 katika Hotel ya Double Tree, jijini Dar es Salaam kujadili hali ya siasa nchini pamoja na ukandamizwaji wa demokrasia . Taarifa iliyotolewa  jana  na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema inasema kwamba katika mambo ambayo Kamati Kuu imejadili ni pamoja na kamata kamata inayoendelea kufanywa na vyombo vya dola dhidi ya viongozi, wanachama na wafuasi wa CHADEMA maeneo mbalimbali nchi nzima. Hata hivyo kikao hicho kilijadili na kufikia maadhimio na hatua za kuchukua katika ajenda  ambapo ni pamoja na  kuporomoka kwa uchumi na hali ngumu ya maisha kwa watanzania, ambapo  taarifa kamili juu ya maadhimio hayo na hatua zitakazochukuliwa na chama itatolewa leo  Jumatatu tarehe 31 Julai 2017, kwenye kikao na waandishi wa habari kitakachofanyika jijini Dar es salaam.

RC Geita Amzuia Waziri Kuzindua Filamu Yenye Utata ya Magwangala......

Picha
Uzinduzi wa Filamu ya Magwangala  ambayo imechezwa na wasanii wa Mkoani  Geita pamoja na viongozi wa Halmashauri ya Mji   ulikuwa ufanyike siku jana (Julai 27) umekwama kutokana na kuwepo kwa madai ya Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kulalamika kuwa filamu hiyo inaonekana kuwa na mahudhui ya  uchochezi baina ya wananchi na mgodi Mkoani humo. Uzinduzi  huo ulitarajia kufanywa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura katika ukumbi wa Desire Park . Akizungumza  juu ya hatua ya kukwama  kwa uzinduzi huo Naibu Waziri  Wambura, amesema kuwa kilichotokea alipatiwa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa kwamba kuna picha ambayo sio nzuri na kwamba wao kama mgodi walilalamika juu ya picha hiyo na kwamba wameangalia na kuona kuwa kuna maeneo ambayo yamerekodiwa sio mazuri na tatizo ni mawasiliano baina ya Afisa utamaduni na Mkoa. Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha wasanii  Mkoani Humo ambaye pia ni moja kati ya wachezaji wa F...

MZEE Mkapa Yuko Sahihi,Tanzania Kuna Wajinga na Wapumbavu....

Picha
Ulishaona nchi wageni wanawafanyia wazawa mambo ya ajabu halafu baadhi ya wanainchi wanashangilia! Rais anasafishasafisha uchafu Serikalini baadhi ya wanainchi hawataki.!! Viongozi wanaiba rasilimali za nchi na Rais anahakikisha viongozi wote wa hivyo wanatimuliwa na kushtakiwa baadhi yetu wahataki Sasa tuwaitaje watu kama hao ambao kila Kitu wao hawataki. By tramadol

UCHIMBAJI Kokoto Wapigwa Marufuku Kunduchi

Picha
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imependekeza eneo la Kunduchi Machimbo lirasimishwe kuwa eneo la makazi. Taarifa ambayo imetolewa na Mkuu wa Idara ya Mipangomiji Manispaa ya Kinondoni, Maduhu Ilanga, inasema kwamba eneo hilo lilimilikishwa kwa wachimbaji mbalimbali ambao walimilikishwa kwa kupatiwa leseni za uchimbaji wa kokoto na mawe. "Eneo hilo lilikuwa na leseni za uchimbaji na leseni zake ziliisha Machi 30, 2010,'' inasema taarifa hiyo. Taarifa hiyo inasema kwamba Machi, 2006,Serikali iliamua kupiga marufuku shughuli za uchimbaji wa kokoto na mawe katika eneo la machimbo la Kunduchi, uamuzi huu wa Serikali ulifikiwa baada ya kudhihirika kuwa kulikuwa na uchimbaji usiozingatia sheria ukiendelea na kusababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu ikiwemo Barabara Kuu iendayo Bagamoyo.

MAJI Kukatwa Dar, Pwani........

Picha
Shirika la Majisafi na Majitaka jijini hapa (Dawasco) limesema kesho kutakuwa na katizo la maji kwa saa nane kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 11 jioni kwa maeneo ya mkoa wa Pwani na Dar. Katika taarifa iliyotolewa na shirika hilo leo, imeelezwa kuwa sababu ya kukata maji ni kuzima mtambo wa uzalishaji maji wa Ruvu ili kukamilisha mfumo wa umeme kwa mtambo mpya. Dawasco imesema mtambo huo wa Ruvu Juu upo Mlandizi, Pwani na kuwataka wananchi kuhifadhi maji ya kutosha katika kipindi hicho. Taarifa hiyo iliyataja maeneo yatakayoathirika na zoezi hilo kuwa ni Mlandizi Mjini, Ruvu Darajani, Vikuruti, Kilangalanga, Janga, Mbagala, Visiga, Maili 35, Zogowale, Misugusugu, Tanita, Kibondeni, Kwa Mathias, Nyumbu na Picha ya Ndege. Mengine ni Sofu, Lulanzi, Gogoni, Kibamba njia panda shule ya Kibwegere, Mloganzira, Kwembe, Kibamba Hospitali, Kwa Mkinga, Luguruni, Kimara, Ubungo na baadhi ya maeneo ya Tabata.

TANZIA...Mmiliki wa Impala Afariki Dunia

Picha
Mfanyabiashara maarufu nchini, Maleu Mrema amefariki dunia jana akiwa kwenye matibabu nchini Afrika Kusini. Akizungumza na Mwananchi ndugu wa marehemu,Vincent Laswai alithibitisha msiba huo akiwa nyumbani kwa marehemu eneo la Uzunguni jijini Arusha. Akihojiwa na gazeti hili Laswai amesema kwamba alipokea taarifa za kifo cha marehemu jana saa 12 jioni na uongozi wa familia utatoa taarifa za kifo cha mfanyabiashara huyo leo. Laswai, amesema kwamba ni mapema kuzungumzia chanzo cha kifo kwa sababu bado hawajapata taarifa kutoka katika hospitali aliyokuwa akitibiwa nchini humo. Hivi karibuni marehemu Mrema alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya kiafya ambapo Juni mwaka huu alipelekwa Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya July 31

Picha