XXL wazee wa Keko Furniture wametinga nusu fainali ya Ndondo Cup
Keko Furniture wanaopewa power na kipindi cha XXL cha Clouds FM wamekamilisha idadi ya timu nne ziluzofuzu nusu fainali ya Ndondo Cup 2017 baada ya kuifunga Stim Tosha kwa mikwaju ya penati kufuatia sare ya kufungana goli 1-1 katika dakika 90 za kawaida.
Stim Tosha ambao wapo chini ya kipindi cha Alasiri walitoka nyuma na kusawazisha bao kupitia kwa nyota wao Kelvin Sabath ‘Kiduku’ dakika ya 62 baada ya kutanguliwa na Keko Furniture kwa goli lililofungwa dakika ya 9 kipindi cha kwanza na mshambuliaji Ludovic.
Dakika 90 zikamalizika kwa sare ya timu hizo kufungana goli 1-1 kisha changamoto ya penati kuchukua nafasi yake. Keko wakafanikiwa kushinda kwa penati 4-3 na kujihakikishia nafasi ya kucheza nusu fainali ya Ndondo Cup msimu huu.
Timu ambazo zimefanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali ni pamoja na Kibada One, Goms United, Misosi FC na Keko Furniture.
Jumatatu Julai 31, 2017 itachezeshwa draw ili kupata timu zitakazokutana katika hatua ya nusu faili.
Maoni
Chapisha Maoni