SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 28 Julai 2017

T media news

Picha: Wajumbe wa Kamati ya Maadili ya Malawi watembelea Tanzania kujifunza

Wajumbe wa Kamati ya Maadili ya nchini Malawi watembelea Tanzania kujifunza utendaji kazi wa maeneo mbalimbali nchini, ikiwa ni pamoja na utendaji katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, hususan katika eneo  la utoaji huduma kwa Umma katika kupambana na Rushwa na uadilifu wa Utumishi.


Wajumbe wa Kamati ya Maadili kutoka Malawi wakiwa kwenye Mkutano na Kamati ya uadilifu ya  Wizara ya Ardhi.

Mratibu wa Kituo cha huduma kwa Mteja, Johnson Sanga akionyesha electronic queing machine ya kuhudumia wateja sawa sawa na anayewahi kufika, ambayo hutumika katika Kituo cha Huduma kwa Mteja; Kwa Wajumbe wa Kamati ya Maadili kutoka Malawi.

Kamati ya Maadili kutoka nchini Malawi ikiwa kwenye picha ya pamoja na Kamati ya uadilifu ya Wizara ya Ardhi.

Na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.