Taarifa imenifikiakwamba, yule traffic ambaye ni mdau mkubwa wa michezo na klabu ya Yanga Sgt Ally Kinyogori amepigwa risasi jana usiku akiwa nyumbani kwake.
Taarifa zinadai kwamba, mnamo tarehe May 19, 2016 Sgt Kinyogori baada ya kutimiza majukumu yake ya kikazi traffic makao makuu alirejea nyumbani kwake huko Mwandege mpakani mwa Dar es Salaam na Pwani.
Akiwa sebuleni kwake majira ya saa 3 usiku, watu wasiojulikana waliingia ndani na kumpiga risasi moja kifuani na nyingine ubavuni kisha kutoweka bila kuchukua kitu chochote. Alikimbizwa hospitali akiwa hajitambui.
Kinyogori alikuwa karibu na viongozi na wadau mbalimbali wa michezo na alikuwa makitoa msaada mkubwa pale timu zinapokwama kwenye foleni kwa kuwasiliana na askari waliokaribu na eneo husika pindi anapopokea taarifa kutoka kwa viongozi wa timu husika.