SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 28 Mei 2016

T media news

Real vs Atletico: Fainali nyingine ya ulaya bila namba 10

Wachezaji wakubwa hucheza mechu kubwa, na kawaida baadhi ya wachezaji wakubwa duniani huvalia jezi namba 10 katika timu zao, namba ambayo ina ukubwa wake katika historia ya soka hasa zaidi katika michezo ya fainali – lakini leo usiku haitokuwa siku ya jezi namba 10.

 
 Usiku wa leo kwenye fainali ya Champions League sio Oliver Torres wala James Rodriguez atakayepata nafasi ya kuanza kwenye mchezo wa usiku wa leo.

James itambidi kusubiri nafasi yake katika benchi la Madrid – hali ambayo imekuwepo kwa msimu huu wote baada ya kupoteza nafasi ya kuanza katika Kikosi cha kwanza tangu Zidane alipochukua madaraka ya benchi la ufundi. 

 
 Oliver, kwa upande wake, anaweza hata asiwepo kwehye benchi, hayupo kwenye mipango ya Diego Simeone na huenda akaondoka kwenye klabu hiyo wakati wa dirisha la usajili litakapofunguliwa.

Katika fainali ya Champions League iliyopita iliyowakutanisha mahasimu hawa, hakuna mchezaji aliyevaa namba 10 pia kwenye fainali, Ozil alishaondoka Madrid na Arda Turan nae alikuwa majeruhi hivyo hakuweza kushiriki kwenye mechi hiyo.

 
 James amecheza dakika 28 tu katika fainali katika mechi 4 za Champions League zilizopita, wakati Oliver mechi yake ya mwisho kucheza kwenye UCL ilikuwa katika hatua ya 16 bora vs PSV Eindhoven.