Mamlaka ya kukusanya kodi TRA kupitia madalali wa Yono Auction Mart wamekusanya mali za bilioni 3 pamoja na kutaifisha mali za bilioni 10 kutoka kwa wafanyabiashara waliopitisha makontena 329 kupitia bandari kavu ya Azam bila kulipa kodi na bado wanaendelea na msako bara na visiwani.
Madalali hao wamesema watu walipe kodi na watoe risiti za elekroniki la sivyo mali zitakamatwa.