MAJONZI NA VILIO VYATAWALA KUAGWA DADA WA BILIONEA MSUYA



Waombolezaji wakiaga mwili wa marehemu Anathe Msuya





Dada wa marehemu wakiaga mwili wa ndugu yao.





M toto wa marehemu Anathe, Allan Kimario (aliyelala).





Majonzi na huzuni vimetawala kwenye tukio la kuagwa kwa mwili wa mdogo wa Bilionea Erasto Msuya aliyeuawa kwa risasi mwaka 2013, Anathe  Simon Msuya ambaye yeye aliyeuawa kwa kuchinjwa nyumbani kwake Kigamboni jijini Dar, Mei 25 mwaka huu.

Mamia ya waliofika katika Kanisa la KKKT Usharika wa Mashariki, Salasala jijini Dar wakiwemo wafanyakazi wenzake wa Wizara ya Fedha alikokuwa akifanya kazi marehemu, walishindwa kujizuia kuangua vilio walipokuwa wakipita mbele ya jeneza lililokuwa na mwili huo kutoa heshima zao za mwisho.

Mtoto wa Anathe aliyetajwa kwa jina la Alan Kimario (4) alionekana akilazimishwa kwenda kuuaga mwili wa mama yake kwani alikuwa akitaka aachwe aendelee na michezo yake kutokana na ukweli kwamba, alikuwa hajui hata kinachoendelea.

Mwili wa marehemu Anathe umesafirishwa kwenda Mererani jijini Arusha kwa ajili ya maziko yanayotarajiwa kufanyika kesho (Jumanne).

 Mungu ailaze roho ya marehemu Anathe mahali pema peponi. Amin!

PICHA NA DENIS MTIMA/GPL

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: UTAMU WA MADAM JESCA

Simulizi; MTOTO WA BOSS WANGU

SIMULIZI FUPI: UCHI WANGU UMENIPONZA