SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 23 Mei 2016

T media news

WEMA AZINDUA MOBILE APLICATION YAKE, HABARI ZAKE ZITAPATIKANA HUMO


 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye pamoja na  Miss Tanzania 2006 na Muigizaji maarufu wa Filamu nchini Wema Sepetu wakifunua pazia  kuashiria uzinduzi rasmi wa Wema Sepetu Mobile Application ya msanii Wema Sepetu  kwenye hoteli ya Hyyat Regency jijini Dar es salaam jana ,Katika Aplication hiyo kutapatikana habari mbalimbali za msanii huyo mwigizaji wa filamu pamoja na habari zinazohusu masuala mbalimbali ya kazi zake hii ni kwa mara ya kwanza katika nchi za Afrika Mashariki kwa msanii kuwa na Mobale Aplication yake hivyo msanii mwingine atakayekuja atakuwa anafuata nyayo za Wema Sepetu.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akimpongeza msanii  Wema Sepetu mara baada ya kuzindua Mobile Application ya msanii huyo jana.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akihutubia wakati wa uzinduzi wa Wema Sepetu Mobile Application ambapo alimpongeza Wema kwa hatua kubwa aliyofikia ya kuwa msanii wa kwanza wa Filamu nchini kuwa na Mobile App na kuwataka wasanii wengine kuwa wabunifu na kuja na mipango ambayo itawanufaisha zaidi.


Msanii wema Sepetu akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mobale Aplication yake kwenye hoteli ya Hyyat Regency.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akimpongeza msanii  Wema Sepetuwakipiga picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi huo.


Mtaalamu wa Mobile Application Ndugu Haji Yussuf akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wema Sepetu Mobile Application


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza jambo na Miss Tanzania 2006 na Muigizaji maarufu wa Filamu nchini Wema Sepetu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akipiga picha ya pamoja na Miss Tanzania 2006 na Muigizaji maarufu wa Filamu nchini Wema Sepetu 


Mama yake Wema Sepetu pamoja na baadhi ya wageni waalikwa wakijiunga na huduma hiyo.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akipiga picha ya pamoja na Miss Tanzania 2006 na Muigizaji maarufu wa Filamu nchini Wema Sepetu na mama yake kushoto pamojaMkurugenzi wa Biashara wa kampuni ya Hartman Traders Ndugu Cecil  na Mtaalamu wa Mobile Application Ndugu Haji Yussuf wa pili kutoka kushoto wakati wa uzinduzi wa mobile Application yake ambayo itawasaidia wapenzi na mashabiki wake kupata habari sahihi na za uhakika.